#COVID19 Uganda kumuenzi iddi amin je historia ilipindishwa?

Wakimuenzi ni haki yao.Hata jambazi muuaji na katili sana,kama anajali familia yake(au hata asipojali sana), mabaya yakimkuta, lazima hatakosa wapendwa wa kumlilia na hata kusema 'jinsi alivyokuwa mzuri na mwema kwa walio karibu naye'.

Hakuna tatizo na mema yake.Ila mema na mazuri yake,hayakuahalalisha kutenda aliyoyatenda dhidi ya Tz.Akachapwa kisawa sawa kabisa.Pia propaganda kabla,wakati na baada ya vita yaweza kuwa na kamchango na kwenye vita ni jambo la kawaida,ila,ukweli alivamia Tz.

Cha msingi, alifanya kosa kuivamia Tanzania na kuchukua ardhi ya Tz na askari wake kufanya ukatili ndani ya waTz.Hatimae akakipata kilichomstahili na alistahili.

Ni dhahiri hakosi mema aliyofanya nchini mwake, japo hata kwa wachache. Na si ajabu ni kweli kabisa baadhi ya watu walifanya uovu na kuishia kumchafulia yeye kama kiongozi.Mfano kina Malyamungu,Bob Astles,na makamu wake Idris.Lakini,yeye kama kiongozi alipaswa kusimamia anaowaongoza na 'kuashiria' toka awali kuwa,vitendo vya kikatili hawezi kuvikubali wala kuvivumilia.Waliokuwa chini yake,ama wasingetenda kabisa au vingekuwa vichache sana,tena kwa kificho.

Yakitokea mabaya chini ya uongozi wa anayeongoza,kuwajibika (ama kuwajibishwa kwa namna fulani) ni kawaida.

Tunae Rais mstaafu aliyekuwa mwungwana sana na kuamua kuwajibika alipokuwa waziri kwa makosa yaliyotendwa na waliokuwa chini yake.Huu ni mfano tu.
Amin,Idd.jpg

Idi Amin with only a handful of his children
 
Idd Amini Dada! Sijui hili dada lina maana gani? Naomba niongezee kidogo nilichopata kwa mzee mmoja ye alienda vitani uganda,DADA hakuitaka Kagera kama tunavyoaminishwa pia mzee baba (jk mkubwa) kwanini alichelewa sana kutoa amri ya vita inasemekana hadi kawawa akaingilia kati? Dada hakuitaka kagera ila kutokana na wazimu wake aliingia kagera kwa lengo la kushinikiza apewe watu au mtu wake aliekuwa kafichwa na mzee baba Tz,ni kama vile namteka mwanao ili nikurudishie mwanao naomba unirudishie kwanza mwanangu mtukutu uliemficha
 
Hakuna jema alilolifanya kaidada zaidi ya hayo mapicha yaliyotupiwa hapo juu.... Alikuwa kibaraka mkubwa wa mkulima wa kizungu Bob astless na hili liko wazi Sana... Alikuwa kibaraka wa queen Elizabeth na kwa hili histry haidanganyi....
Alimuua yule General mzuri maskini nimesahau tuu jina lake mwanzoni kabla ya mapinduzi.. akaruka kwenye kilichotajwa seng'eng'e kwenye vitabu vya kumbukumbu kiasi Cha kujeruhika mwili wake mbona hili lipibwazi Sana. Kwa ushauri wa Bob na kwaamri yake alimuua Askofu Janan Luwumu maskini asiye na hatia na kusingizia ajali ya gari.. mbona hili sio Siri na Ni yeye na Bob walionekana lastly na marehemu.
Yapo maovu mengi jamaa amefanya na kumbuka dunia haikumuona Kama dikteta hakukuwepo walio kuwa upande wa mwalimu rejea malalamiko aliyoyatoa mwalimu kipindi kile.
Msimponde mwalimu kwa kila issue nyie vijana muwe na utu
Echolima mkongwe Kuna uzi huku
Nimeambatanisha picha ya Askofu Luwumu RIP
250px-Luwum_and_Amin.jpg
images (7).jpeg
 
Idd Amini Dada! Sijui hili dada lina maana gani? Naomba niongezee kidogo nilichopata kwa mzee mmoja ye alienda vitani uganda,DADA hakuitaka Kagera kama tunavyoaminishwa pia mzee baba (jk mkubwa) kwanini alichelewa sana kutoa amri ya vita inasemekana hadi kawawa akaingilia kati? Dada hakuitaka kagera ila kutokana na wazimu wake aliingia kagera kwa lengo la kushinikiza apewe watu au mtu wake aliekuwa kafichwa na mzee baba Tz,ni kama vile namteka mwanao ili nikurudishie mwanao naomba unirudishie kwanza mwanangu mtukutu uliemficha
Ni vyema ukawa mchunguzi wa histry na kuzungumzia ukweli kuliko hisia tetesi na mihemko hasa ukizingatia watu humu ndani Ni wepesi kuaminisha...
Amin alitaka mpaka wake uwe bandari ya Tanga na alitamka hivyo akiikanyaga kanyaga bendera ya CCM pale alikuwa njiani tuu...
 
mkuu kuna chanzo kilichosababisha kuingia kwenye ardhi ya tanzania soma vizuri historia hiyo
Asante kaka.Nikipata taarifa sahihi,sisiti kubadili mtazamo.Kwani,napenda kuzingatia lile ambalo hatimae hujua ndilo kweli,hata kama lipo kinyume na ufahamu wangu wa mda mrefu.Ni kwa kuwa nilisoma vitabu vingi sana vya waandishi mbali mbali kuhusu ile vita na huyu mtu.Ila sisimamii kuwa ndio kweli pekee au ndio ukweli kabisa.Ila ndiko yalinipa picha.
Unaweza kunishauri nisome wapi labda,kwani nitashukuru zaidi kuujua ukweli.Asante kwa ushauri
 
Idd Amini Dada! Sijui hili dada lina maana gani? Naomba niongezee kidogo nilichopata kwa mzee mmoja ye alienda vitani uganda,DADA hakuitaka Kagera kama tunavyoaminishwa pia mzee baba (jk mkubwa) kwanini alichelewa sana kutoa amri ya vita inasemekana hadi kawawa akaingilia kati? Dada hakuitaka kagera ila kutokana na wazimu wake aliingia kagera kwa lengo la kushinikiza apewe watu au mtu wake aliekuwa kafichwa na mzee baba Tz,ni kama vile namteka mwanao ili nikurudishie mwanao naomba unirudishie kwanza mwanangu mtukutu uliemficha
Nadhani jina hasa lilikuwa ni Dadaa.Hili la Dada ni ama kosa la kimaandishi au ile ile ya kumchafua tu.Dadaa ni jina la kikwao na ni jina linalomhusu,kwa kadiri nijuavyo
 
Idd amin dada mla nyama za watu..
Muua mtoto wake mwenyewe.
Kawamwaga watu mto wa mamba.
Kaua ndugu zetu wa kagera na mabomu yake.

Huyu boya tulitakiwa kumdaka tukamfunga bongo hapa hapa akawa analima na kuchunga ng'ombe.
nenda ukamshike yupo bermuda triangle anapunga upepo
 
Hiyo historia ya uwongo

Back
Top Bottom