#COVID19 Uganda kumuenzi iddi amin je historia ilipindishwa?

Ni vyema ukawa mchunguzi wa histry na kuzungumzia ukweli kuliko hisia tetesi na mihemko hasa ukizingatia watu humu ndani Ni wepesi kuaminisha...
Amin alitaka mpaka wake uwe bandari ya Tanga na alitamka hivyo akiikanyaga kanyaga bendera ya CCM pale alikuwa njiani tuu...
Kwenye aya ya mwisho pale "kuikanyaga kanyaga bendera ya CCM" ingekuwa imetokea miaka ya hivi karibuni hata Tanzania kungekuwa na vita (sisimua dhidi ya washangiliaji) vya wenyewe kwa wenyewe.
 
Bahati mbaya Historia ya Amini inaandikwa kwa kalamu ya Maadui zake na kusomwa katika miwani ya Maadui zake na wasio maadui zake wanajua Historia nyingine kabisa
 
Hakuna jema alilolifanya kaidada zaidi ya hayo mapicha yaliyotupiwa hapo juu.... Alikuwa kibaraka mkubwa wa mkulima wa kizungu Bob astless na hili liko wazi Sana... Alikuwa kibaraka wa queen Elizabeth na kwa hili histry haidanganyi....
Alimuua yule General mzuri maskini nimesahau tuu jina lake mwanzoni kabla ya mapinduzi.. akaruka kwenye kilichotajwa seng'eng'e kwenye vitabu vya kumbukumbu kiasi Cha kujeruhika mwili wake mbona hili lipibwazi Sana. Kwa ushauri wa Bob na kwaamri yake alimuua Askofu Janan Luwumu maskini asiye na hatia na kusingizia ajali ya gari.. mbona hili sio Siri na Ni yeye na Bob walionekana lastly na marehemu.
Yapo maovu mengi jamaa amefanya na kumbuka dunia haikumuona Kama dikteta hakukuwepo walio kuwa upande wa mwalimu rejea malalamiko aliyoyatoa mwalimu kipindi kile.
Msimponde mwalimu kwa kila issue nyie vijana muwe na utu
Echolima mkongwe Kuna uzi huku
Nimeambatanisha picha ya Askofu Luwumu RIP
View attachment 1193184View attachment 1193185
mtwa mkulu
Makosa makubwa 6 aliyoyafanya IDD AMIN kwenye utawala wake ambayo wananchi wa Uganda na Dunia nzima hawawezi kuyasahau wala kumsamehe wala kum-enzi.

1.1971 Baada tu ya kunyakua madaraka kutoka kwa Dr.Milton Obote alianza kuua wanajeshi wa kabila la Acholi na Langi kwa sababu tu makabila hayo jeshini ndiyo walikuwa wengi na alijua walikuwa wanamuunga mkono Dr Obote.Kwa hali kama hiyo jamii ya makabila hayo hayawezi kabisa kum-enzi na hayawezi ku,sahau kwa unyama aliowafanyia vijana wao.

2.1972 Mwezi Agost IDD AMIN aliwafukuza wananchi wa Uganda wenye asili ya Asia kwa kisingizio cha vita vya kiuchumi na aliwapa siku 90 wawe wameondoka Uganda,Kisha kuwamilikisha jamaa zake biashara kubwakubwa na majumba ya waasia hao aliwagawia jamaa zake kitu kilichokuja kusababisha mdololo wa uchumi maana waliokabidhiwa biashara hizo hawakuwa na ujuzi wa biashara hizo.

3.1973 Mauaji ya watu mashuhuri nchini Uganda yalishamiri watu wenye Elimu waliuliwa kwa visingizio mbalimbali
4.1974-1976 Mauaji ya maafisa wa kijeshi wa Jeshi la Uganda kwa visingizio vya kula njama za kumpindua vilevile alianzisha uhasama na nchi zingine(Annoying Other Countries) Mbali ya Kuanzisha uhasama na nchi ya Tanzania IDD AMIN aliwachokonoa sana Kenya ambao nao walijibu kwa kufunga mpaka wao na Uganda hivyo kusababisha nchi ya Uganda kuzidi kudolola kiuchumi,Ikumbukwe kuwa Bandari ya Mombasa nchini Kenya ndiyo ilikuwa inapitisha mizigo yote ya Uganda hivyo kufungwa kwa mpaka kuliifanya Uganda kuumia kiuchumi na maumivu hayo yaliwaumiza sana wananchi wa kawaida.Kosa lingine kubwa alilolifanya IDD AMIN ni kuruhusu magaidi wa kipalestina waliokuwa wameiteka ndege ya Air France kutua kwenye uwanja wa ndege wa Entebe kitu kilichokuja kusababisha makomandoo wa Israel kuingia nchini humo na kuwakomboa mateka wao na kisha kuziharibu ndege za kijeshi za Uganda MIG-21 zilizokuwa zimeegeshwa hapio uwanjani hivyo kusababisha hasara kubwa sana kwa nchi.

5.1977 Askofu mkuu Janan Luwum aliuwawa na haikupita muda mrefu aliuwawa tena Mkuu wa Polisi OLYEMA
6.1978 Kosa kubwa kanisa alifanya la kuivamia Tanzania na kutangaza mto kagera ndiyo mpaka halali kosa hilo ndilo lililomuondoa madarakani Tarehe 11-04-1979,Maovu kama hayo niliyoyaeleza hapo juu sidhani kama kunaweza kutokea mtu akaamua kumu-enzi labda awe ndugu yake wa damu siamini kama waliweza kumu-enzi kitaifa mtu aliyefanya madudu mengi namna hii.
 
Bahati mbaya Historia ya Amini inaandikwa kwa kalamu ya Maadui zake na kusomwa katika miwani ya Maadui zake na wasio maadui zake wanajua Historia nyingine kabisa
Hebu tupe wewe historia nzuri ya kumpamba IDD AMIN maana huyo hapambiki kabisa vitendo alivyovifanya vinamfuata nyuma yake wewe utamsafisha vipi???.
 
Hata kama hapambiki ndio ana makosa yake mengi sana lakini ana mazuri yake ambayo hayasemwi.

Angalia hapa kwetu TZ wachina na wahindi mpaka wanatupangia mshahara na kwa ujumla ni manyapara wetu.

HIyo sio hali niyoikuta Uganda na hasa Entebbe na Ji ja na Kampala. Uganda ni nchi ya waganda full stop.

Ingawa ni miaka kidogo imepita toka nikanyage pale lakini uchumi wao unarudi ingawa jeshi linasauti kubwa sana kule kama ilivyo CCM hapa yaani kule wajeda wanajisikia sana, Lakini mchina sio kama huku ameingila mpaka umachi nga.

Yote hii ni mojaya kazi aliyofanya Mwana wa Afrika Iddi Amin Dada Field Marshall, The Conqueror of the British Empire . Hakuuza nchi.

Wala hakujipendekeza kwa mabeberu. Utakuta viongozi wengi wa Afriva wote na wa Russia wakomunisti wote wana wa nanga magharibi aka mabeberu lakini kumbe huko watoto wao wanasoma na wammali kibao.

Angalia Yahya Jahme walimkuta ana bank Accounts 75 nchi za magjaribi huko huko na kila siku alikuwa anatukana mabeberu na kuvaa nguo nyeupe na Qurani kubwa mkononi. Hawa ndio vio gozi wa Africa mnaowapedna ndio waliotufikisha bara hi hapa tulipo
 
Nimebahatika kuishi uganda miaka 5..
Iddi amini hajawahi kuwa adui kwa waganda wenzake.. Ni raisi pekee aliyefanya mabadiriko makuubwa ya kimaendeleo kwa juhudi kubwa kuliko raisi yeyote kipindi kile..

Alitanua barabara na kuzirekebisha vizuur saana.
Aliweka kipaumbele wananchi wake katika suala zima la ajira na maendeleo.
Alichukia unyanyasaji wa wawekezaji toka mataifa makubwa.
Alipunguza kodi zoote zisizokuwa za msingi.


Iddi amini alikuwa na ugomvi na mataifa makubwa na ndio waliopandikiza propaganda hadi tukawa tunaimbishwa nyimbo mashulen ili kumchukia huyu... Na ilikuwa ni kwa nia nzuuri tu ya kutujengea spirit ya kumshinda adui yetu....
 
Idd amin dada mla nyama za watu..
Muua mtoto wake mwenyewe.
Kawamwaga watu mto wa mamba.
Kaua ndugu zetu wa kagera na mabomu yake.

Huyu boya tulitakiwa kumdaka tukamfunga bongo hapa hapa akawa analima na kuchunga ng'ombe.

Muwe mnatumia walau muda wenu kidogo kutafuta ukweli wa mambo badala ya kuziachia akili zenu kulishwa ujinga na kuamini ujinga huo ndiyo ukweli. Haya uliyoandika ni upuuzi mtupu na msomi yeyote hawezi kuandika upuuzi huu.
 
mtwa mkulu,

Mbona wengine huwataji waliodhulumu mali za watu kwa kisingizio cha utaifishaji na kuwaweka watu kizuizini bila ya hatia na wengine kupotezwa, kuminya demokrasia na utawala bora kwa miaka 24 aliyotawala, kuiingiza nchi kwenye umaskini mkubwa kwa sera mbovu za ujamaa na kujitegemea na mengine mengi mabaya. Wewe unaona ya Amin tu?! Acha unafiki.
 
Muwe mnatumia walau muda wenu kidogo kutafuta ukweli wa mambo badala ya kuziachia akili zenu kulishwa ujinga na kuamini ujinga huo ndiyo ukweli. Haya uliyoandika ni upuuzi mtupu na msomi yeyote hawezi kuandika upuuzi huu.
Kasome vitabu.... cheki documentaries...hizo ndo sifa za idd amini
 
Muwe mnatumia walau muda wenu kidogo kutafuta ukweli wa mambo badala ya kuziachia akili zenu kulishwa ujinga na kuamini ujinga huo ndiyo ukweli. Haya uliyoandika ni upuuzi mtupu na msomi yeyote hawezi kuandika upuuzi huu.
Kasome vitabu.... cheki documentaries...hizo ndo sifa za idd amini
 
Back
Top Bottom