Mahandeiboho
Member
- Dec 27, 2016
- 94
- 43
Ugomvi kati ya wafugaji na wakulima unaongezeka na umekuwa sugu. Kamata kamata ya polisi na vikao vya usuluhishi vya wanasiasa, wakuu wa wilaya, kata na vijiji ni kupoteza muda na rasilimali. Kinachotakiwa ni kuboresha sera za umiliki wa ardhi, kilimo, mifugo na kupanga kitaalam matumizi bora ya ardhi. Kutoa elimu kwa wadau kuhusu matumizi bora na endelevu ya ardhi.
Tujifunze kutoka Kenya (Swinerton Plan). Serikali iwa shirikishe wataalam wa ardhi, kilimo, mifugo, range management, wanyama pori, misitu na wataalamu wa sera. Wakutane waigawe nchi ki ikolojia katika zone 6. Ramani zichorwe na zitumike kupanga matumizi bora na endelevu ya ardhi.
Mashamba ya size mbalimbali yapimwe hati zitolewe na watanzania wamilikishwe. Zone 1 na 2 zitumike kulima mazao yanayohitaji mvua nyingi na udongo wenye rutuba kama migomba, kahawa, chai, mbogamboga na matunda, miwa, na ufugaji wa ndani (intensive) au nje kwa uthibiti (semi intensive) wa ngombe wa maziwa, mbuzi wa maziwa na mifugo mingine inayo tunzwa kwa utaratibu huo.
Zone 3 & 4 (Grasslands and woodlands) hizi zitumike kuzalisha nafaka kama mahindi, ngano, mpunga, viazi, maharage, nk na ufugaji wa ngombe wa maziwa katika mashamba yaliyo pimwa na kuende lezwa kwa uzio (paddocks) uoteshaji na utunzaji wa majani. Zone 5 na 6 (semi arid and arid lands) hizi zitumike kwa kufuga ng'ombe mbuzi na kondoo wa nyama kazi inayofanywa na pastoralists wa Tanzania.
Kila mtu atalazimika kufuga mifugo inayolingana na uwezo wa eneo lake. Wakulima watakuwa mbali na wafugaji na hakutakuwa na muingiliano. Maeneo ya hifadhi ya Misitu na Wanyamapori yabainishwa na kutengwa.
Tuchangie mada hii tupate ufumbuzi wa kudumu.