#COVID19 Uganda kumuenzi iddi amin je historia ilipindishwa?

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,091
8,547
Habari wana jamvi,

Niende kwenye mada hasa nikibase kwenye historia ya Idd Amin aliyekuwa Rais wa Uganda.
Historia inamtafsiri Iddi Amin kama raisi katili kutokea katoka katika nchi ya Uganda ambae alitolewa kwa mapinduzi na majeshi ya Tanzania baada ya kuvamia mkoa wa Kagera na kudai kuwa ni sehemu ya Uganda, na kukimbilia uhamishoni Saudi Arabia hadi pale kifo kilipompata mwaka 2003. Vyombo vya kimataifa vilimtangaza Idd Amin kama Rais katili Africa kiasi cha kutungiwa mpaka filamu zenye kuonyesha ukatili wa kutisha wa Amin mpaka kufikia hatua ya kula nyama za watu.

Leo hii serikali ya Uganda inafanya maadhimisho ya kumkumbuka Rais Idd Amin kama Rais shujaa na mwanamapinduzi ambae na mwanaharakati ambae alipigania wananchi wake katika kupata maendeleo yao.

Shirika la BBC swahili limekutana na watu ambao walikuwa wakifanya kazi na kuishi ndani ya serikali ya Idd Amini na kumsifia kuwa alikuwa ni Rais mwenye huruma na wananchi wake isipokuwa kulikuwa na baadhi ya askari wake waliokuwa wanatumia vibaya madaraka waliyopewa na Idd Amini, hivyo serikali na umoja huo wa watu waliokuwepo kwenye utawala wa Idd Amin wamezindua maadhimisho/maonyesho yakiambatana na makumbusho ambayo itakuwa inatoa historia halisi ya Rais Idd Amin kama Rais shujaa wa nchi ya Uganda

Je historia ya Rais Idd Amin wa Uganda na kisa halisi cha vita ya Kagera vilipindishwa?
20190829_220716.jpeg
 
Idd Amin Dada ni Rais ambaye alipaswa kuenziwa na kupewa ukubwa kuliko hata aliopewa TATA Mandela.
.
Hata Julius Nyerere hamfikii Iddi Amin ni mtu pekee mweusi duniani kupigiwa magoti na wazungu licha ya kaujinga kadogo tu alikokafanya ka kuwavamia kina Nshomile
 
Idd Amin Dada ni Rais ambaye alipaswa kuenziwa na kupewa ukubwa kuliko hata aliopewa TATA Mandela.
.
Hata Julius Nyerere hamfikii iddi Amin ni mtu pekee mweusi duniani kupigiwa magoti na wazungu licha ya kaujinga kadogo tu alikokafanya ka kuwavamia kina Nshomile
kwanini historia yake sasa inapotoshwa?
 
Idd amin dada mla nyama za watu..
Muua mtoto wake mwenyewe.
Kawamwaga watu mto wa mamba.
Kaua ndugu zetu wa kagera na mabomu yake.

Huyu boya tulitakiwa kumdaka tukamfunga bongo hapa hapa akawa analima na kuchunga ng'ombe.
 
Chochote unachofundishwa ni kwa interest za aliyekuandikia amekusudia nini, hiyo unaita Vita ya Kagera huko Uganda ilikuwa positive sana tu.... hata sasa wakazi wengi wa Kagera hujinasibisha na Uganda.
Rejea kwa Adolf Hitler.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom