Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,602
- 6,809
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anne Semamba Makinda
Baada ya jina la Waziri Mkuu kusomwa na Spika, Mwanasheria Mkuu wa serikali alipewa nafasi ya kutoa hoja au kuongea; Mheshimiwa Tundu Lissu alimuuliza Spika kuhusu kanuni ya Bunge 53 (6) (c) ambayo inamtaka kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani kuongea mara hoja ya serikali inapotolewa; Spika alijibu kuwa hakukuwa na hoja ya serikali kwa Mwanasheria Mkuu wa serikali kuongea kwa sababu Baraza la Mawaziri lilikuwa halijaundwa.
Katiba inasema:
Ibara ya 6
Katika sehemu hii ya sura hii; isipokuwa kama maelezo yahitaji vinginevyo, neno serikali maana yake ni pamoja na serikali ya Jamhuri ya Muungano, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, serikali za mitaa na pia mtu anayetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya serikali yoyote
[Maswali ya Msingi: Je, Mwanasheria Mkuu hakuwa mtu ambaye anatekeleza madaraka au mamlaka ya serikali? Hivi huko kutoa maana nyingine ya serikali, yaani ni Baraza la Mawaziri si kuvunja katiba na kanuni ya Bunge 50(6)(c)?]