Uganda yavunja mkataba na kampuni ya Urusi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
160701155434_museveni_and_park_512x288_afp.jpg

Serikali ya Uganda imevunja mkataba wake na kampuni ya Urusi kuhusu mpango wa kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta.

Serikali ilikuwa imekamilisha mazungumzo na kampuni hiyo ya Rostec Global Resources Consortium.

Lakini inasema baadaye kampuni hiyo ilianza kuongeza masharti mengine hata baada ya makubaliano ya mwisho kufikiwa. Mkataba huo sasa umekabidhiwa kampuni ya SK Engineering kutoka Korea Kusini.

Kampuni hiyo iliibuka ya pili katika shughuli ya kutoa zabuni. Hatua hiyo imejiri wiki chache baada ya Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye kuzuru Uganda.

Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom