Uganda yapitisha Sheria Mpya ya wahalifu kujichagulia hukumu

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,607
2,000
Nchini Uganda mfumo mpya wa kisheria umeanzishwa ambapo washtakiwa katika kesi za adhabu kali kama vile mauaji sasa watapewa fursa ya kujiamualia ni kiwango gani cha adhabu wapewe.

Katika huo mfumo huo mpya ,kuna matarajio kwamba mchakato wa kisheria wa kusikiliza kesi utakuwa wa haraka na kuokoa sio tu muda lakini pia gharama za kusikiliza kesi na kutoa hukumu.

Kulingana na mwandishi wa BBC Issac Mumena mshtakiwa ataweza kukiri kosa na kupewa muda wa kutoa adhabu dhidi yake.

Kulingana na mwandishi huyo hatua hiyo ni miongoni mwa mimkakati ya kupunguza mrundikano wa kesi Uganda.

Hilo ni kutokana na idadi ndogo ya majaji wa kusikiliza na kutoa hukumu kwa wakati mfupi na wa haki.

Hatua hiyo itapunguza muda na gharaza za kusikiliza kesi

Chini ya mchakato huo kuna matarajio kwamba mchakato wa kisheria wa kusikiliza kesi utakuwa wa haraka na wa kuokoa sio tu muda bali pia gharama za kusikliza kesi na kutoa hukumu.

Wakili na mwanasiasa Asuman Basalirwa amesifu mfumo huo. Kulingana na wakili huyo mtu atapewa fursa na jaji kukiri makosa aliyofanya na kumtaka jaji kumpatia kifungo hafifu.

''Mtu atakuwa na fursa ya kujadiliana kuhusu kiwango cha huku atakachopaewa. Iwapo mtu amefanya makosa atapelekwa mahakama na anapofika mahakamani anapewa fursa na jaji kumwambia jaji huyo kwamba yeye alifanya makasa hayo na sasa anaomba kupewa hukumu ndogo'', alisema.

Takwimu za kitengo cha sheria Uganda
Takwimu za kitengo cha sheria katika jela kuu ya Luzira zinasema kuwa kuna takriban kesi 1000 zinazostahili adhabu ya kifo ama kifungo cha maisha.

Iwapo mfumo huo utatumiwa unaweza kupunguza sana na kuwapatia fursa watu ambao hawakutenda makosa kusikilizwa kwa muda ufaao na kuwaachia iwapo waliotenda watakiri na kuhukumiwa haraka.

Afisa mkuu wa mawasiliano katika kitengo cha sheria Solomon Muyita anasema.

Makubaliano yatawasilishwa mbele, iwapo ni miaka 10 unaweza kuamua kwamba ingekuwa bora iwapo ungehudumia miaka miwili halafu mwendesha mashtaka anaweza kusema miaka miwili ni michache kwanini tusifanye mitano. Kumbuka kwamba unaweza kujadiliana kwa kutumia wakili wao ama hata wewe mwenyewe.

Miongoni mwa washtakiwa watakaonufaika chini ya mfumo huo ni wale wa kesi za mauaji , ubakaji, unajisi na ujambazi ambapo silaha zilitumika.
BBC
 

Ngamba

JF-Expert Member
Jun 6, 2013
732
225
Mtoa mada acha kupotesha watu, pre bargaining ni sheriali ambayo imekuwepo zaidi ya miaka 20, ni sio keli mtuhumiwa anajichagulia adhabu bali anaomba mahakama imwoneee huruma inapotoa adhabu
 

sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
5,154
2,000
Mtoa mada acha kupotesha watu, pre bargaining ni sheriali ambayo imekuwepo zaidi ya miaka 20, ni sio keli mtuhumiwa anajichagulia adhabu bali anaomba mahakama imwoneee huruma inapotoa adhabu
Kwa Uganda ilikuwepo kabla?
 
Top Bottom