Ugoigoi wa wabunge wa CCM unamfanya Zitto atambe. Hakuna wa kumjibu? hadi Serikali na spika wanawajibia au vilaza wengi?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Na Thadei Ole Mushi.

Kwa sasa Zitto yupo juu, Yupo kileleni sana anafuatiliwa na watanzania kwa ukaribu. Anachambua mambo mawili kwa wakati mmoja Ripoti ya CAG na Ripoti ya IMF.

Nimetafakari sana ni mbunge gani pale CCM anayeweza kumjibu Zitto kwa hoja anazotoa nikagundua hatuna. Yaani hatuna Mbunge anayeweza kuthubutu kusoma kurasa zaidi ya mia za Ripoti ya CAG. Inawezekana Zitto anatdanganya lakini nani pale CCM anayeweza kuchambua kama anavyofanya? Nani anayeweza kuthubutu kusoma Lugha ngumu ya IMF iliyoandikwa?

Zitto anasoma sana, vitabu na taarifa muhimu za kiuchumi. Haachi hata page moja anapekua kila ukurasa na analeta mtizamo wake. Na anajua hakuna mbunge wa CCM mwenye uwezo wa kusoma Kurasa zote za CAG na akisoma hawezi kupata maana na akipata hatothubutu kuja kuisema.

Si kosa la wabunge wetu, kosa ni la mfumo wa Chama, tumewafanya kuwa mihuri ya kupitishia agenda za Serikali Bungeni. Sasa hiki anachokifanya Zitto huku njee anatuumbua, ndio maana kina magazeti yamejipanga kumtukana na kumdhalilisha.

Tunaelewa kwa nn anatukanwa, hatuna mtu wa viwango vyake. Aliwahi kujaribu Polepole kwa kukopa maduhuli ya Serikali ili hesabu zibalance lakini haikuwezekana. Tumewafungia wabunge wetu na hawaoni umuhimu wa kusoma au kutafiti chochote ndio maana Zitto anatuburuza atakavyo.

Niliwahi kusema wabunge wetu wanahitaji maandalizi yafuatayo:-

1. Wabunge wetu wapatiwe mafunzo ya mara kwa mara juu ya namna ya kuchangia, namna ya kuandaa hoja, nanmna ya kuiwasilisha mbele ya watu nk. Hili linaweza kufanyika kabla ya kuingia Bungeni. Wasaidiwe katika kuaandaa hoja zao na wataalamu.

2. Wabunge wetu wakubali kuingia gharama kuwa na vijana ambao watawasaidia kuwaandalia material za kuzungumza bungeni katika kila mada,hoja, au nafasi wanayotaka kuchangia. Hii itasaidia kuwafanya wapate mawazo mbadala. Si sahihi mbunge kuongea bungeni bila kuwa na utafiti wa kutosha, ukishakuwa mbunge sio kwamba unajua kila kitu hapana.

3. Chama kiandae utaratibu wa kuchagua nani awasilishe nini ndani ya bunge kulingana na aina ya mtu na aina ya Hoja. Wabunge hawa waitwe na wawasilishe hoja zao kwenye jopo la wataalamu na wawasikilize na kuwarekebisha. Hili naamini litakuwa linafanyika kwa upande wa pili. Yaani akisimama mbunge wao tu anakupiga na hoja hadi unaridhika. Watakuwa wanaitwa na kuwasilisha hoja zao kabla ya kuingia bungeni.

4. Chama kiongeze jukumu hili kwa kitengo cha utafiti cha chama. Sijui kitengo hiki kina tafiti gani hadi sasa ila tafiti hizo zitumike kuwaandaa wabunge wetu kabla ya kwenda bungeni.

5. Wabunge wetu walazimishwe kwendana na wakati yaani wasaidiwe kufahamishwa dunia inakwendaje. Wawe uptodate.... wasaidiwe kutafsiriwa matukio yanayotokea kila siku ya kiuchumi na kisiasa.

6. Wabunge wetu wasaidiwe na Inteligensia ya chama kupata taarifa muhimu za hoja na michango ya wapinzani kabla ya kuwasilishwa bungeni.

7. Wabunge wetu wasifichwe siri na taarifa muhimu. Inawezekana hata hii taarifa ya IMF hawana lakini ilifika kwa ZITTO kabla yao.

Wabunge wetu Pambaneni na Zitto acheni ugoigoi.

Ole Mushi
0712702602.
 
Zitto ana hali ya kusema na kuchambua chochote sababu anajiendesha kwa mujibu wa ilani ya chama chake...

Wa chama tawala hawawezi thubutu sababu mpaka wapewe maagizo na ruksa ya kufanya hivyo... or else wataonekana siyo wazalendo ni wasaliti...


Cc: mahondaw
 
Cha ajabu wanaotumwa kujibu hoja za Zitto ni Lusinde, Msukuma, Nkamia na Mlinga.

CCM ya sasa haiamini katika hoja bali nguvu ya vyombo vya usalama.!
 
haiwatetemeshi popote, uchaguzi ukija wanashinda kwa kishindo

Wanaccm kuanzia rais mpaka walio chini yake huwa hawashindi kwa wingi wa kura, bali tume ya uchaguzi na vyombo vya dola ndio huwa zinatumika kuwatangaza washindi. Kwakuwa huwa wanaingia bungeni/madarakani kwa njia zisizo halali ndio maana unaona hawana uwezo wa kujenga hoja kwani sio wawakilishi halali wa wananchi kupitia box la kura. Na hawahitaji kuwa na uwezo wa kuijenga hoja, kwani hila na dola kuwabeba ndio silaha yao.
 
Back
Top Bottom