#COVID19 Uganda yatangaza mgonjwa wa kwanza wa Corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Wizara ya Afya imethibitisha kisa cha kwanza cha Covid19 nchini Uganda. Waziri wa Afya Dkt Ruth Aceng amesema mgonjwa huyo ni mganda mwenye miaka 36 aliyerudi kutoka Dubai 21 Machi, saa nane usiku

Mtu huyo alienda Dubai Machi 17, alitumia siku nne huko kwa masuala ya kibiashara. Alikuwa na afya njema wakati anaenda Dubai Dkt Aceng alisema

Mtu huyo ametengwa, abiria wote waliosafiri nae wako karantini na passport zao zinashikiliwa na serikali ya Uganda

Kesi za CoronaVirus duniani hadi sasa ni 304,334, watu 12,983 wameripotiwa kufa, 94,677 kati ya waliopata CoronaVirus wamepona
 
Poleni Sana Waganda
Tuzidi Kumuomba Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Atunusuru
 
Uzuri Uganda washajipanga hata karantini walikua tayari wameziandaa kabla hata ya kupata kesi ya mgonjwa! Ila hapa bongo ndo kwanza tunataka kuaagiza sanitizer na mask uchina na wagonjwa wako zaidi ya 6...
 
Back
Top Bottom