Uganda imezindua mpango wa kitaifa wa chanjo dhidi ya Corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Waziri wa afya huko Uganda Ruth Aceng anasema wafanyakazi wa huduma za afya watakuwa wa kwanza kupatiwa chanjo wakifuatiwa na waalimu pamoja na makundi ya watu walio kwenye hatari ikiwemo wazee

Uganda imezindua Jumanne mpango wa kitaifa wa chanjo siku mbili baada ya kupokea dozi za ziada laki moja za chanjo ya COVID-19 zilizotolewa na serikali ya India. Kufikia sasa Uganda imepokea dozi 964,000 za chanjo kupitia michango.

Waziri wa afya nchini humo Ruth Aceng, anasema wafanyakazi wa huduma za afya watakuwa wa kwanza kupatiwa chanjo, wakifuatiwa na waalimu pamoja na makundi ya watu walio kwenye hatari, ikiwemo wazee.

Awali waziri huyo wa afya alisema waganda wanaotaka chanjo lazima wawasilishe kitambulisho cha taifa, na wale wasio raia wa Uganda wawasilishe Pasipoti.

Aceng alionya kuwa chanjo haimaanishi umma unapaswa kuachana na kanuni za usalama dhidi ya COVID-19 ili kusaidia kuzuia kuenea kwa virusi hivyo. Uganda imethibitisha maambukizi takribani 40,500 na vifo 334 kwa mujibu wa chuo kikuu cha Johns Hopkins cha nchini Marekani katika kitengo kinachofuatilia masuala ya COVID.

Chanzo: VOA
 
Back
Top Bottom