Uganda, Maandamano kupinga ukomo wa umri wa rais; Meya wa Kampala akamatwa, Polisi wafunga ofisi za wapinzani

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Polisi nchini Uganda wamezifunga ofisi za chama cha upinzania cha 'Forum for Democratic Change (FDC)' kutokana na kupanga kufanya maandamano kupinga ukomo wa umri wa mgombea urais. Polisi wamekaa nje ya makao makuu ya ofisi Najjanankumbi hakuna anayeruhusiwa kuingia ofisini humo.

FDC.jpg

Wakuu wa chama hicho walikuwa wamepanga kuandamana kuelekea bungeni leo ili kumshinikiza spika wa bunge kutokuruhusu majadiliano kuhusu mswada huo wa ukomo wa umri wa mgombea urais kufanyika.

Ulinzi umeimarishwa kwenye mji mkuu wa Uganda, Kampala kutokana na kupangwa kwa maandamano hayo.

Kwenye taarifa iliyotolewa jumatano usiku, IGP Gen Kayihura alisema wamepokea taarifa kuwa kuna makundi ya watu wamepanga kuandamana kwenye mji mkuu na sehemu nyingine za nchi ili kupinga kujadiliwa huko kwa mswada wa ukomo wa umri. Pia aliwaonya waganda kutokufanya hivyo.

Pia, Meya wa jiji la Kampala, Erias Lukwago amekamatwa na polisi.

Bwana Lukwago amekamatwa asubuhi ya leo nyumbani kwake Wakaliga, Rubaga jijini Kampala akiwa anajiaandaa kwenda kazini.

mr.jpg


Bwana Lukwago na makundi mengine ya viongozi walipanga leo kuandamana kutoka City hall mpaka City Square ambapo walipanga kuenda kuzindua kampeni ‘Togibikula’ ili kupinga marekebisho ya katiba kuhusu ukomo wa umri wa urais.

Amepelekwa katika kituo cha polisi Kira.

Mapema, Bwana Lukwago alimwambia mwandishi wa habari kupitia simu kuwa polisi wamezingira nyumba yake kuanzia majira ya saa kumi na moja asubuhi.

“Nimeamka saa kumi na moja asubuhi na kukundua kuwa polisi wamezingira nyumba. Wamenizuia na kutoniruhusu kuondoka nyumbani kwangu” alisema Bwana Lukwago.
 
Madaraka ndicho kitu pekee waafrika wanakithamini! Wapo tayari kuua ndugu zao ili waendelee kuwa madarakani!
Viongozi wa aina hii kamwe hawawezi kuisaidia Afrika.
Nasi tumeingiza ujinga huo kwenye siasa zetu!
 
Back
Top Bottom