Ugomvi wa familia ya Nyerere na serikali wiki za mwisho wa uhai wa Julius Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugomvi wa familia ya Nyerere na serikali wiki za mwisho wa uhai wa Julius Nyerere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SubiriJibu, Mar 23, 2012.

 1. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,131
  Likes Received: 779
  Trophy Points: 280
  Maria Nyerere asidhani anaweza kuwafanya wote tusikumbuke yaliyotokea London wakati Nyerere yuko mahututi kitandani.

  Kama umemsikia vizuri yeye mwenyewe aliomba mjadala huu usiendelee ili yasije yakaibuka mengine zaidi. Anajua mengi yako juu ya hili na tunayoyajua yanatosha kuleta joto nchini.

  Kama mtakumbuka, Mwalimu alizidiwa mnamo mwishoni mwa Septemba 1999. Habari zikatangazwa na BBC lakini Mkapa alikuwa New York na akakanusha kwamba anaendelea vizuri. Mkapa alipotoka New York akaamua kupita London kuona hali ya Mwalimu.

  Ukweli ni kwamba alichokiona pale na alichoambiwa na madaktari ni kwamba hali ni mbaya na aliambiwa ni vema awatangazie watanzania wajiandae na lolote.

  Ndipo baada ya siku mbili akatangaza kuwa Mwalimu amelazwa huko St, Thomas Uingereza.

  Sasa hapa ndipo vurugu mechi ya habari ikaanza. Ndipo hapa familia ya Julius Nyerere na hasa Mama Maria inataka tuikumbushe yaliyotokea.

  Nakumbuka asubuhi moja BBC walimhoji kwa kirefu mtoto wa Nyerere yaani Anne Nyerere yule anayesli kwa Padri Nkwera. Huyu Anne mimi ndiye aliyenifanya wakati uleule tujue kuwa kuna ugomvi mkubwa kati ya serikali na familia ya Nyerere kuhusu ugonjwa wa Mwalimu.

  Anne alisikika kumnukuu baba yake (Julius Nyerere) kwamba alipokuwa Butiama Mkapa alienda kumtembelea na akamkuta Nyerere akiwa katika hali mbaya. Nyerere akamuuliza Mkapa mara tatu "Je, mmeshamueleza daktari wangu kuhusu hali yangu?" Mkapa hakujibu swali hili.

  Hiyo inaonyesha familia ilianza kugombana na serikali tangu Nyerere bado yuko kitandani Butiama. haya ni kwa mujibu wa Anne alivyohojiwa na BBC.

  Na hapo BBC walifanya busara sana kuchukua maneno machache ya huyu Anne Nyerere. Kama wangechukua kila kitu basi kuna watu wanasema ama Anne Nyerere angefungwa au nchi ingetikisika.

  Kwanza Anne alieleza kuwa kuna wakati hata familia walikataliwa kumuona Nyerere kana kwamba wao ni watu baki wakati huyo ni baba yao yuko kitandani. Ugomvi huu ukamalizwa na Kingunge Ngombare Mwiru ndipo watoto yaani Makongoro, Anne na nadhani na Manyerere Jackton wakaruhusiwa kumwona chumbani!


  Anne Nyerere aliwaeleza BBC kwamba familia ya Mwalimu inalaumu kwamba wanasiasa wa Tanzania waliujua ugonjwa wa Mwalimu tangu 1994 lakini walimficha ili wamtumia mwaka 1995 kwenye kampeni kwa manufaa yao.

  Akamlaumu Professa Mkwakyusa yaani Daktari wake kwamba hakumshauri vizuri kuhusu hata kufuatilia lishe maana Mwalimu alikuwa akiingia kazini anasahau hata kula.

  Ulikuwa ni ugomvii mkubwa kiasi kwamba Profesa Mwakyusa akaona kuwa familia haina imani naye tena na hivyo akafungasha virago kkurudi Tanzania asiendelee kumuuguza Mwalimu. Familia iliona acha aende.

  Ndipo hapa kazi kubwa ikafanywa tena kati na ikabidi asaidiwe Makongoro Nyerere kutuliza ugomvi huu. Bila Makongoro basi hali ingekuwa mbaya, maana Kingunge alishindwa akaishia kuwa mshauri zaidi kuliko kuwa msuluhishi. Hivyo, ugomvi ule wa familia na serikali uliisha kwa kushauriana lakini si kwa kukataa hoja za wanafamilia.


  Hivyo, kinara mkubwa wa ugomvi wa Nyerere wala si huyu Vincent wa CHADEMA. Kinara mkuu ni huyu Anne Nyerere. Kwa nini Anne Nyerere alikuwa kinara kwenye ugomvi huu. Ni kwa sababu hata sasa tunajua kuiwa Anne na mama yake Maria Nyerere wote ni wafuasi wa Padri Nkwera yaani WANAMAOMBI.

  Uanamaombi wao uliwafanya waamini kwamba kwa maombi ya Pari Nkwera na wao Nyerere atapona kama walivyoponyshwa wengi na Padri Nkwera. Hivyo, kulikuwa pia na ubishi kwamba Nyerere aendelee kuombewa na Padri Nkwera.

  Uanamaombi huu uliwafanya wanafamilia wapendekeze Padri Felician Nkwera aambatane na msafara wa kumsindikiza Nyerere hadi London. Wazo ambalo serikali ya Mkapa haikulikubali, ndipo trip ya kwanza wakaondoa Nyerere na Maria Nyerere. Alipzidiwa akafuata Anne Nyerere na sikumbuki wengine vizuri ila nakumbuka Makongoro ilibidi achangiwe nauli ya kwenda huko.


  Walipofika huko London, ndipo yalipotokea hayo niliyokwisha kueleza na hiki ninachokieleza. Kuwasili kwa Anne Nyerere huko London akajiona yuko huru zaidi na akaamini sasa atafanikiwa kumsafirisha Padri Nkwera hadi London. taabu ikawa ni gharama ukizangita kuwa hata Makongoro alichangiwa.

  Yeye Anne hakuona tatizo la gharama. Alijua kuwa baba yake yaani Julius Nyerere alikuwa na urafiki mkubwa na Muamar Ghaddafi wakati huo na kama mtakumbuka hata ule msikiti wa Butiama una mkono na msaada wa Ghaddafi. Hivyo, Anne akawasiliana moja kwa moja na Tripoli kwa Ghaddafi na Ghaddafi akawa radhi kutoa gharama za kumsafirisha Padri Nkwera kwenda London.

  Ghafla kikatokea kitu ambacho Anne hakuwa amekkitarajia. Padri Nkwera atapata visa lakini ni itabidi ijulikane ni nani alimgharamikia nauli na makazi huo Londo ukizingatia kuwa watoto kama Makongoro na nadhani hata wengine waklichaniwa. Hapa ndipo Anne alipoona kuwa hana budi kuushirikisha ubalozi wa Tanzania. Zaidi ni kwamba hata nauli sasa ijulikane kwamba ametoa Ghaddafi.

  Nauli kutolewa na Ghaddafi haikuwa tatizo kwani serikali ya Tanzania mnakumbuka hata ilivyotetea juzijuzi bendera ya Ghaddafi. Tatizo likaja kuwa Uingereza na mataifa karibu yote ya West yalikuwa na uhusiano mbaya na Ghddafi.
  je, iweje Uingereza inayomuugza Nyerere isikie kuwa amesaidiwa na Ghaddafi. Wanadiplomasia wakaona aheri kulitupilia mbali wazo la Padri Nkwera na Nyerere atibiwe na kama ni kufa basi afe kifo cha kawaida.

  Hii ikamuudhi sana Anne ndipo akaanza kutoa yote niliyoyaeleza na ndipo sisi wanadunia wengine tukajua kuwa kulikuwa na ugomvi mkubwa kwenye familia ya Nyerere wakati wa ugonjwa na walalamikiwaji ni kama nilivyotaja.

  Sina hakika kama hata leo Anne Nyerere alishawahi hata kusalimiana na Mwakyusa. Lakini haya ndiyo yaliyojiri.


  Leo ,mama Maria anapokuja na kueleza kana kwamba kulikuwa shwari basi akumbuke kuwa familia yao ni kubwa na hivyo inafuatiliwa kila linapotokea la kuandikwa ambalo wakisahau watu basi si rahisi kusahau wote.

  Katika ugonjwa ule wa Nyerere ndipo waandishi wa habara wa Tanzania walijisifu kwamba walitumia busara ya hali ya juu maana wangandika kila kitu na hakuna aliyewakataza walijidhibiti wao wenyewe basi kusingekalika, maana jinsi hali ya Mwalimu ilivyokuwa inazidi kuwa mbaya ndivyo imani kwamba tutampoteza ilivyozidi na ndivyo panic ilivyozidi, ndivyo na hasira zilivyopanda na ndivyo na siri zilivyozidi kutoka na ndivyo hata serkali ilivyozidi kushindwa kudhibiti taarifa sahihi kutoka kitandani alikolala Mwalimu.

  Mnakumbuka siku za kwanza habari zilikuwa zinatolewa na ubalozi zinaenda Ikulu Dar kisha kwa wanahabari. Lakini kadiri Mwalimu alivyozidi kuelekea kifo hii ikashindwa na watoa habari ndiyo waka kama hawa akina Anne Nyerere na ndipo tupendao habari tukasikia kila kitu.

  Hii ndivyo kiduchu ilivyokuwa, hivyoVincent Nyerere amegusa kidogo tu.
   
 2. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Jamani tuachane na porojo. Nyerere amekufa na Cancer ya damu. Tumuache mzee apumzike! Wazazi wakiumwa mambo yanasemwa mengi hapa kwenye familia zetu lakini Nyerere amekufa kwa Cancer na huo ndiyo ukweli.


   
 3. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,984
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  ARUMERU NA MTAJI WA BABA WA TAIFA, hakuna sera
   
 4. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Dah!hii sasa ni season 2 episode 1 ngoja tuone mbeleni itakuaje
   
 5. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kama kweli ukitajwa tajwa kama ni marehemu huwezi pumzika... Basi kazi ipo kwa Mwalimu Kupumzika kwa Amani....
   
Loading...