Ugomvi na Chuki (BIFU) zinazoendelea kwenye Media zetu zina athari gani kwenye Tasnia ya Habari kwa Tanzania yetu?

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,592
11,831
Kwa wadau wote wa Tasnia ya hapabari hapa nchini mnaweza mkalitazama hili na kulijadili kwa mapana huenda likawa na matokeo fulani hasi ama chanya kwenye sekta ya habari hapa nchini.

Tumeona matukio mengi tu na niseme labda ni tabia inayochipuka kwa kasi kubwa kwenye sekta ya habari kwa hiki kinachoitwa BIFU ( Chuki, ungomvi, malumbano) baina ya vyombo vya habari na watu fulani fulani ama taasisi fulani kuto rusha matangazo yanayo wahusu watu hao.

Imefika hatua sasa hata Kama tupo kwenye tukio la kitaifa anapoanza kuzungumza mtu fulani utakuta chombo fulani Cha habari kinakata matangazo haraka sana. Kuna mifano mingi Sana katika hili

Haijaishia hapo, Kuna baadhi ya wasanii kazi zao hazusikiki kabisa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwasababu Bifu baina ya Media na msanii husika.

Mfano Clouds, Wasafi, Efm n.k haya mambo yamejitokeza sana.

Sasa hebu tujiulize hali hii ina athari zipi kweye Tasnia ya habari kiujumla? Karibuni wadau tupate maoni yenu na hasa naamini hapa JF Kuna wadau wengi wa sekta ya habari karibuni tulizungumzie hili.
 
Hayo yapo tu!! Tangu kuumbwa kwa Dunia hii!! Hayajaanza leo wala jana!!
Ni pAle shetani alipo asi malaika wakakata mawasiliano mpaka leo hawaongei.

Isipokuwa tu Mungu na shetani wanapiga story. Pale Mungu alipo muuliza devil km amemuona mtumishi wake Ayubu.....
Shetani kila mtu hamtaki ila anakula timing ya kuwakamata watu,
 
Haina athari yoyote ila unaleta ushindan zaid kwenye vyombo vyenyewe ,wanahabri na wasanii
 
Back
Top Bottom