Uganda: Msichana wa miaka tisa mwenye asili ya Congo afariki kwa ugonjwa wa Ebola.

mbahachu

Member
Jul 26, 2019
19
10
Maafisa nchini Uganda wanasema msichana wa miaka 9 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo aliyethibitishwa kuwa na virusi vya Ebola Alhamisi amefariki Uganda akipokea matibabu.

Maafisa wanaeleza kwamba alifariki wakati mazungumzo yakiendelea kuhusu kumrudisha DR Congo kwa matibabu.

Mamake msichana huyo aliyewasili na mwanawe Uganda kupitia mpaka wa nchi hiyo na Congo wa Mponde - ametengwa na atarudisha nchini alikotoka kuangaliwa zaidi.

Mama na mwana huyo wanaarifiwa kuingia Uganda ambako walifika kutafuta matibabu.

Wizara ya afya Uganda ilithibitisha kisa hicho kipya cha ugonjwa wa Ebola katika mji wa magharibi wa Kasese.

Msichana huyo alipatikana akiwa na homa wakati wa ukaguzi wa Ebola katika eneo la mpaka wa Mpondwe.

Sampuli ya damu iliyotumwa kufanyiwa ukaguzi jana Alhamisi jioni imethibitisha kwamba anaugua Ebola.

Dalili za awali huenda ni pamoja na homa ya ghafla, kudhoofika haraka, maumivu ya misuli na kuumwana koo.

Kiwango kinapozidi mtu anaweza kuanza kutapika, kuharisha na mara nyingine - kuvuja damu ndani na nje ya mwili.

Msichana huyo alitengwa na kuhamishwa katika kituo cha kuwashughulikia wagonjwa wa Ebola.

Uganda imeidhinisha na kuendeleza kwa ufanisi vituo vya ukaguzi katika mpaka wake na Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo katika jitiahada ya kuuzuia mlipuko uliosababisha vifo vya karibu watu 2000 katika mwaka uliopita.

Mnamo Juni, kuliripotiwa visa viwili vya Ebola nchini humo.Mwanamume raia wa Uganda na mkewe wa Congo waliwapoteza watoto wao wawili wa kiume baada yakurudi kutoka safari katika Jamahuri ya Kidmeokrasi ya Congo walikokwenda kuwaona jamaa zao.
Mgonjwa kusafirishwa kurudishwa Congo:

Akizungumza na BBC mapema hii leo, msemaji wa wizara ya afya nchini Uganda, Ainebyoona Emmanuel ameeleza kwamba wizara ya afya Uganda inashirikiana kwa karibu na wizara ya afya huko DRC kuona namna msichana huyo na mamake wanaweza kurudishwa nchini Congo ambako kuna matibabu bora dhidi ya Ebola.

"Msichana huyo na mama yake waliingia nchini kupitia mpaka wa Mpondwe kutafuta matibabu katika wilaya ya Bwera Kasese na alitambuliwa katika eneo hilo la kiingilio na kikosi cha ukaguzi akiwa na dalilia zifuatazo; joto jingi, mwili kudhoofika, upele na damu inayovuja kutoka mdomoni. Alitengwa na kufikishwa katika kitengo cha hospitali ya Bwera ambapo anashughulikia hivi sasa," taarifa ya wizara ya afya ilieleza Alhamisi.

Alipoulizwa iwapo ni jambo la busara kumsafirisha mgonjwa huyo, kwa kuzingatia dharura ya kumtibu mgonjwa anapogunduliwa kuwa na Ebola, msemaji huyo ameelza kwamba ni uamuzi wanaoweza kuuchukua.

Na zaidi uamuzi huo umechukuliwa kwasababu kuna matibabu bora nchini Congo na ombi hilo limeidhinishwa kutokana na kwamba maafisa wa kutoka DRC watafika Uganda na matibabu na kuhakikisha kwamba mgonjwa anahudumiwa wakati wote anapokuwa katika safari ya kurudi Congo.
 
Mungu wangu, wanasema UKIMWI ulingiia Tanzania kutoka Uganda kupitia "Katerero", tutapona kweli nahiyo EBOLA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom