Uganda: Mama amlisha mtoto wake damu ya hedhi na bilinganya

Invigilator

JF-Expert Member
Aug 16, 2016
3,207
5,990
Mwanamke mmoja anaefahamika kwa jina la Annet Namata nchini Uganda amempa mtoto binti yake wa kambo chakula alichokichanganya na damu yake ya hedhi.
Baada ya kula chakula hicho ambacho damu ya dada huyo ilichanganywa na mchuzi wa biringanya mtoto huyo alianza kutapika mfululizo nje varandani.Wakati huo mwanamke huyo (Annet) alikuwa tayari keshatoka kwenda matembezini(kuzulula).

Bahati majirani walimuona mtoto huyo akitapika mfululizo walimfuata kumuuliza tatizo,akiwa hawezi hata kuongea aliwaonyesha sahani ya chakula ambapo waliona vitu vya ajabu ndipo wakamtaarifu mume wa Annet Bwana Unusu Lungu. Baada ya kuja kujionea mume huyo alipatwa na hasira kali akamfuata mkewe huyo alipo kisha kuanza kumpiga hadi alipokili kutenda unyama huo.

Awali, Annet Alijitetea kuwa mtoto huyo wa kike umri wa Shule ya msingi alichukuwa mwenyewe damu hiyo ya hedhi Kwenye ndoo akachanganya na chakula ale. Alieleza hayo baada ya yeye kulazimishwa ale chakula hicho ndipo akasema kina damu ya hedhi yeye hawezi kula.

Alipobanwa zaidi na mumewe Na mmoja wa viongozi wa kike wa eneo Hilo amekiri kumuwekea mtoto vitu hivyo akisema anaomba msamaha kwani mumewe alikuwa akimpenda sana mwanae kuliko yeye hata zawadi nyingi humnunulia mwanae kuliko yeye. Ndipo akapandwa na hasira akafanya hivyo baada ya kuwaeleza mashoga zake ambao anadai ndio walimshauri Annet achukue damu yake ya hedhi amuwekee mtoto huyo kwenye chakula Ili awe mwendawazimu na upendo uhamie kwake.

Suala Hilo limefikishwa police Kwa hatua zaidi huku mtoto huyo akipatiwa huduma.
 
Attachments

  • FB_IMG_1560434009877.jpeg
    FB_IMG_1560434009877.jpeg
    20.4 KB · Views: 87

Huyu anatakiwa anyongwe tu
 
Back
Top Bottom