UGANDA: Mtoto wa miaka 10 amuua mwenzake kwa wivu wa mapenzi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,193
4,105
Polisi wilayani Bududa mashariki mwa Uganda wanamsaka mwanafunzi wa miaka 10 kwa tuhuma za kumchoma kisu mwenzake ambaye alidai kupora mpenzi wake wa miaka 11. Mtuhumiwa huyo, ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Buwali.

Polisi walimtambulisha mwathirika huyo kama Sam Watsosi, 16. Watsosi alidaiwa kuchomwa na kisu siku ya Jumapili kwa tuhuma kwamba alikuwa akihusiana na mpenzi wa muda mrefu wa mtuhumiwa.

Baada ya tukio hilo, lililotokea Bunamubi, Watsosi alikimbizwa katika hospitali ya Bududa akitokwa na damu nyingi. Alifariki Jumatatu jioni.

Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Bududa (DPC) Bwana Jaffar Magayisi, alithibitisha tukio hilo Jumatano asubuhi na kusema walikuwa wanamsaka mtuhumiwa.

"Tunamsaka mwanafunzi huyo, ambaye kwa sasa amekimbia na baba yake kufuatia kifo cha mwenzake," alisema.

Kuna mvutano mkubwa katika eneo hilo kwani ndugu za marehemu walitishia kushambulia familia ya mtuhumiwa kwa kulipiza kisasi.

Lakini DPC aliwataka familia ya Watsosi itulie, akisema mtuhumiwa atakamatwa na kushtakiwa kwa mauaji mahakamani

Bwana Charles Mutabali Kibeti, mwenyekiti wa LCIII alisema "Inashangaza sana kuwa mtoto wa miaka 10 anaweza kuwa na rafiki wa kike, ambaye yuko tayari kufanya chochote kumlinda akiwa na umri mdogo,"
 
Ama kweli dunia tambara mbovu,
Sasa 10yrs , halafu ana mpenzi wa muda mrefu!! Akili inakataa aisee, walianzana wakiwa na umri gani sasa!R.I.P mtoto uliyechomwa kwa kisuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom