Ugomvi wa Askari na Makondakta wa Daladala

Baba Watoto

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
393
278
Habari zenu Waungwana,
Leo alfajiri sana nilipanda daladala, baada ya mwendo kidogo nikasikia purukushani, konda anasema 'Jamani ee humu kunawenzenu watatu, hii gari ya biashara bwanaa' mara akaingia mmoja so huku nyuma kukawa na askari wawili, safari ikaendelea. Konda akaanza tena zogo kidogo kuwa gari ya biashara na nini na nini askari mmoja akamjibu kuwa wenzake (gari zilizotangulia) ndio wenye makosa kwa kuwa hawakusimama, abiria nao wakaingilia kidogo baada ya konda kurudi mlango (Tulikua nyuma); hawa abiria wakawa wanamuunga mkono konda.
Hii ikanifanya niwaze kidogo ( huwa naogopa sana kuchangia mada kwenye usafiri wa jamii), ina maana kile kiwanda chetu cha Nyumbu ndio taabani, hakiwezi hata kufufuka ( nilisikiaga tetesi kuwa kinafufuliwa ) ss hii ingefanya rahisi kidogo maana, si tunatengeneza wenyewe bwana? Au kweli vyombo vyote vya usalama vimeshindwa kuwa na usafiri wao unaojitosheleza, kweli? au kama ni gharama basi kwanini hawa wandugu wasijengewe nyumba bora wakawa wanakaa kambini maana najua maeneo wanyo makubwa tuuu. Mawazo yalikuwa mengi kiasi cha kufikia kuwaza kama kweli kuna ulazima kwa serikali kulipia chakula au vifaa kwa wafungwa walioko magereza maana hawa jamaa wanaweza zalisha chakula kingi sana kwa taifa zima, anyways yalikua mawazo marefu sana na nikaona kweli kuna raha ya ajabu kuishi Tanganyika, I mean Tanzania.
 
Back
Top Bottom