Uganda Airways kuongeza Senene katika orodha ya vyakula ndani ya ndege baada ya video ya mchuuzi kusambaa mitandaoni

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Baada ya kusambaa kwa video inayomuonesha mchuuzi wa Senene aliyekuwa akiuza bidhaa zake ndani ya Ndege ya Shirika la Ndege la Uganda, Shirika hilo limesema linafikiria kuongeza Senene (Nsenene) katika orodha ya vyakula ndani ya ndege katika safari za kimataifa zinazofanywa na ndege zake.

Awali, video hiyo ilizua hisia tofauti kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, wengi wakijiuliza, mchuuzi huyo aliweza vipi kupenyeza na bidhaa hiyo katika uwanja wa ndege na kufanikiwa kuiza, huku wengine wakimpongeza kwa ‘ujasiri’ wake.



Shirika la Ndege la Uganda limekiri kuwa Wasafiri wa ndege hiyo, aina ya Airbus A330 iliyokuwa ikitoka Uwanja wa Entebbe kwenda Dubai Novemba 26, 2021, walionekana kufurahia bidhaa hiyo, na kuwa wamejifunza kutokana na tukio hilo. Shirika hilo limesema litatumia fursa hiyo kukuza utamaduni wa vyakula vya asili vya Uganda duniani.

“Hatukubaliani na kitendo cha abiria kuuza vyakula ndani ya ndege pamoja na viwango duni vya abiria kuwauzia wasafiri… kwa sababu inashusha hadhi ya Shirika la Ndege la Taifa,” taarifa ya Shirika hilo ilieleza.



Waziri wa Kazi na Usafiri, Jenerali Katumba Wamala aliagiza kufukuzwa kazi kwa wafanyakazi wa Shirika hilo waliokuwa ndani ya ndege wakati mchuuzi huyo alipokuwa akiuza bidhaa yake.

Mchuuzi huyo aliyetambulika kama Paul Mubiru, ameomba radhi kwa kitendo hicho na kusema kuwa alirekodi video hiyo kwa lengo la kuichapisha katika mtandao wa kijamii wa TikTok.

 
Duuh Africa bhana....huku wafanyakazi wanafukuzwa huku wengine wanapongeza

IMG_1805.jpg
 
Back
Top Bottom