Uganda yapiga marufuku kundi la uangalizi wa Uchaguzi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mamlaka nchini UgaDna imepiga marufuku miungano ya zaidi mashirIka 60 iliyobuniwa kuchunguza uchaguzi mkuu wa mwaka 2021 kwa misingi kwamba sio halali.

Ofisi ya Kitaifa ya Uganda ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali - ambayo inadhibiti shughuli za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali imesema shirika la kitaifa la uangalizi wa uchaguzi halijasajiliwa.

Ofisi hiyo imesema baadhi ya mashirika chini ya muungano huo hayajasajiliwa wala hayana kibali cha kuhudumu nchini humo

Mkuu wa ofisi hiyo, Stephen Okello, amesema kundi hilo linatakiwa kusitisha shughuli zake mara moja ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa umma.

Raia wa Uganda watashiriki uchaguzi mkuu wa urais na ubunge mwezi Januari mwaka 2021.

Shirika la kimataifa la Action Aid nchini Uganda, katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wake, limesema kundi hilo lilibuniwa mwezi uliopita kukuza uadilifu katika uchaguzi kuongeza imani ya raia na ushiriki.

Serikali ya Uganda imekuwa ikikosoa mashirika yasiokuwa ya kiserikali kwa kufanya kazi kwa maslahi ya nchi za kigeni kurejelea kazi ya serikali na kuhudumu katika mazingira yasiyoeleweka.

Mwaka 2017, polisi walivamia ofisi za karibu mashirika matatu ya aina hiyo kwa tuhuma za kujihusisha na shughuli haramu za kifedha na uasi ili kudhoofisha nchi
 
Back
Top Bottom