Ugomvi wa CCM na CHADEMA

mwanda-mbo

Member
Jan 16, 2014
21
3

UTANGULIZI

Inapotokea migongano baina ya mtu na mtu, watu na watu, au vikundi au kikundi cha watu Fulani na watu Fulani, kwa hakika na dhairi kabisa, kwamba uhalisia na dhamira halisi iliyo fichika kwa ndani kabisa hudhiirika, kwa sababu taswira ya mtu wa ndani hujitokeza na kushindwa kujificha pindi mtu au watu wanapo kuwa kwenye hali ya gadhabu na hasira Kwa dhairi; tumeweza japo kwa sehemu kujua dhamira za viongozi wa taifa hili juu ya mustakabali na mwelekeo wa nchi yetu kwa namna ya wazi, pale tulipoona vyama vya siasa vikigongana hata kufikia mahali, wenye dola kuamua kutumia dola na majeshi na wenye kutumia nguvu ya umma nao wakatumia, na kila mmoja akiwa na malengo Fulani ya kuyatimiza.

Mgongano huo ulionipa nafasi ya kujua dhamira ya watawala wa nchi hii, jinsi isivyo njema, kwamba wako tayari hata kuua raia tu, kwa kulinda maslai yao na kile wanacho amini wao hata kama ni kinyume na matakwa ya watanzania, ndicho kimenipelekea kutaka kujua zaidi kwanini chama tawala; wamekuwa na ugomvi mkubwa kiasi hiki na watu, vyama vya upinzani haswa CHADEMA ilihali nao ni watanzania, lakini bila huruma; CCM wamefikia hatua hata ya kutoa roho za watu ili kulinda kile wanacho amini wao.

Kwa lugha nyingine tungesema CCM wanagombania nini na CHADEMA NA UKAWA? Na watu walio na mawazo tofauti na CCM kiasi kufikia, kutumika kwa risasi za moto na kung'olewa watu meno?

Mwalimu Nyerere alipata kusema maneno haya----hakuna watu wana haki ya kufanya maamuzi kwaniaba ya watu wengine, japo huenda Nyerere alijilekeza katika sera za wakoloni na wakoloni mambo leo lakini bado maneno yake yanaleta tafsili pana zaidi katika kizazi cha leo
Kufanya maamuzi Kwa niaba ya watu wengine bila kuwahusisha na kusikia mawazo yao kwanza; ni udikteta na ni kuwafanya hao unao wafanyia maamuzi, kuwa ni wajinga, hawajui chochote na hawawezi kufikili bila ya msaada, pia unakuwa, umekuwa kipimo cha ujinga na busara zao, jambo ambalo si sahihi kabisa.

Mwalimu Nyerere pia alipata kusema katika kitabu chake cha freedom and developmet-kama kunaitajika maendeleo ya kweli, basi watu lazima wausishwe; kwa maneno haya, kwanza kabisa mwalimu anajipinga mwenyewe pale ambapo aliamua mambo kinyume na alivyokuwa anamini na kuandika katika maandishi tofauti kama tulivyoona, mfano katiba ya Tanzania ya 1977, ambayo ilitungwa na watu 20 tu na kupitishwa na bunge la muungano (bunge la CCM) ambalo halikuwa bunge la katiba; na ndani ya masaa matatu kwa wachangiaji wasiozidi watatu, katiba hiyo ikapatikana; kinyume kabisa na demokrasia na uhuru wa fikra na kwasababu watu hawakuusishwa kabisa kama ambavyo alikuwa akisisitiza na ndio maana katiba hiyo ya CCM imekuwa katiba mbovu miongoni mwa katiba mbovu katika historia ya Africa, kwa maana nyingine mwalimu alihubiri kinyume na alivyo tenda, na hili ndilo lililozaa falsafa dhaifu za zidumu fikra za mwenyekiti, hata kama fikra hizo ni za kuangamiza taifa na watu wake.

Kwa baati mbaya Sana, mwalimu alirithisha utamaduni huo mbaya kabisa katika kukuza demokrasia, kwa kumfanya mwanadamu kwamba hakosei na kuwa kama MUNGU, kiasi leo imekuwa shida kabisa kwa watawala wa CCM kukosolewa na hawataki kabisa kuwausisha wananchi katika masuala hasa yanayo wausu wananchi wenyewe na taifa kwa ujumla.

Kwa msingi wa maneno ya mwalimu Nyerere, kama kunaitajika maendeleo ya kweli basi watu lazima wahusishwe, na kwa madhumuni ya kukuza demokrasia na kuongeza ushiliki wa watu katika masuala ya taifa ambayo ndio maendeleo; na kuongeza uwajibikaji, uwazi na utawala bora kwenye serikali,hapa ndipo uwepo wa vyama vya siasa ukalazimika kuingia katika mfumo wa nchi yetu, yaani watu wenye mawazo na fikra tofauti na za Mwenyekiti na watu watakao kosoa sera na mifumo ya Mwenyekiti kwani ilithibitika wazi fikra za mwenyekiti hazikuweza kuwa kipimo cha ujinga kwa watanzania na ndizo zilizo dhoofisha utawala bora kwa kutowausisha watu ili kuleta maendeleo, na pia ndizo zilizo leta mfumo wa rushwa na udikteta pamoja na ugandamizaji wa haki za binadamu na kufanya maendeleo ya taifa hili yategemee fadhili na dhamiri za Mwenyekiti, kama akiwa mwema kama alivyo kuwa mwenyekiti wa kwanza basi ni neema na kama akiwa mbaya basi ni kuumia tu, kama ambavyo tunaendelea kuumia sasa, maana kila mwenyekiti anaekuja kupitia CCM ni afadhali aliepita

Ikimaanisha dhairi kwamba, walikuwako watu wenye mawazo tofauti Na fikra za Mwenyekiti Na yenye mlengo wa kizalendo na maslai mapana kwa wananchi. Chaajabu Sana katika taifa hili

wamekuweko watu wanao tukuza fikra za Mwenyekiti kwamba ndio sahihi na kwamba Mwenyekiti hakosei kabisa na anaekwenda kinyume nae basi akatiliwe mbali; hashaa! Kwani taifa hili ni la kifalme? Kwa mfano; swala la katiba mpya katika inchi yetu ya Tanzania, ni kama vile Mwenyekiti wa CCM alitambua kuwa ili maendeleo na katiba bora ipatikane ni lazima watu wausishwe kama maneno ya mwalimu Nyerere, na ikawa vyema mwanzoni, lakini Mwenyekiti alipogundua kuwa maoni na fikra za wananchi zimepingana na yeye; akayakatilia mbali maoni ya wananchi na akaleta maoni yake kwa namna ileile ya katiba ya 1977, hashaa!

Je Mwenyekiti wa sasa nae ni mnafki Pia? au bado anaimani ileile ya zidumu fikra za Mwenyekiti na kwamba yeye ndie anaeye jua kuliko watanzania wote; na kama kweli kwamba Mwenyekiti ndie mwenye busara katika taifa hili kuliko watu wote, je ilikuwaje ashindwe kujua umasikini wa wanachi anao waongoza ili hali akikili kwamba taifa ili ni tajiri sana katika rasilimali? Sasa mtu Kama huyu asie jua umaskini wetu tu, ana uhalali gani wa kutuamualia juu ya aina gani ya katiba tunayo itaka? Huu ni upunguani!

NINI UGOMVI WA CHADEMA, UKAWA NA CCM

Jambo la kawaida kabisa katika demokrasia ya vyama vingi, ni migongano ya sera na vipaumbele na hata ilani zao na huweza kuzua mijadala mikubwa sana ila mwisho wa siku mfanya maamuzi wa mwisho apate fursa nzuri ya kuchagua ni mfumo, sera, au ilani ipi kati ya hizo za vyama vya siasa ni bora na inaonyesha njia ya kutuvusha hapa tulipo na kutupeleka hatua nyingine ya maendeleo.

Ijapokuwa sisi sote ni watanzania japo wakati mwingine watanzania tunaingiwa na hofu kwamba hawa wenzetu (CCM) ni kweli watanzani? au ndio wakoloni weusi? Na Kama hawa ni watanzania wenzetu, kwanini wanatufikisha mahali tusipo taka kufika? na pia ugonvi kati ya CCM na CHADEMA ni nini?

Katika nchi yetu hii ya Tanzania hali sio shwari kabisa, kwani ugomvi wa vyama vya siasa umehama mstari kabisa, sio tena sera, ilani, mfumo, bali tumefikia mahali watu wanapigwa risasi za moto na kuuawa tu kwasababu wanaandamana kudai haki yao na maslai yao,waandishi wa habari wanauwawa kwasababu wanapiga picha katika mikutano ya CHADEMA na si CCM, madaktari wana ng'olewa meno tena na watu wanaoitwa, eti usalama wa taifa kisa wanasimamia madai yao tena yenye maslai mapana kwa taifa, wanafunzi wanapigwa hadi kuvunjwa viungo na jeshi la polisi, lililo pewa dhamana ya kulinda raia, wakiwemo wanafunzi, tu kwa sababu wanaisiwa ni wafuasi wa upinzani, watu wanapigwa hadi kufa na kubakwa eti na jeshi la wanchi kisa wanaandamana kudai haki yao ya kunufaika na rasilimali ya gesi, eti, CCM wanadai ni wana siasa wa cuf, na chama Fulani ni cha dini Fulani; shame!

Swali kubwa ambalo nimekuwa nikijiuliza kwanini CCM huwa hawajibu hoja kwa hoja, ua kama ni maandamano na wao waandamane na wafuasi wao waonyeshe kutoridhishwa na waandamanaji wa upizani au ni kwamba hawana wafuasi?, bali ccm wameamua kujibu maandamano kwa risasi za moto na kuwabaka raia wa Tanzania wasio na hatia, kwanini imekuwa ndio mila mpya ya CCM kutumia mabavu na nguvu za dola, hata kuua raia wake bila hata kuwa na huruma kwa kuzima fikra zilizo kinyume na za mwenyekiti, kwanini hawataki kuwapa kile kitu wananchi wanataka kama wanafunzi wanataka mikopo wapewe lakini matokeo yake wana vunjwa na kupewa vilema, machinga wanataka maeneo ya biashara matokeo yake waambulia virungu na kunyang'anywa mali zao, wachimbaji wadogowadogo wa madini wana nyang'anywa maeneo yao na kupewa, eti wawekezaji ili hali wao ndio walio gundua rasilimali hiyo na matokeo yake wakidai maeneo yao wanaambulia kupigwa hata kuuwawa tena na chombo cha usalama yaani jeshi la polisi, vyama vya upinzani vinataka tume huru lakini mwenyekiti hataki kutoa, anakubali kisha hatekelezi, yaani anafanya hiayana, na analeta vitisho, wao CCM wametengeneza green guard; CHADEMA wakitengeneza red brigade tayari Mwenyekiti ana kuja juu; kwanini?

Katika utafiti wangu, baada ya muda mrefu kujiuliza swali hili linalo wafanya CCM, KUTOKUBALI FIKRA HURU, na kutojikita katika kuwapa kile raia wake wanataka na kinyume chake wana jikita katika kuwaangamiza wale walio mstali wa mbele katika kudai haki na usawa kana kwamba watawamaliza kabisa na hali itakuwa kama zamani enzi za Mwenyekiti wa kwanza, nikagundua jambo moja tu kubwa-MASLAI BINAFSI MASLAI, huu ndio ugomvi wa CCM kwa CHADEMA na UKAWA, kwasababu yale yote yanayo wafanya CCM kugombana na hata kutafuta kuuwa ukawa na viongozi wake ni MASLAI YA CCM na Mwenyekiti;

Kwanza kwa muda mrefu vyama vya upizani vimetumia njia za mazungumzo ya moja kwa moja na yasio ya mojakwamoja katika kutetea wananchi na maslai mapana ya taifa, lakini hawakuweza kufanikiwa. Nafikili katika kutokata tamaa waliamua kutumia njia nyingine ya kikatiba ambayo imekuwa mwiba kwa fikra za Mwenyekiti na inakuwa ngumu kufuta maana ni swala la kikatiba nalo ni maandamano ili kuwalazimisha mifisadi wa taifa ili kutenda haki ama waachie nchi, ningeweza kutaja mambo mengi sana yanayo ligusa taifa na pengine yanayo mgusa mwananchi mmoja mmoja, lakini nigusie haya machache

(a) RUSHWA, taifa hili linalo ongozwa na serikali ya CCM, na kwa msingi wa katiba ya sasa isiyo tokana na wananchi bali fikra za Mwenyekiti tena wa CCM, kwamba ina mpa mamlaka ya kumteua swaiba wake kuwa mkuu wa jeshi la polisi na ndivyo ilivyo, sasa jeshi hilohilo ndio linaongoza kwa rushwa nchini mpaka sasa na hakuna jitihada za makusudi katika kukomesha rushwa hiyo; kwanini?
Mikataba ya kifisadi tena ya wazi sana kwamba wapo watu Fulani wanakula dili na kulisababishia taifa hasara, lakini kwasababu wamekula dili kwa jina la CCM.

Viongozi tena Mwenyekiti ana diliki kuwatetea wezi; kama sio kwamba na yeye anahusika; ni nini? Huo uchungu wa kuwatetea wezi wa ESRCOW, EPA, KAGODA, RADAR ,MEREMETA, RICHMOND, na mengine mengi anutoa wapi wakati wakina babu seya wana sotea jela bila huruma ili hali babu seya waligarimu, maisha ya watu wachache sana ukilinganisha na hizo EPA jinsi zilivyo watesa watanzania na zinaendelea kuwatesa bila huruma kwa gharama za maisha na rushwa iliyo kithili kila mahali.

(b) MAUJAI YA RAIA, katika taifa hili la kifalme linalo mpa mamlaka Mwenyekiti kuuwa raia wake tena hachukuliwi hatua zozote kwasababu kwanza nani wa kumchukulia hatua, maana wote alio watuma ni wateule wake licha ya kwamba yeye ndio kawapa kazi ya kuuwa, mwisho wa siku hata Mwenyekiti mwenyewe anakinga ya kutoshtakiwa, na chaajabu; tofauti na wauwaji wengine ambao hawako CCM, kama majambazi n:k, kwamba wakikamatwa wanasekwa ndani, bali hawa wateule wa Mwenyekiti hupandishwa vyeo na kustaafu kwa heshima kama ispekta kamuhamba alivyo tekeleza kazi nzuri ya kumuua mwandishi wa habari DAUDI MWANGOSI, na kisha akaahamishiwa temeke Dar es salaam na baadae kupandishwa cheo na kisha kustaafu kwa heshima, sasa niambie kama haikuwa kazi ya Mwenyekiti, ilikuwaje alimhamisha na kumpandisha cheo muuaji? Hapana haingii akilini Mwenyekiti lazima ana maslai, lakini pia yuko huyu mwingine eti alikuwa mkuu wa usalama wa taifa kitengo cha siasa, mpanga mauaji nae baada ya kazi nzuri sana amepelekwa kuwa balozi wa Tanzania Canada! shame on you Mwenyekiti!

(c) KATIBA, baada ya hawahawa CHADEMA NA UKAWA, pamoja na kupigwa na hata wengine kupoteza maisha, kukomaa mpaka kieleweke, hatimae tukaanza mchakato wa kupata katiba mpya; na kama maneno ya Mwenyekiti wa kwanza kwamba ili maendeleo ya kweli yapate kuwepo lazima watu wausishwe, kweli tangu mwanzo watu wakausishwa kama laki 4 na ushee, eeh! Kumbe wananchi wana mawazo tofauti na Mwenyekiti yaani wamekataa fikra za Mwenyekiti wa kwanza hadi wa sasa katika namna ya kuongoza nchi, kwani wameshindwa tu kuondoa rushwa sasa umaskini huu wa watanzania watauondoaje?, basi kama ilivyo ada maslai ya Mwenyekiti yakawekwa hatarini na kama alivyo, hataki kabisa kuwa kielelzo cha kivitendo, akageuka na kuyatupilia mbali maoni ya mwananchi; kwani ni mjinga na hajui chochote, kumbe ukweli ni kwamba kama maoni ya wananchi yangepita Mwenyekiti asingekuwa tena MFALME, MBABE, MKATILI, MWIZI, MUUAJI, MBAMBIKIAJI WA KESI, n:k, je haya si kulinda maslai ya Mwenyekiti na wasaidizi wake?
Ni mambo mengi sana ningeweza kuyasema lakini nilitaka kukupa picha ndogo sana, sasa mgogoro mkubwa wa CCM unao wafanya kutumia mabavu na vyombo vya dola tofauti kabisa na katiba ya nchi na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeidhinisha kwa maslai ya taifa, ili kuimamarisha utawala bora na ustawi wa jamii ya Tanzania, unao wafanya viongozi wa CCM

Kutamka; LIWALO NA LIWE, WAPIGWE TU, hao wapinzani (UKAWA) wa fikra za Mwenyekiti ni kwamba.

(a) USALAMA WA VIONGOZI WA CCM UKO HATARINI, kama leo matakwa ya wananchi yote kwa ujumla wake pamoja na katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi, watuumiwa wa ufisadi wachukuliwe hatua stahiki za kisheria tangu awamu ya Mwenyekiti wa kwanza mpaka leo, tume huru ya uchaguzi, n:k, basi CCM wote; unaowajua, hakuna atakae pona, maana rushwa inawatafuna, sasa ukiruhusu mfumo utakao wabana, inamanisha hawa wote watapotea na swala ambalo hawako tayari sio tu kumpoteza Mwenyekiti bali na wao wamsaidiae kazi za kifisadi, hivyo hawatakuwa tayari kuruusu jambo lolote lile hata kama lina maslai mapana kwa taifa kwa sababu tu linaleta mushkeli kwa usalama wao na familia zao na utajiri wao wa wizi, kama walivyo pinga katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi, kama ijulikanavyo kama katiba ya Warioba

(b) USALAMA WA MALI ZAO, VIJISENTI VYAO, na hili ndio mgogoro mkubwa; kwani usalama wa mali za hawa maccm, mafisadi zitaendelea tu kuwa salama kama mfumo wa uongozaji taifa ili uteandelea kuwa huu wa zidumu fikra za Mwenyekiti, hata kama amekwisha kufa; kwani fikra za huyu Mwenyekiti hazitaki katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi; kwani itataifisha malizao wezi wote wa CCM, pia fikra za Mwenyekiti hazitaki kabisa utawala bora na kueshimu sheria, kwani wataua lini raia ili kuwatisha kutodai haki zao, tena fikra za Mwenyekiti hazitaki kabisa ufisadi na rushwa kuisha kwani watapiga dili wapi; tena kama walivyo fanya kikamilifu katika dili la ESCROW, EPA, MEREMETA, UDA, RADAR, n:k kwa ushilika wa Mwenyekiti na wadau wake.

(c) HOFU YA KUONDOKA MADARAKANI, kama alivyopata kusema katika moja ya ibada katika kanisa la FULL GOSPEL BIBLE FELLOWSHIP, Askofu Mkuu , ZACHARY KAKOBE, kwamba serikali ya CCM, inhofu ya kuondoka madarakani, na kimsingi hofu hiyo inatokana na uovu ambao viongozi wa CCM walio ufanya; kwani wanajua vyema, UKAWA ni watu wanao taka kutenda haki na kuludisha hadhi ya taifa hili kama taifa linalo heshimu watu wake na demokrasia na hakuna alie juu ya sheria; na kuleta maendeleo ya kweli kama ilivyo kuwa imani ya Mwenyekiti wa kwanza katika andishi lake katika kitabuchake cha freedom and development, sasa kama wakiingia madarakani (UKWAWA) maana yake ni hii, kwanza fedha zote za wananchi zilizo ibiwa na kupelekwa ughaibuni kufichwa zitarudishwa, kama ambavyo alipata kusema DR. SLAA, katika moja ya mahojiano yake katika televisheni, hivyo kufanya wale ndugu na wafuasi wa Mwenyekiti kukaa tumbo joto, kwani watakuwa maskini tena; ilihali wamesha zoea kutembelea kilimo kwanza yaani mashangingi kwa lugha ya mtaani! (magari ya kifahali)

Kwa ufupi CCM haiko tayari na haito kuwa tayari kukubali na kuamini katika fikra huru na demokrasia ya kweli, kwani usalama na kuendelea kuwepo kwa CCM katika uhai wake ni mfumo huu ambao unalinda maslai ya Mwenyekiti na viongozi wake katika chama cha wezi yaani CCM, mfumo usioheshimu na kukubali FIKRA HURU.

Hivyo ugomvi wa CCM na UKAWA na haswa CHADEMA, ni jinsi wanavyo linda maslai yao ya sasa na ya baadae; na usalama wao wa sasa na baadae, kwa maana hiyo CCM hawatakuwa tayari kuruhusu jambo lolote lile litakalo atarisha uhai wa CCM,- japo ukweli ni kwamba UPEPO HUVUMA UPENDAKO, haya ni maneno ya YESU KRISTO na huwezi kushindana na upepo kwani utavunjika tu, ni suala la muda tu, haki itatamalaki katika taifa hili na tutasahau milele zidumu fikra za Mwenyekiti wa CCM, na tutakua kweli taifa la kidemokrasia lenye kueshimu na kuwajali raia wake, MUNGU ibariki na kuiludisha, TANGANYIKA.

MWANDISHI; ANDERSON E. NDAMBO
0718 582371
andambo@yahoo.com
 
Back
Top Bottom