Ugomvi wa Gazeti la Bingwa na Simba ulianzia wapi?

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Mimi ni mwanamichezo si mshabiki wa team yoyote. Nimekuwa nikifuatilia kwa kina jambo moja ambalo nlishawahi kudokezewa kwa kifupi tu.

Kuwa gazeti la dimba halina mahusiano mazuri na simba jambo ambalo limekuwa likifanya gazeti hilo kuandika kwa chuki na wakati mwingine ushabiki.story ya leo ilinifanya haraka sana nimtafute okwi kijua kuna ukweli gani katika kilichoandikwa. Alishangaa sana....na aliongea kwa hasira kwa nini gazeti hilo limwandike vibaya hivyo na hajawahi hata kuongea nalo na hana tatizo lolote zaidi ya ugonjwa ambalo linafahamika toka team yake ya taifa akiwa uganda.

*SIMBA SPORTS CLUB*
*DAR ES SALAAM*
*4/1/2017*

*TAARIFA KWA UMMA*

Klabu ya Simba inapenda kukanusha taarifa iliyoandikwa na Gazeti la leo la Bingwa la tarehe 4-1-2018, iliyotoka na kichwa cha habari kikubwa kwenye ukurasa wake kwanza, iliyoandika *_OKWI, KWASI WAIGOMEA SIMBA._*

Taarifa hiyo inaeleza wachezaji hao Emmanuel Okwi na Asante kwasi hawatacheza hadi walipwe fedha zao za usajili.

Kiukweli taarifa hiyo imejikita kwenye kuharibu taswira ya klabu,na yenye nia ovu kwa timu yetu ambayo ipo kwenye mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayoendelea huko Zanzibar kwa sasa.

Mara kwa mara gazeti hilo limekuwa likiandika taarifa za namna hiyo kwa klabu,hali inayopelekea uongozi wa Simba kulaumiwa na Wanachama wake juu ya mwenendo wa taarifa zinazotolewa na chombo hicho kilichopo chini ya kampuni ya Habari Co-operation.

Binafsi nimekuwa mara kwa mara nikijaribu kuwasiliana na wahariri wa magazeti ya kampuni hiyo ili kujaribu kuweka sawa taarifa zao,lakini kwa sababu wanazozijua wao kumekuwa hakuna mabadiliko yoyote.

Kwa taarifa iliyoandikwa leo ambayo imezua taharuki kubwa hususan mitandaoni,klabu imeonelea iliweke sawa kwa kuwaambia Wanachama na washabiki wake kuwa,haidaiwi na mchezaji yoyote pesa yoyote si tu ya usajili hata za mishahara.

Hivyo imelitaka gazeti hilo kuthibitisha taarifa yao ndani ya siku mbili au kukanusha kwa uzito ule ule taarifa yao iliyojaa upotoshwaji usiovumilika.

Vinginevyo klabu ya Simba itachukua hatua stahiki kwa gazeti,mwandishi,mhariri na kampuni hiyo ambayo tunaiheshimu sana.

Tupende pia kuwaarifu pia mchezaji Emmanuel Okwi ataonekana uwanjani hivi karibuni baada ya ruhusa yake ya matibabu kumalizika,
huku Kwasi akiendelea kuitumikia klabu kama mlivyoona leo kwenye mchezo dhidi ya Jamhuri toka kisiwani Pemba.

Kukosekana kwa Kwasi juzi kwenye mchezo dhidi ya Mwenge kulitokana na maamuzi ya benchi la ufundi na kuandikwa jina lake kwenye kikosi, kulitokana na makosa ya kiuandishi kama ambavyo wao gazeti la Bingwa linavyokosea(errors ).

Matarajio yetu ni kuona jambo hili halitajirudia tena na tuna mategemeo makubwa kuona masasahihisho haya yanafanyika kwa wakati kama tulivyoandika huko juu.

*IMETOLEWA NA....*

*HAJI S MANARA*
*Mkuu wa Habari*
*SIMBA SPORTS CLUB*

*SIMBA NGUVU MOJA*
IMG-20180104-WA0015.jpg
 
swali lingekuwa hivi SIMBA ni kwanini kila wakati huwa wanakuwa na shida ya kumalizia kuwalipa wachezaji wao hela za usajiri hasa kipindi hiki ambacho MO DEWJI kasema kawapa bili moja ya usajiri
 
Nmeulizia hiyo habari. Kwa mtu wa ndani kabisa ambaye naye ni jamaa yangu nikitaka tu uthibitisho. Ni habari ambayo haina ukweli.na si mara ya kwanza kuna na tatizo kama hili. Anyway nachotaka kusema ni kuwa kuna baadhi ya magazeti waandishi au wamiliki wake walishaamua kushabikia simba na wengine yanga.hii si nzuri kwa tasnia ya habari.

Gazeti linavyanzo vingi vya kupata habari hivyo sio lazima wazungumze na Okwi ndipo wachapishe gazetini.
Hiko kichwa cha habari bado hakithibitishi kama kunatofauti kati ya gazeti na simba au la! Labda kama ndani kuna maelezo tofauti na heading.
 
Bingwa au dimba nayo ni magazeti ya kusoma?mie nasoma blogs tu za watu kwa mbali na kwakujilazimisha husoma championi na mwanaspoti ingawa kwa mwaka huu sijayasoma pia,tanzania vyanzo vya habari magumashi na inahitaji moyo sana.
 
*SIMBA SPORTS CLUB*
*DAR ES SALAAM*
*4/1/2017*

*TAARIFA KWA UMMA*

Klabu ya Simba inapenda kukanusha taarifa iliyoandikwa na Gazeti la leo la Bingwa la tarehe 4-1-2018, iliyotoka na kichwa cha habari kikubwa kwenye ukurasa wake kwanza, iliyoandika *_OKWI, KWASI WAIGOMEA SIMBA._*

Taarifa hiyo inaeleza wachezaji hao Emmanuel Okwi na Asante kwasi hawatacheza hadi walipwe fedha zao za usajili.

Kiukweli taarifa hiyo imejikita kwenye kuharibu taswira ya klabu,na yenye nia ovu kwa timu yetu ambayo ipo kwenye mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayoendelea huko Zanzibar kwa sasa.

Mara kwa mara gazeti hilo limekuwa likiandika taarifa za namna hiyo kwa klabu,hali inayopelekea uongozi wa Simba kulaumiwa na Wanachama wake juu ya mwenendo wa taarifa zinazotolewa na chombo hicho kilichopo chini ya kampuni ya Habari Co-operation.

Binafsi nimekuwa mara kwa mara nikijaribu kuwasiliana na wahariri wa magazeti ya kampuni hiyo ili kujaribu kuweka sawa taarifa zao,lakini kwa sababu wanazozijua wao kumekuwa hakuna mabadiliko yoyote.

Kwa taarifa iliyoandikwa leo ambayo imezua taharuki kubwa hususan mitandaoni,klabu imeonelea iliweke sawa kwa kuwaambia Wanachama na washabiki wake kuwa,haidaiwi na mchezaji yoyote pesa yoyote si tu ya usajili hata za mishahara.

Hivyo imelitaka gazeti hilo kuthibitisha taarifa yao ndani ya siku mbili au kukanusha kwa uzito ule ule taarifa yao iliyojaa upotoshwaji usiovumilika.

Vinginevyo klabu ya Simba itachukua hatua stahiki kwa gazeti,mwandishi,mhariri na kampuni hiyo ambayo tunaiheshimu sana.

Tupende pia kuwaarifu pia mchezaji Emmanuel Okwi ataonekana uwanjani hivi karibuni baada ya ruhusa yake ya matibabu kumalizika,
huku Kwasi akiendelea kuitumikia klabu kama mlivyoona leo kwenye mchezo dhidi ya Jamhuri toka kisiwani Pemba.

Kukosekana kwa Kwasi juzi kwenye mchezo dhidi ya Mwenge kulitokana na maamuzi ya benchi la ufundi na kuandikwa jina lake kwenye kikosi, kulitokana na makosa ya kiuandishi kama ambavyo wao gazeti la Bingwa linavyokosea(errors ).

Matarajio yetu ni kuona jambo hili halitajirudia tena na tuna mategemeo makubwa kuona masasahihisho haya yanafanyika kwa wakati kama tulivyoandika huko juu.

*IMETOLEWA NA....*

*HAJI S MANARA*
*Mkuu wa Habari*
*SIMBA SPORTS CLUB*

*SIMBA NGUVU MOJA*

swali lingekuwa hivi SIMBA ni kwanini kila wakati huwa wanakuwa na shida ya kumalizia kuwalipa wachezaji wao hela za usajiri hasa kipindi hiki ambacho MO DEWJI kasema kawapa bili moja ya usajiri
Unategemea Okwi aseme amegoma?
Gazeti linavyanzo vingi vya kupata habari hivyo sio lazima wazungumze na Okwi ndipo wachapishe gazetini.
Hiko kichwa cha habari bado hakithibitishi kama kunatofauti kati ya gazeti na simba au la! Labda kama ndani kuna maelezo tofauti na heading.
Yanga Bigwa Mara 27
 
Kuanzia leo hii sisi wanachama wa Simba na mashabiki tutahamasishana Nchi mzima Kwa kulisusia gazeti la bingwa .hatutalisoma Wala kulinunua gazeti hilo..

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
Kama wameandika habari za uongo na ukweli upo na unaweza ukadhibitishwa kwanini wasiwafungulie mashtaka
 
Gazeti linavyanzo vingi vya kupata habari hivyo sio lazima wazungumze na Okwi ndipo wachapishe gazetini.
Hiko kichwa cha habari bado hakithibitishi kama kunatofauti kati ya gazeti na simba au la! Labda kama ndani kuna maelezo tofauti na heading.
Soma vizuri
 
swali lingekuwa hivi SIMBA ni kwanini kila wakati huwa wanakuwa na shida ya kumalizia kuwalipa wachezaji wao hela za usajiri hasa kipindi hiki ambacho MO DEWJI kasema kawapa bili moja ya usajiri
Churwa analima matikiti huko Zambia unajua sababu ni Nini?? Donald ngoma anaye anachunga mbuzi sijui wapi Huko unajua sababu ni Nini??
 
Mara nyingi hawa wachezaji mastaa wanasumbua sana nakumbuka hata niyonzima aliwahi kusumbua yanga wakataka kumtema ndio akaomba msamaha.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom