Ugomvi wa JK, Lowassa waiua CCM: Lusinde, Mwigulu wapigwa stop mikutano ya kampeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugomvi wa JK, Lowassa waiua CCM: Lusinde, Mwigulu wapigwa stop mikutano ya kampeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 5, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  • LUSINDE, MWIGULU WAPIGWA STOP MIKUTANO YA KAMPENI

  Na Martin Malera

  UHASAMA wa kisiasa na kikazi baina ya wanasiasa wawili waliopata kuwa maswahiba wakubwa, Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, unatajwa kuwa kiini cha kuzorota, kuyumba na kuporomoka kwa mvuto wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake machoni mwa jamii, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

  Taarifa ambazo Tanzania Daima Jumatano limezikusanya kutoka katika vyanzo anuai vya kuaminika ndani ya serikali na katika duru za CCM zinaeleza kwamba uhasama kati ya wanasiasa hao umevuta wapambe wa kila namna kwa kila upande unatajwa kuwa sababu ya mkwamo wa kiutendaji na kiuwajibikaji ndani ya serikali na hata miongoni mwa viongozi wa juu wa chama tawala.  Baadhi ya viongozi wa juu wa serikali na wale wa CCM waliozungumza na gazeti hili, wameyahusisha matukio ya hivi karibuni ya kuanguka kwa chama hicho tawala katika uchaguzi mdogo za ubunge kule Arumeru Mashariki na zile za udiwani katika nane zilizofanyika mwishoni mwa wiki zimetajwa kuwa yanachagizwa na hali hiyo.  “Katika kipindi cha miaka inayokaribia minne ya utawala wa Rais Kikwete utendaji wa kazi serikalini na mshikamano wa kikazi na kisiasa ndani ya taasisi za dola na za kisiasa umezorota kwa sababu tu watu wawili waliokuwa marafiki wakubwa wamekosana na kusababisha mpasuko mkubwa wa kiuwajibikaji,” alieleza mmoja wa wanasiasa ambaye amefanya kazi kwa karibu na wanasiasa hao wote wawili.  Kwa mujibu wa mwanasiasa huyo ambaye hivi sasa ni mstaafu, hali hiyo ya uhasama imesababisha serikali igote katika kutekeleza ahadi zake na wakati huohuo viongozi wa CCM wakipwaya kuchukua maamuzi stahili kwa sababu ya kuibuka kwa makundi yenye uhasama mkali yote ama yakiwa upande wa Rais Kikwete na mengine upande wa Lowassa.
  “Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ile ya mwaka 2005 na hata ya mwaka 2010 umekwama kwa sababu hoja zimeelekezwa zaidi katika kuwindana na kumalizana kisiasa.  “Mara usikie kundi la Lowassa likijipanga kumuangusha Rais Kikwete kwa kumng’oa kwanza katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na baadaye tukasikia katika uenyekiti wa taifa kabla ya upepo kubadilika na kumsikia Rais akiibuka na nadharia ya kujivua gamba ambayo ilisemekana kumlenga Lowassa na kundi lake. Katika hali ya namna hii serikali na chama vyote vinakwama na hilo ndilo lililotokea,” anaeleza kada mwingine wa CCM na kiongozi wa serikali aliyezungumza na gazeti hili.  Mchambuzi mwingine wa masuala ya siasa anauelezea uhasama wa kisiasa na kikazi wa Kikwete na Lowassa kuwa msingi wa baadhi ya wasaidizi wa Rais ndani ya serikali na wale walio CCM kushindwa kuchukua maamuzi ya msingi, kwa sababu ya hofu ya kuogopa kuonekana wakiwa ama upande wa Rais au wa ‘mgomvi’ wake huyo wa kisiasa.  Mchambuzi mwingine wa masuala ya siasa anasema mlolongo wa matukio yanayohusisha uhasama wa wanasiasa hao wawili unaweza ukawa kiini kikuu cha baadhi ya wazee wa chama hicho kufikia hatua ya kuitabiria kifo CCM.  Kwa mujibu wa mchambuzi huyo, ingawa anguko la CCM lilitabiriwa pia muda mrefu na makada mbalimbali akiwemo marehemu Horace Kolimba, hata kabla ya Kikwete na Lowassa kuingia madarakani, mahusiano ya kikazi kati ya wanasiasa hao wawili yanaweza yakawa chagizo la kupoteza dira kwa CCM na serikali yake.  Mchambuzi huyo anaendelea kueleza kuwa kile kilichotokea Arumeru Mashariki tangu katika hatua ya uteuzi wa mgombea wa CCM hadi wakati wa kampeni ni kielelezo cha kushamiri kwa uhasama kati ya wanasiasa hao wawili ambao sasa umechukua sura ya muonekano halisi wa siasa za zama hizi.  “Hivi nani hajui namna jina la Lowassa lilivyohusishwa na uteuzi wa mgombea wa CCM Arumeru. Je kuna mtu hajui kwamba hata ule uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kuamuru kurejewa kwa uteuzi wa mgombea wake ulimlenga zaidi Lowassa huyohuyo? Katika hali ya namna hiyo ulitarajia kampeni za ndani ya chama zingekuwaje?” anahoji mchambuzi huyo.


  Kada mwingine wa CCM aliyezungumzia suala hilo alifikia hatua ya kusema kwamba uhasama kati ya wanasiasa hao wawili na makundi yao ndiyo msingi mkubwa wa makada kadhaa ndani ya chama hicho kufikia hatua ya kushangilia ushindi wa CHADEMA Arumeru ikiwa ni namna yao ya kumng’ong’a Lowassa.


  “Tumewasikia viongozi wa juu wa CCM (anawataja kwa majina) wakishangilia kushindwa kwa Sioi Sumari katika kinyang’anyiro cha ubunge Arumeru. Kimsingi si ajabu hata chama kimefikia hatua ya kukubali harakaharaka kushindwa kwa kuwa kinaliona tukio hilo kuwa linalomgusa zaidi Lowassa na kundi lake kuliko ilivyo kwa mwingine yeyote,” anaeleza kada huyo wa CCM.  Mtu mwingine aliye karibu na Lowassa ameieleza Tanzania Daima Jumatano kuwa wakati akirejea jijini Dar es Salaam juzi mwanasiasa huyo alisikika akizungumza kupitia katika simu yake ya kiganjani akieleza kusononeshwa na hatua ya baadhi ya wana CCM kuzihujumu kampeni za Arumeru lengo likiwa ni kumuumiza yeye.  “Nilikuwa karibu na Lowassa pale KIA (Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro) na kikamsikia akisema maneno haya, ‘tumehujumiana na kumalizana wenyewe ndani ya chama’ kabla ya kukata simu,” alieleza mtu huyo.  Kada mwingine wa CCM ameieleza Tanzania Daima Jumatano kuwa chama chao kimepoteza mvuto kwani katika jimbo la Arumeru Mashariki, wengi walioipigia kura CHADEMA ni wafuasi na wapenzi wa CCM ambao miaka miwili iliyopita ndiyo waliompigia kura marehemu Jeremiah Sumari.  “Kwenye uchaguzi wa 2010 Joshua Nassari alipata kura 19,123 huku marehemu Jeremiah Sumari akiongoza kwa kupata kura 34,661. Tofauti kati yao ni kura 15,538.  “Kwenye uchaguzi huu wa juzi Nassari amepata kura 32,972 wakati Siyoi (Sumari) amepata 26,757 tofauti kati yao ikiwa ni kura 6,215.

  Ukiangalia unaweza kuona vitu vitatu vya haraka haraka. Kwanza, kura zilizopatikana kati ya wagombea wawili wa CCM na CHADEMA kulinganisha na 2010 zimeongezeka kwa kura 5,945.  “Jambo la pili linatokana na hilo la kwanza; mgombea wa CCM hii juzi (Sumari) amepata kura chache kuliko mgombea wa CCM mwaka 2010 akiwa na kura pungufu ya kura 7,904. Tukichukua tofauti ya kura pungufu alizopata Sumari na kulinganisha na kura zaidi alizopata mgombea wa CHADEMA tunaweza kuona kuwa tofauti kati yao ni kura 1,689.  “Hii kwa kuangalia tunaweza kusema kwa uhakika mkubwa kuwa Nassari asingeweza kushinda kwa kishindo hivyo bila kuungwa mkono na wana CCM! Unaweza kuuliza unajuaje ni wana CCM? Ndiyo! Watu wenye kupiga kura huwa wanajitokeza tena kupiga kura watu wasio na kawaida ya kupiga kura, hawapigi kura hata uitishe uchaguzi mara ngapi! Kiasi kikubwa cha waliopiga kura 2010 watakuwa wamepiga kura tena juzi ila kati yao wapo wengi zaidi waliohama kutoka CCM kwenda CHADEMA na hii ni hatari kwa chama chetu,” alisema kada huyo.  Kwa mujibu wa kada huyo, kama CCM itachukulia kushindwa huku kuwa ni kushindwa kwa kawaida basi hawajui kinachowasubiri.


  Timu ya kampeni ya CCM lawamani

  Pamoja na sababu nyingine za kushindwa kwa CCM, chama hicho kimeshusha lawama kwa timu ya kampeni iliyoendesha mikutano ya kumnadi mgombea wao Arumeru.


  Lawama nyingi zinaelekezwa kwa Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, ambaye amekuwa akilaumiwa kwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya viongozi wa CHADEMA.  “Ile timu ya kampeni sijui iliteuliwa na nani, lakini tukiri kwamba hatukuwa na timu nzuri ya ushindi kuanzia meneja wa kampeni, Mwigulu Nchemba, Lusinde na wengine na wakati mwingine hawawezi kwenda kwenye kampeni,” alisema.  Hatua ya Lowassa kuamua kuingia kwenye kampeni za majukwaani ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipojiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu kutokana na kuguswa na ufisadi wa kampuni ya Richmond, imeelezwa kuwa imechangia pia kuanguka kwa chama hicho katika uchaguzi huo.  Ingawa chama hicho kimetangaza kuipongeza CHADEMA kwa ushindi, kinatarajia kukaa na kufanya tathmini kubaini chanzo cha anguko hilo, huku kikikamia kutekeleza maazimio yake ya kuwavua gamba makada wake wanaotuhumiwa kwa ufisadi.  Wakati huohuo mamia ya vijana wafuasi wa CHADEMA, wamejiandikisha kwenda mkoani Dodoma kumsindikiza mbunge wao mteule, Nassari anayetarajiwa kuapishwa rasmi kushika kiti hicho.  Habari zinasema kuwa CHADEMA imekodi magari maalumu kwa ajili ya wanachama na wafuasi wa CHADEMA wanaotaka kuambatana na mbunge huyo mteule.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Masikini Mwingulu hatahudhuria Mikutano ya CCM? sasa hizo skuf zake zitakwenda wapi jamani?

  Ilikuwa fashion ya aina yake nchini wengi tulianza kuiga kwa upande wa upinzani!!!
   
 3. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hata Kabla ya ugovi wa hao wanasiasa wawili. Mambo kwenye serikali ya ccm hayajawahi kuwa mazuri! Kwani watu wana matatizo mengi, na hayajawahi kutatuliwa hata kabla ya hao akina JK na EL!
   
 4. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Teh teh....
   
 5. S

  STIDE JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wasimlaumu Mwiguru, wamlaum aliemteua!! Lakini pia ukimulika tochi ndani ya magamba ni nani aliebora zaidi ya hawa?
   
 6. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Lowasa arudi akachunge,mwigulu akavune mtama,lusinde akavue bwawa la mtera
   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mi natamani ccm itoweke ktk fikra ya Watanzania!

  Mafisadi hawana jipya tena!
   
 8. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,000
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Wameshaanza kushikana uchawi wenyewe kwa wenyewe,ngoja tusubiri tuone nani mwisho wao,
  sisi kimya tunaendelea kuwasoma udhaifu wao tu.
   
 9. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Lawama nyingi zinaelekezwa kwa Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, ambaye amekuwa akilaumiwa kwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya viongozi wa CHADEMA.
  "Ile timu ya kampeni sijui iliteuliwa na nani, lakini tukiri kwamba hatukuwa na timu nzuri ya ushindi kuanzia meneja wa kampeni, Mwigulu Nchemba, Lusinde na wengine na wakati mwingine hawawezi kwenda kwenye kampeni," alisema.

  Wamesahau mchango mkubwa wa Mkapa na Wasira katika kuwanyima CCM kura
   
 10. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,335
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  CCM wataendelea kula matapishi yao wenyewe
   
 11. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mfa maji... Mbona kule Igunga mwigulu huyu huyu alisifiwa?
  Watambue ccm imefika mwisho, ilo ndo la msingi.
  Kwa hiyo ishu ya JK muda wote anaoutumia kuzurura nchi za nje nalo ni swala la ugomvi wake na EL? Kwa hiyo EL anamtisha asikae pale ikulu?
  Pia matatizo ya umeme, mdororo wa uchumi nao unasababishwa na bifu lake na EL?
  Hao ccm watumia akili kufikiri, m/kiti wao ndo hamna kitu... Wasitafute mchawi.
   
 12. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ha ha ha ha
   
 13. n

  nyabwai Member

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Hakuna cha mchawi Mwingulu wala Lusinde wala Ma watermelon kwenye uchaguzi na hata ndani ya CCM. Laana ya BABA WA TAIFA INAWATAFUNA. Marehemu baba wa Taifa ililiona aunguko la CCM na aliwambia Upunzani wa kweli hautatoka nje, Utatoka ndani ya CCM na utakuwa na Nguvu.

  Sasa wao waendelee tu kuwa wavivu wa kufikiri na kutafakari. Na isitoshe watu wamechoka chama na serikali visivyo wasikiliza wananchi wanataka nini jamani wanatupeleka tu wanavyotaka wao. Nina asiyejua kuwa rushwa ilitembezwa wakati wa kura za maoni katika kutafuta mgombea wa CCM.

  Wametumia gharama kiasi gani kutoa rushwa ili mtu wao ashinde. Hiyo pesa si wangeliwachimbia basi hata visima vya maji au kujenga hospitali itakayokidhi mahitaji yao. Nusu ya waliojiandikisha kupiga kura hawakupiga kwa nini, sasa hapo ile mbinu chafu ya CCM kununua hati za kupigia kura pia imekigharimu chama dhambi nyingine hiyo.
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Nilichoona na nilichosoma ni kwamba Lusinde na Nchemba wamelaumiwa tu kwa kutumia lugha ya matusi na kutokuwa organized, which means wanaweza kuendelea kupanda jukwaani.
  Hata hivyo ccm watakuwa wanawaonea tu hao vijana, maana kama ni matusi kila mwanaccm akiwemo wassira, mkapa, na hata lowassa wote walitumia lugha ya matusi.
  Anguko la ccm halitokani na vita ya wababe hao wawili yaani Jk na EL, bali kutokana na ccm kushindwa kuwatumikia wananchi.
   
 15. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  ATTENTION:Hao ni wagonjwa!
  Wawahishwe Mirembe kwa matibabu
   
 16. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Katika chaguzi ndogo zilizofanyika jumapili ukiondoa arumeru, CCM ilipata kura nyingi zaidi ya CDM. ARUMERU TATIZO NI TIMU NZIMA, KUANZIA MGOMBEA AMBAYE HAJULIKANI, MPAKA WAPIGA POROJO AMBAO WALIKUWA HAWANA CHA MAANA WALICHOZUNGUMZA.
   
 17. 911

  911 Platinum Member

  #17
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Adui wakigombana shika jembe ukalime,wakipatana......
   
 18. MBUTAIYO

  MBUTAIYO JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Hiyo team ya kampeni ndio cream ya ccm ambayo Nape alisema ni watu maalum watakaoalikwa, wasioalikwa hawataruhusiwa kupiga kampeni, EL alialikwa?
  Na sasa itakuwaje chaguzi zijazo wakati wanawatosa mabingwa wa kampeni?
   
 19. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #19
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Lizaboni, Kiwira na Kirumba CHADEMA walishinda. sasa hizo kura nyingi walizipata wapi?
  Point ni kwamba CCM hata kura walizopata Arumeru wasingezipata kama si baadhi ya wapiga kura kuwalipa fadhila kutokana na mgawo waliokuwa wamepokea.
  Wangepiga kampeni kavu kavu kama chadema bila kugawa pesa na kutembea na TOT na Comedy CCM wangeambulia asilimia labda 20 tu za kura.
  Huko kwingine unakosema ccm walipata kura nyingi labda unazungumzia Dar, ambapo watu wa huko bado wanahitaji elimu ya demokrasia, ambapo CHADEMA sasa wapo njiani kuwaelimisha, ikiwa ni pamoja na mikoa ya kanda ya pwani waliopandikizwa mbegu mbaya ya udini na CCM.
   
 20. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu kingine ambacho CCM wamesahau au wanaona uoga kukiongelea kama sababu ya anguko:
  1. Mkapa kuanzisha mipasho na kupiga umbeya kama ladies badala ya kufanya kilichomleta Arumeru. Ukweli ni kwamba malumbano ya Vicent Nyerere na Mkapa umempunguzia umaarufu sana Mkapa na kushusha kwa kiasi kikubwa kura za CCM baada ya kugundulika na watu woote hata watoto wadogo wa Arumeru kuwa Mkapa hakuwa na na data na hivyo alidanganya.

  2. Kuwadanganya wananchi kuhusu EPZ(Mary Nagu), Kuwa eti Mbunge wa CHADEMA hawezi kupata support ya serikali wakati ni uongo(Wassira, Mchemba, Nagu na Lusinde ?

  3. Kumleta mganga wa kienyeji (Maji Marefu)kumpigia Sioi kampeni ili kuwatisha wananchi wakati CCM ikijua watu wa kaskazini wanamtegemea Mungu na hawaogopi uchawi bali wachawi na waganga ni watu wa wanadharauliwa.

  4. Fisadi kuhusika kumnadi mkwe wake na watu wakaogopa kuwa mgao wa umeme unaweza kuanza tena kutokana na kuwa na kumbukumbu chungu ya mathila ya Richmund ambayo author wake ni Edward Lowassa.


  CCM kuendelea kufikia kuwa eti wamekosa ubunge kutokana na tofauti ya JK na Lowassa watakuwa wanadhihirisha wana mtazamo finyu sana kuhusu kukubalika kwao kwa jamii. Naomba Mungu aendelea kuwapa upofu wa fikra CCM ili ifikapo 2015 washangazwe na WATZ.
   
Loading...