#COVID19 Uganda yazindua tiba ya majaribio ya dawa asili kutibu corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amezinduwa tiba ya majaribio ya kutibu virusi vya corona katika hospitali kuu ya taifa ya Mulago mjini Kampala kwa kutumia dawa asilia kutoka nchini humo.

Majaribio hayo yalitakiwa kuzinduliwa mwaka jana lakini yalicheleweshwa kwa kupata kibali kutoka Baraza la taifa la sayansi na tekinlojia yaani UNST.

Wakati wa uzinduzi wa dawa hiyo inayotengenezwa na wanasanayansi wa taifa hilo kwa kutumia miti ,Rais Museveni amelaumu mataifa ya Afrika kwa kutegemea mataifa ya Ughaibuni kupata tiba ya corona na chanjo badala ya kufanya utafiti wao wenyewe kwa kutumia wanasayansi wa mataifa yao.

Mmoja wa watafiti ,daktari Bruce Kirenga kutoka chuo kikuu cha Makerere anelezea majaribio ya dawa hiyo na idadi ya wagonjwa watakaonza kuwafanyia majaribio:

Kwa mjibu wa waziri wa afya wa Uganda, anasema majaribio hayo yamefuata ushauri wa Shirika la Afya duniani WHO, ikiwa kufikia leo idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona nchini Uganda imefikia watu 39, 261 huku wagonjwa 318 wamefariki na 14, 051 wamepona.

1611840305548.png
 
Heey. Natumai na yule wakwetu atafanya mambo very soon.

Yaani hata huyu mwanamgambo amemshinda!

No way
 
Hii tamthilia sijui ipo season gani cha msingi tuzidi kuchukua tahadhali japo za kiujanja ujanja.
 
Back
Top Bottom