UGANDA: Watanzania 13 wa familia ya Gregory Teu, wafariki katika ajali. Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Ajali Uganda.jpg

Watu 13 wamepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea Katonga wilayani Mpiji nchini Uganda.

Ofisa wa polisi wa Katonga, Philip Mukasa amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu ikihusisha basi aina ya Toyota Coaster lililogongwa na lori.

Mukasa amesema basi lililohusika katika ajali hiyo lina namba ya usajili ya Tanzania na lori lina namba za Uganda.

Amesema lori lililokuwa katika mwendokasi lilipasuka gurudumu hivyo kuyumba na kugonga gari hilo la abiria.

CHANZO: Mwananchi

---
Tangazo la Ajali ya Gari TZ 540 DLC

Gari tajwa hapo juu lilipata ajali karibu na mto Katonga, barabara ya Masaka kuamkia leo tarehe 18/09/2017.

Lilikuwa likiwarudisha Watanzania wa Familia ya Bw Gregory Teu ambao walikuja kwenye harusi tarehe 16/09/2017 hapa Kampala. Bibi harusi ni mtoto wa Bw na Bibi Gregory Teu wa Dar es salaam.

Jumla ya abiria waliokuwa kwenye gari ni abiria 19. Kati yao 13 wamefariki dunia na 6 wamelazwa Nsambya hospital.

Ubalozi unaendelea kufuatilia msiba huu pamoja na kupata majina yote ya waliokufa na kunusurika.

Naibu Balozi Mh. Maleko pamoja na Brigedia Generali S S Makona wameelekea Nsambya Hospital kuona Walio nusurika.

Asante sana

Ofisi ya Ubalozi

--------
Majina ya waliofariki dunia...

Teu.png


----------------------------------------------
Rais Magufuli amtumia salamu za rambirambi Naibu Waziri wa zamani, Gregory Teu kufuatia vifo vya watu 13 wa familia yake kwa ajali ya gari.​

Teu.jpg

 
R. I. P Mwenyezi Mungu akawe faraja kwa ukoo huo unapitia katika kipindi kigumu sana
 
Hao wazikwe huko huko Uganda... Poleni ukoo kwa yaliyowafika... The scene of accident has literally broken my heart in pieces...
 
Nilivyoona picha za jana usiku za ajali hii zikihusisha gari yenye namba za Tanzania nikakata hata tamaa ya kufuatilia maana nilijua msiba wetu huu! Kweli Mungu ana mipango Yake!
 
Back
Top Bottom