Ugomvi baina ya Uchina na Marekani wazidi kuwa mkubwa

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
?Televisheni ya Press TV imeripoti kuwa, ugomvi baina ya Marekani na Uchina unazidi kuwa mkubwa.
Televisheni hiyo imesema kwamba, ugomvi baina ya nchi hizo mbili umeongezeka baada ya Marekani kutangaza mikakati yake mipya ya ulinzi.
Kitendo cha kijeuri cha Marekani cha kuitaka Uchina nayo itangaze ina mikakati gani ya kijeshi, kimewakasirisha viongozi wa Beijing na kusema kuwa madai ya Marekani dhidi ya mikakati ya kiulinzi ya Uchina hayana msingi wowote.
Viongozi wa Marekani wana woga mkubwa kuhusiana na kuzidi ushawishi wa kiuchumi, kisiasa na kijeshi wa Uchina na hivi karibuni Rais Barack Obama wa Marekani aliashiria kuwa hawezi kuruhusu Uchina iwe na nguvu kubwa za kijeshi akisema kuwa atahakikisha Marekani inaendelea kuwa na nguvu kubwa zaidi za kijeshi duniani.
Hivi karibuni pia viongozi wa Uchina waliwaonya viongozi wa Marekani wasieneze ubabe wao barani Asia.
 
habari yako integrity imepungua sana kwa kifupi press TV ni television ya taifa ya iran, so wanataka jamii ibadili attention ya issue yake ya nuclear na vikwazo vingine!
 
habari yako integrity imepungua sana kwa kifupi press TV ni television ya taifa ya iran, so wanataka jamii ibadili attention ya issue yake ya nuclear na vikwazo vingine!

Na hapo ndipo wanaposhindwa kuelewa..sky news,press tv,cnn,rt,cctv na nyinginezo zipo kwa ajili stabilize nchi zao,tuangalie na kusoma upande wa pili wa shilingi.,by the way ur absolutely correct
 
Back
Top Bottom