Ugh, Spika, Makinda, na maana ya 'serikali' kikatiba!

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anne Semamba Makinda

Baada ya jina la Waziri Mkuu kusomwa na Spika, Mwanasheria Mkuu wa serikali alipewa nafasi ya kutoa hoja au kuongea; Mheshimiwa Tundu Lissu alimuuliza Spika kuhusu kanuni ya Bunge 53 (6) (c) ambayo inamtaka kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani kuongea mara hoja ya serikali inapotolewa; Spika alijibu kuwa hakukuwa na hoja ya serikali kwa Mwanasheria Mkuu wa serikali kuongea kwa sababu Baraza la Mawaziri lilikuwa halijaundwa.

Katiba inasema:
Ibara ya 6
Katika sehemu hii ya sura hii; isipokuwa kama maelezo yahitaji vinginevyo, neno ‘serikali’ maana yake ni pamoja na serikali ya Jamhuri ya Muungano, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, serikali za mitaa na pia mtu anayetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya serikali yoyote

[Maswali ya Msingi: Je, Mwanasheria Mkuu hakuwa mtu ambaye anatekeleza madaraka au mamlaka ya serikali? Hivi huko kutoa maana nyingine ya serikali, yaani ni Baraza la Mawaziri si kuvunja katiba na kanuni ya Bunge 50(6)(c)?]
 
hata mimi kwa uelewa wangu..... serikali ilikuwepo ila baraza la mawaziri halikuwepo.....hivyo basi kila waziri mkuu anapoteuliwa halafu ni wazi baraza la mawaziri linakuwa halipo... then kifungu hiki kinakuwa hakina kazi... na hii inasisitizwa kuwa hoja ya kuthibitisha waziri mkuu ikiletwa kama hoja ya serikali au kamati ya bunge...

mimi nimechoka.... tundu lisu alikuwa sahihi
 
NADHANI TATIZO LILIKUWA NI BALAZA LA MAWAZIRI KUKAMILIKA ILI YEYE KAMA SPIKA KUJIRIDHISHA KUWA SASA SERIKALI IMEKAMILIKA,NA MDA MWINGINE NI UELEWA WA BAADHI YA KANUNI ZA BUNGE AMBAZO ZINA HARIBU MAANA KAMILI YA ib YA 6 YA KATIBA,NI MAPUNGUFU AMBAYO TUNAHITAJI KUYAPIGANIA

MAPINDUZIIIII DAIMAAAAA
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anne Semamba Makinda

Baada ya jina la Waziri Mkuu kusomwa na Spika, Mwanasheria Mkuu wa serikali alipewa nafasi ya kutoa hoja au kuongea; Mheshimiwa Tundu Lissu alimuuliza Spika kuhusu kanuni ya Bunge 53 (6) (c) ambayo inamtaka kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani kuongea mara hoja ya serikali inapotolewa; Spika alijibu kuwa hakukuwa na hoja ya serikali kwa Mwanasheria Mkuu wa serikali kuongea kwa sababu Baraza la Mawaziri lilikuwa halijaundwa.

Katiba inasema:
Ibara ya 6
Katika sehemu hii ya sura hii; isipokuwa kama maelezo yahitaji vinginevyo, neno ‘serikali' maana yake ni pamoja na serikali ya Jamhuri ya Muungano, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, serikali za mitaa na pia mtu anayetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya serikali yoyote

[Maswali ya Msingi: Je, Mwanasheria Mkuu hakuwa mtu ambaye anatekeleza madaraka au mamlaka ya serikali? Hivi huko kutoa maana nyingine ya serikali, yaani ni Baraza la Mawaziri si kuvunja katiba na kanuni ya Bunge 50(6)(c)?]

Hata mimi naona Spika Makinda alichemsha kwenye hili wandugu! Kwanza alidai kwamba Mwanasheria Mkuu ametoa hoja toka "Serikalini," baada ya Tundu Lissu kuuliza swali lake kwamba hoja ya Serikali lazima ijadiliwe, unless imepitia kwenye Kamati, Spika Makinda akadai kwamba eti Serikali haijaundwa bado huku Wabunge mbumbumbu wa CCM wakimpigia makofi! Sasa kama Serikali ilikuwa haijaundwa hiyo hoja toka "Serikalini" ilitoka kwenye Serikali ipi? Huku si kusogeza "goal post" ili mradi uonekane kwamba ume-excercise madaraka ya Uspika?
 
Back
Top Bottom