Uganda. Mama aliyejifungua mapacha wawili wenye baba tofauti

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Katika hali ya kushangaza huko nchini Uganda, wanaume wawili na watu wengine wamejikuta kwenye mshangao baada ya kukuta wote wawili ni baba wazazi wa watoto wawili mapacha.

Inaelezwa kuwa wanaume hao waliingia kwenye mgogoro siku za hivi karibuni kila mtu aking’ang’ania kuwa baba mzazi wa mapacha hao, na ndipo walipoamua kwenda hospitali ili kupima kipimo cha DNA.

Hatahivyo matokea ya daktari yalionesha kuwa wanaume hao wote wawili ni baba halali wa mtoto mmoja wa mapacha hao, yaani kila mmoja ana mtoto mmoja kati ya mapacha hao.

Inaeelezwa kuwa wanaume hao Joseph Baseka Sengendo, 25, na Patrick Ssegane, 30, wamezaa na Rashida Nakabugo, ambapo Sengendo anatajwa kuwa mume wa ndoa wa mwanamke huyo.

Wanaume hao wanasemekana kuwa ni ndugu
.
 
Habari tata kama hizi ..weka link..usikute wewe hujaelewa vizuri kilichoandikwa humo.
 
Duh
Halafu ni ndugu.. huyo mke bomuuuuu
Watu wa ajabu sana. Wengine wanaona raha kugonoka na kila mtu. Huyo mwanamke kwa msemo wako ni bomu tena nyuklia. Anabahati sana angekuwa bongo huyo lbd angesubiri siku ya Makonda.
Dunia hii utagonoka na wangapi?
 
Utakuwa ni uganga na ushirikina... Hakuna Biology kama hiyo..
Genetically itakuwa huyo mdada alifanywa kwa muda ambao haukupishana sana kumbuka muda wa sperm za X kufanya uchevushaji kwa Y ni mrefu kidogo
 
Katika hali ya kushangaza huko nchini Uganda, wanaume wawili na watu wengine wamejikuta kwenye mshangao baada ya kukuta wote wawili ni baba wazazi wa watoto wawili mapacha.

Inaelezwa kuwa wanaume hao waliingia kwenye mgogoro siku za hivi karibuni kila mtu aking’ang’ania kuwa baba mzazi wa mapacha hao, na ndipo walipoamua kwenda hospitali ili kupima kipimo cha DNA.

Hatahivyo matokea ya daktari yalionesha kuwa wanaume hao wote wawili ni baba halali wa mtoto mmoja wa mapacha hao, yaani kila mmoja ana mtoto mmoja kati ya mapacha hao.

Inaeelezwa kuwa wanaume hao Joseph Baseka Sengendo, 25, na Patrick Ssegane, 30, wamezaa na Rashida Nakabugo, ambapo Sengendo anatajwa kuwa mume wa ndoa wa mwanamke huyo.

Wanaume hao wanasemekana kuwa ni ndugu
.

dah nimeikumbuka probability and ale lies
 
Madaktari na wakunga wabobezi hawashangai. Japokuwa hutokea kwa nadra na pia wachache wanaweza fuatilia hili.
 
Back
Top Bottom