Ugh, Wabunge nao watengua katiba!

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,348
6,471
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano

Tumeona jinsi Rais na Makamu wa Rais pia Spika wakivunja baadhi ya masharti ya katiba yetu licha ya kula kiapo cha kuilinda, kuitetea, kuifuata, kuitii na kuihifadhi lakini Bunge kwa niaba ya wananchi lenye mamlaka kikatiba kupitisha azimio la kuwaondoa viongozi hawa madarakani kushindwa kufanya hivyo.

Katiba inasema:
Ibara ya 46A
(1) ... Bunge linaweza kupitisha azimio la kumwondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikipitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii

(2) ..., hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais:
(a) Ametenda vitendo ambavyo kwa ujumla vinavunja katiba
(b) Amekiuka ibara ya 20(2)

Ibara ya 50
(3) Bunge litakuwa na madaraka ya kumuondoa Makamu wa Rais madarakani kama yale lililyonayo kuhusiana na Rais, isipokuwa kwamba hoja yoyote ya kumshtaki Makamu wa Rais itatolewa tu kama inadaiwa kwamba:

(a) Ametenda vitendo ambavyo kwa ujumla vinavunja Katiba au sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma
(b) Ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya katiba

[Maswali ya Msingi: Je, wabunge hawaoni kama hawa viongozi wanavunja katiba mapema kiasi hiki baada ya kushika madaraka yao? Kama viongozi hawa wanavunja katiba na wao wanabaki kimya basi `ni dhahiri nao wanavunja katiba walioapa kuilinda na kuifuata au hawaijui katiba na kuapa tu ilimradi wameapa? Kama wawakilishi wetu wanavunja aktiba, je si sahihi kwa wananchi kuwaadhibu watakapokuja kuomba kura zetu kwenye uchaguzi mkuu? Je, tusipofanya hivyo na sisi wananchi tutakuwa tunavunja katiba hasa ukiangalia Ibara ya 26 (1) Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano?]
 
Back
Top Bottom