UGANDA yaongoza kwa ufasaha wa lugha ya kingereza barani Afrika

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Uganda imetajwa kuwa nchi yenye raia wanaozungumza lugha ya kingereza kwa ufasaha barani Afrika

Utafiti uliofanywa na Shirika la Lugha duniani World Linguistic Society umesema Uganda inaongoza ikifuatiwa na Zambia halafu Afrika Kusini ikiwa katika nafasi tatu na Kenya katika nafasi ya nne
4774316ec38c689177a3906d1aeac176.jpg
Kulingana na gazeti la The New Vison nchini Uganda, utafiti huo unajiri kufuatia kanda ya Video iliomuonyesha Malkia wa urembo kutoka Rwanda akishindwa kujielezea kiingereza

The New Vison linasema kuwa mwaka 2015 mmoja wa Malkia hao wa urembo katika shindano la Malkia wa urembo nchini Rwanda Uwase Honorine alishindwa kujibu maswali aliyoulizwa na majaji wa shindano hilo

Rwanda iliyokuwa chini ya koloni la Ufaransa ilianza kuzungumza kiingereza baada ya kukosana na Ufaransa

Gazeti la The New Vison linasema kuwa kingereza nchini Uganda ndio lugha rasmi, na ndio lugha inayotumiwa katika shule na taasisi tofauti nchini humo

Watoto huanza kujifunza lugha hiyo katika shule za msingi

The New Vison linasema kuwa hivi majuzi Serikali iliziagiza shule kufunza lugha za nyumbani kwa wale wanaosoma katika shule za msingi lakini ikasisitizia kuwa kingereza ndio lugha itakayotumiwa katika mtaala

Mataifa yanayozungumza kingereza kwa ufasaha :

1.Uganda
2.Zambia
3.South Africa
4.Kenya
5.Zimbabwe
6.Malawi
7.Ghana
8.Butswana
9.Sudan

Chanzo: BBC
 
Upuuzi tu huu! Kiingereza kizungumzwe kwa ufasaha kisizungumzwe mamangu kule kibosho kindi atadhurika ama kufaidi nini? Mbona mdingi mmoja kiingereza kinampa shida sana lakini anadunda tu ile mbaya?
 
By knowing better English, how much G.D.P. does Uganda and the other 8 got? And may be yes but their accent is uglier than ours, listen to Kansiime!!
 
Akheri kuboresha lugha yetu, hizi nchi hatuna tofauti kubwa sana nazo kimaendeleo. Lugha yetu ikikua na ikaweza kutumika katika masuala ya maendeleo, kwa hakika tutapiga hatua kubwa zaidi.
 
Hongera zao waganda. Idd Amin alitaka kuwaingiza chaka Kiswahili ila Mungu alikuwa upande wao. English ni lugha bora kabisa duniani; mataifa kutoka pande zote za dunia wanatafuta kuijua lugha hii adhimu.

Kiswahili na Kiarabu kwa mfano, ndizo lugha zenye maneno na tungo nyingi zaidi za matusi. Hakuna lugha inayofikia lugha hizi kwa matusi na mipasho ya nguoni. Kwenye matusi na mipasho tuko vizuri.
 
Ninaweza kuamini hili, rafiki zangu wa-Ganda, Kiingereza ndiyo lugha ya kwanza mpaka kijijini ndiyo lakini pia wanaongea ki lugha.
 
Uganda imetajwa kuwa nchi yenye raia wanaozungumza lugha ya kingereza kwa ufasaha barani Afrika

Utafiti uliofanywa na Shirika la Lugha duniani World Linguistic Society umesema Uganda inaongoza ikifuatiwa na Zambia halafu Afrika Kusini ikiwa katika nafasi tatu na Kenya katika nafasi ya nne
4774316ec38c689177a3906d1aeac176.jpg
Kulingana na gazeti la The New Vison nchini Uganda, utafiti huo unajiri kufuatia kanda ya Video iliomuonyesha Malkia wa urembo kutoka Rwanda akishindwa kujielezea kiingereza

The New Vison linasema kuwa mwaka 2015 mmoja wa Malkia hao wa urembo katika shindano la Malkia wa urembo nchini Rwanda Uwase Honorine alishindwa kujibu maswali aliyoulizwa na majaji wa shindano hilo

Rwanda iliyokuwa chini ya koloni la Ufaransa ilianza kuzungumza kiingereza baada ya kukosana na Ufaransa

Gazeti la The New Vison linasema kuwa kingereza nchini Uganda ndio lugha rasmi, na ndio lugha inayotumiwa katika shule na taasisi tofauti nchini humo

Watoto huanza kujifunza lugha hiyo katika shule za msingi

The New Vison linasema kuwa hivi majuzi Serikali iliziagiza shule kufunza lugha za nyumbani kwa wale wanaosoma katika shule za msingi lakini ikasisitizia kuwa kingereza ndio lugha itakayotumiwa katika mtaala

Mataifa yanayozungumza kingereza kwa ufasaha :

1.Uganda
2.Zambia
3.South Africa
4.Kenya
5.Zimbabwe
6.Malawi
7.Ghana
8.Butswana
9.Sudan

Chanzo: BBC

Wameishinda hata Shelisheli? Au Sheli sheli haipo Barani Afrika? Kwa maana Washelisheli sehemu kubwa ni Wazungu native speaker wa English language!
 
Kama kuna mtu bado anaona kingereza akifahi basi ni juha. Nasema ni juha kwasababu waswahili mnasahau sana, kila siku mnachekana hapa kuhusu kingereza ikimaanisha bado tunaikubali ni lugha ifaayo kufahamika kwasasa duniani.

Wengi wetu watanzania hatuna confidence kwakuwa english hatujui ukiambiwa leo kuna kazi ubalozi flan au sehemu flani interview ni kingereza unahaha.

Bado hata kwenda nje na kufanya biashara za kimataifa hatuwezi kwakuwa hatujui wengi wetu kingereza au tuna broken ya kufa mtu.

Mnasahau mnamcheka kiba kila siku pamoja na sizonje, hii nikuonesha english ni bora katika dunia ya sasa na tunaihtaji kuliko wakati mwingine wowote. Watanzania hawana marafiki nje wakuwapa exposure kisa tu lugha ni tabu.

Na kama english mnasema si kitu basi kubalini iondolewe hata Sekondari na isiwe second language ya Taifa hili muone aibu yake. Watu wanasema ukoloni, mnaona kwenye lugha tu? Alietangulia katangulia hakuna jinsi basi hata vitu kama simu vya mzungu tunavyotumia ni ukoloni, tengenezeni vifaa vyenu vya kibongo ili tujue hamtaki ukoloni na mpo huru.

Alietangulia katangulia tu English ndio lugha maarufu kwasasa duniani katika nyanja zote
 
Kama kuna mtu bado anaona kingereza akifahi basi ni ****. Nasema ni **** kwasababu waswahili mnasahau sana, kila siku mnachekana hapa kuhusu kingereza ikimaanisha bado tunaikubali ni lugha ifaayo kufahamika kwasasa duniani.

Wengi wetu watanzania hatuna confidence kwakuwa english hatujui ukiambiwa leo kuna kazi ubalozi flan au sehemu flani interview ni kingereza unahaha.

Bado hata kwenda nje na kufanya biashara za kimataifa hatuwezi kwakuwa hatujui wengi wetu kingereza au tuna broken ya kufa mtu.

Mnasahau mnamcheka kiba kila siku pamoja na sizonje, hii nikuonesha english ni bora katika dunia ya sasa na tunaihtaji kuliko wakati mwingine wowote. Watanzania hawana marafiki nje wakuwapa exposure kisa tu lugha ni tabu.

Na kama english mnasema si kitu basi kubalini iondolewe hata Sekondari na isiwe second language ya Taifa hili muone aibu yake. Watu wanasema ukoloni, mnaona kwenye lugha tu? Alietangulia katangulia hakuna jinsi basi hata vitu kama simu vya mzungu tunavyotumia ni ukoloni, tengenezeni vifaa vyenu vya kibongo ili tujue hamtaki ukoloni na mpo huru.

Alietangulia katangulia tu English ndio lugha maarufu kwasasa duniani katika nyanja zote
Umesema sawa kabisa.. ila inaonekana hujasafiri wewe na ukaona jinsi nchi za wenzetu ambavyo zinathamini lugha zao..

Huu upumbavu wa kuzungumza kiingereza vizuri huwezi kuukuta Japan au Urusi au Ujerumani..

Kwanza hakuna nchi hata moja duniani ambayo imeendelea kwa kutegemea lugha ya kuazima

Kama akili zako zimeishia kujua kiingereza ili uajiriwe ubalozini basi sawa, ila ufahamu tu FIKRA SAHIHI HUJA KWA LUGHA SAHIHI..
 
Nchi zote hizo ambazo zina wazungumzaji wazuri wa Kiingereza ukiacha Afrika Kusini zote ni maskini..

Hao Uganda hata kimaendeleo tumewapita mbali sana..
 
Umesema sawa kabisa.. ila inaonekana hujasafiri wewe na ukaona jinsi nchi za wenzetu ambavyo zinathamini lugha zao..

Huu upumbavu wa kuzungumza kiingereza vizuri huwezi kuukuta Japan au Urusi au Ujerumani..

Kwanza hakuna nchi hata moja duniani ambayo imeendelea kwa kutegemea lugha ya kuazima

Kama akili zako zimeishia kujua kiingereza ili uajiriwe ubalozini basi sawa, ila ufahamu tu FIKRA SAHIHI HUJA KWA LUGHA SAHIHI..
Sasa wewe na ujerumani na japan na urusi mnajifananisha? Acha umbwela wewe, uwezi jilingaNJisha na mataifa yalioendelea tangu hata kingereza hakijawa lugha maarufu duniani.

Leo nchi yako hata sindano za kushonea zinatoka nje wewe leo unataka uwe kama ujerumani na japane ambako usipowafata kwa lugha yao utawafata kwa tecnolojia na uchumi wao.

Unasema sijasafiri, nikupe kopi ya passport yangu? Poor u

Kila nchi duniani, hata huko unakotaja wanasaka walimu wakingereza kwa udi na uvumba, kwa taarifa yako japane ina shule nyingi za kingereza kuliko shule za primary Tanzania. Na wanatafta walimu kutoka nchi za kingereza kila siku. Kama imekuingia njoo na fact mpya.

English bado ni lugha bora kwa sasa dunian katika nyanja zote
 
Akheri kuboresha lugha yetu, hizi nchi hatuna tofauti kubwa sana nazo kimaendeleo. Lugha yetu ikikua na ikaweza kutumika katika masuala ya maendeleo, kwa hakika tutapiga hatua kubwa zaidi.
Naunga mkono hoja... Mbona hata nchi zilizoendelea kiingereza hakitiliwi maanani..! China, Ujerumani, Japan
 
Hongera zao waganda. Idd Amin alitaka kuwachomekea Kiswahili ila Mungu alikuwa upande wao. English ni lugha bora kabisa duniani; mataifa kutoka pande zote za dunia wanatafuta kuijua lugha hii adhimu.
Ni lugha bora... Lakini si muhimu kivile
 
Wameishinda hata Shelisheli? Au Sheli sheli haipo Barani Afrika? Kwa maana Washelisheli sehemu kubwa ni Wazungu native speaker wa English language!
Hivi Visiwa kule kuwa na wazungu kutoka mataifa mbalimbali na kuchanganyika na wenyeji ndo imeharibu sifa hata ya kuingia kumi bora..!
 
Back
Top Bottom