Ugawaji vyandarua waendelea vizuri Dar es Salaam

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,267
33,039
UKIACHILIA mbali tukio la wizi wa vyandarua lililotokea mtaa wa Mwembe Madafu Kata ya Sandali, wilayani Temeke, kazi ya ugawaji wa vyandarua katika Jiji la Dar es Salaam imefanikiwa kwa asilimia kubwa.

Siku moja kabla ya ugawaji wa vyandarua, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Chiku Gallawa alimpeleka Polisi Mtendaji Mtaa wa Mwembe Madafu, Salim Shamte kwa tuhuma za kuiba vyandarua 150 vilivyotolewa bure kwa ajili ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Uchunguzi uliofanywa kwa kutembelea baadhi ya vituo, zoezi hilo lilionekana kwenda vizuri na kutokuwa na foleni katika vituo vingi vya kugawia, isipokuwa kituo cha mtaa wa Hananasif, Kinondoni ambacho kilionekana dhahiri kuelemewa na wingi wa watu.

Msimamizi katika kituo cha Mkunguni B Kata ya Hananasif, Esther Masaoe alisema mwitikio ni mkubwa na mpaka jana alikuwa amegawa vyandarua zaidi ya nusu ya watu waliowaandikisha katika mtaa wake.

Lakini mtaa wa Hananasif, ofisa Mtendaji wa mtaa, Dandasi Kijo alisema kituo, hicho kimekuwa na misururu mirefu ya watu kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu waliojiandikisha.

“Hapa tumeandikisha zaidi ya watoto 2000, na wanaotoa huduma ni watu wawili na ndio maana zoezi linakwenda taratibu. Lakini pia tunapata tatizo la watu wengine wamepoteza kadi na wengine hawakuandikishwa. Kwa waliopoteza tunaangalia uwezekano wa kutaka vielelezo vingine na kugawa,” alisema.

Naye Christina Elisha alisema utaratibu mbovu katika kituo hicho ndio umefanya watu kutumia muda mwingi katika kuchukua vyandarua.

“ Jana (juzi) walianza kugawa na wakakusanya kadi na alifunga saa tisa, lakini leo tumekuja wanaendelea kuita kadi za jana wakati wenyewe hawapo jambo ambalo linafanya tukae kituoni kwa muda mrefu sana,” alisema.

Kwa upande wa Wilaya ya Ilala, vituo kadhaa vilivyotembelewa na gazeti hili utaratibu ulienda vizuri katika kugawa vyandarua hivyo.

“Tunaendelea vizuri na mwitikio ni mzuri, lakini hapa tunakabiliwa na tatizo la watu ambao hawakuandikishwa kujitokeza kuchukua vyandarua wakiwa na kadi za kliniki,” alisema Leonard Madaha Ofisa Mtendaji wa mtaa wa Kasulu Kata ya Ilala.

Ofisa Mtendaji wa mtaa wa Tindwa Kata ya Sandali wilayani Temeke ambako hakukuwa na watu wanaochukua vyandarua, Yona Migwano alisema: “ Mtaa wangu ugawaji unakwenda vizuri, nilichofanya ni kuwashirikisha wajumbe ambao ndio wanawafahamu wananchi.

Pamoja na kuwa nimetakiwa kupeleka majina mawili ya wagawaji, lakini tuliona ni bora hawa wajumbe tuwagawie kiasi cha fedha ili kurahisisha kazi.” Kata hiyo imeandikisha watoto 504 na mpaka jana mchana walikuwa wamegawa vyandarua 438.

Katika mtaa wa Maendeleo A, Kata ya Sandali wilayani Temeke, zoezi lilikuwa linakwenda vizuri na changamoto waliyokutana nayo ni kwa baadhi ya wazazi kushindwa kupeleka watoto kituoni hapo.

“Sheria inatuagiza kuwa mtu anayepewa chandarua ni lazima aje na kadi ya kliniki na mtoto wake, lakini wengine watoto wamesafiri au wamelazwa mtu kama huyo hatuwezi kumpa hata kama tunamfahamu,” alisema.
HabariLeo | Naali, Mgosi, Chuji wachomoza TASWA

Tatizo hili la Ugonjwa wa Malaria Litaisha lini jamani? Bado tupo nyuma Kimaendeleo Nchi yetu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom