#COVID19 Uganda: Serikali yatoa Tsh Bilioni 69.5 kununua magari ya wabunge wakati visa vya COVID-19 vikiongezeka

Parody

Member
Sep 13, 2020
24
69
Wananchi wa Uganda wameonesha kukasirishwa na hatua ya serikali ya nchi hiyo kutoa zaidi ya dola milioni 30 za Marekani (sawa na zaidi ya Tsh bilioni 69.5) fedha za kununua magari ya wabunge wakati taifa hilo likiwa katikati ya mapambano dhidi ya virusi vya corona na kuinua uchumi wa nchi kutokana na athari za virusi hivyo.

Serikali ya nchi hiyo imetoa kiasi cha Shilingi milioni 200 za Uganda (sawa na Tsh milioni 130.9) kwa kila mbunge, ili wabunge wote 529 wapate magari, wakati visa vya maambukizi ya Covid-19 vikiongezeka.

Wengi wamedhihirisha hasira zao kupitia mitandao ya kijamii wakati ambapo taifa hilo likiwa katika masharti ya kutotoka nje kwa muda wa wiki sita

Hasira za wananchi hao zinachochewa na tofauti ya kipato cha mbunge na mwananchi wa kawaida ambapo Watunga Sheria hao wanalipwa zaidi ya Tsh milioni 18 kwa mwezi wakati mshara wa wastani wa mwalimu ukiwa Tsh. 170,000 kwa mwezi huku mfanyakazi (manual laborer) akipokea Tsh. 65,000 kwa mwezi.

Taifa hilo lenye wakazi milioni 45 limeshuhudia visa 91,710 vya maambukizi ya Covid-19 na vifo 2,496. Takriban watu milioni 1 pekee ndio waliopatiwa chanjo.

1627192712678.png
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom