Uganda yafuta mradi wa kufua umeme wa maji

Catarina anna

Member
Jul 26, 2019
14
7
Uganda imeachana na mradi wa kujenga bwawa la kufua umeme katika maporomoko ya maji ya Marchison. Mradi huo ulikuwa ukikosolewa sana na walinzi wa mazingira na wadau kadhaa wa sekta ya utalii.

Serikali ya Uganda inaashiria mradi huo wa umeme wenye uwezo wa kutoa megawatt 360 "ungechafua mandhari na kuvuruga mfumo wa ikolojia na kwa namna hiyo ungeharibu pia shughuli za utalii.Zaidi ya watalii 100.000 wanatembelea kila mwaka maporomoko ya Murchison ili kujionea maajabu ya dunia.

Kwa mujibu wa waziri wa utalii Ephraim Kamuntu serikali imepitisha uamuzi huo kaatika kikao cha hivi karibuni cha baraza la mawaziri. Uchumi wa Ugaanda unanawiri kwa mujibu wa benki kuu ya dunia ukuaji wa kiuchumi unafikia asili mia sita kwa mwaka nchini humo.
 
Back
Top Bottom