Uganda yakamata washukiwa wa ugaidi huku wengine 7 wakiuawa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
4,044
2,000
Uganda inasema kwamba washukiwa saba wameuwawa na wengine 106 wanashikiliwa kutokana na matukio ya kigaidi.

Hayo yametokea wakati wa oparesheni iliyofanywa na vikosi vya usalama wakihusishwa na washukiwa watatu wa mabomu ya kujitoa muhanga katika mji mkuu Kampala wiki iliyopita, kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la Reuters ya Jumatatu.

Kundi la Islamic State ambalo lina ushirikiano na kundi la uasi la Uganda la Allied Democratic Forces (ADF) limedai kuhusika na shambulizi la Nov 16, ambalo limeuwa watu saba ikijumuisha watu watatu waliojitoa muhanga, na kujeruhi dazeni zaidi.

Afisa mmoja wa polisi alikuwa miongoni mwa wengine wanne waliofariki dunia na kati ya watu 37 waliojeruhiwa 27 walikuwa ni maafisa wa polisi.
Polisi haukutoa taarifa za kina za namna ya washukiwa hao saba walivyo uliwa.
 

masonya

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
934
1,000
Hawatakiwi kuwa hai, mkiwatambua wahusika miongoni mwao hakuna kuwapeleka mahakamani wameua wauawe wawahi peponi kukutana na bikra 70 msifanye makosa Kama Kenya hawahitaji. Huku Tanzania pale kibiti hakuna aliyepelekwa mahakamani. Mkiwalea ya msumbiji halali yenu
 

NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
11,208
2,000
kwa mfano mama na katoto kake kachanga wamepita eneo lililolipuka alafu wanapoteza maisha ni faida ipi hao isis wanapata?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom