Uganda kutumia ndege zisizo na rubani kusafirisha ARVs kwa wakazi wa Visiwa vya Ziwa Victoria

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Wakati chupa za dawa zikipakiwa katika ndege zisizokuwa na rubani kwa ajili ya kusafirishwa, kundi la watu limekusanyika kwa mbali kutazama ndege hiyo yenye upana wa mita 1.5 katika eneo la Kituo cha Afya cha Bufumira III, jimbo la Kalangala nchini Uganda.

Mzigo huo wa dawa za kufubaza makali ya VVU (Antiretrovial Drugs, au ARVs) unatarajiwa kuwafikia wananchi zaidi ya 1,000 walioathirika na Virusi Vya Ukimwi katika eneo la visiwa vya Ssese ndani ya Ziwa Victoria lenye vituo 78 vya afya, ambalo lina maambukizi ya juu zaidi ya VVU nchini humo.

Eneo hilo lina kiwango cha maambukizi cha asilimia 18, zaidi ya wastani wa Kitaifa wa maambukizi wa asilimia 5.6, huku ripoti zikionesha kuwa kiwango cha maambukizi kinafikia asilimia 40 katika baadhi ya jamii za wavuvi.

Matumizi ya ndege zisizo na rubani yanaonesha mapinduzi ya kiteknolojia katika kuwafikia wananchi hao wanaoishi katika maeneo yasiyofikika kwa urahisi. Ndege hizo zinazogharimu takriban Tsh. milioni 11 kila moja, zinaweza kubeba hadi kilo moja ya dawa na kusafiri umbali wa hadi kilomita 150.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Magonjwa ya Kuambukiza ya Chuo Kikuu cha Makerere (IDI) ameipongeza hatua hiyo akisema kuwa matumizi ya ndege hizo yatawawezesha watoa huduma za afya kutekeleza majukumu mengine kwa ufanisi na kuwezesha kuwa na jamii yenye afya zaidi.

IDI imeshirikiana na Serikali ya Uganda kupitia Wizara ya Afya na Chuo cha Ubunifu wa Afya, wakitumia wataalamu wa ndani waliopewa mafunzo kurusha na kuongoza ndege hizo.

Licha ya kupongezwa kwa kuondoa changamoto ya ubovu wa barabara katika kufikisha huduma, mradi huo unakabiliwa na changamoto ya uhaba wa dawa kutokana na fedha kidogo zilizotengwa katika bajeti ya Afya.

Mataifa mengine ya Afrika kama Rwanda na Ghana yanatumia ndege zisizo na rubani kusafirisha dawa na sampuli za damu, yakiwahudumia zaidi ya watu milioni 22.

Chanzo: The Guardian

1620134141717.png

1620134155564.png
 
hata Tanzania mbona ipo hiyo?

Back
Top Bottom