Ugali wa kwenye makopo

Enny

JF-Expert Member
May 26, 2009
962
130
Hamjambo wana JF. Nimekumbuka kuna kipindi nilifanya kazi mazingira ambayo ilikuwa vigumu kupata unga na kusonga ugali bali tuliweza kununua vyakula vingi vya makopo kama nyama, samaki, maharage sasa ikawa vyakula hivyo tunakula na mikate. sasa nikafikiria hivi hamna uwezekano wa kutengeneza ugali wa makopo? Na hiyo ikawa biashara nzuri hasa kwa hapa nchini?
 
Hebu uliza kama Waha wanakula UDAGA.

Why not? Kama watu wa siku hizi hasa Dar, hawana muda. Kwanza kufukuzia pesa na mwisho kupoteza muda mwingi kwenye foleni. Unaweza ukaanza na kesho ukakuta Bakhresa anakuja na kukupiga kikumbo.

Law za biashara zitakuambia kama ni biashara nzuri au mbaya. Wao wanasema SUPPLY AND DEMAND. Achana na watu wanaokuja na majibu ya kukatishana tamaa. Mwisho wa siku ni kwamba wewe unauza na wao wananunua. Juzi niliona mashine ya kutengeneza PIZZA. Unalipa na kuchagua Additions zote unazotaka. Unga unachanganywa, nyongeza zinawekwa na pizza inaokwa. Dakika 15 tayari.

Hao hao wanaokucheka leo, kesho ndiyo watakuwa wateja wako. Ila angalia na uwezekano wa mashine inayosonga ugali..........
JUST START.
 
Huko feri ugali unawekwa ndani ya rambo za sh hamsini hamsini then hivyo vilambo vyenye ugali uliosongwa hutumbukizwa ndani ya sufuria yenye maji ya uvuguvugu basi wakati wote ni wa motooo
 
Very interesting idea!

Kuwezekana inawezekana. Moja ya ishu kubwa pengine itakuwa jinsi ya kuuhifadhi huo ugali kwenye kopo ili kupunguza uvaaji koti. Vinginevyo robo ya ugali huo itaishia kwenye koti pekee (ambalo haliwezi kulika).
 
Hamjambo wana JF. Nimekumbuka kuna kipindi nilifanya kazi mazingira ambayo ilikuwa vigumu kupata unga na kusonga ugali bali tuliweza kununua vyakula vingi vya makopo kama nyama, samaki, maharage sasa ikawa vyakula hivyo tunakula na mikate. sasa nikafikiria hivi hamna uwezekano wa kutengeneza ugali wa makopo? Na hiyo ikawa biashara nzuri hasa kwa hapa nchini?

Hiyo biashara lazima itadoda. Thats the way I see it.. :D
 
Hiyo biashara lazima itadoda. Thats the way I see it.. :D
Kwa sehemu ninayofanyia kazi nje ya TZ hamna unga na kila siku piza , burger na chips watu wengi tuliozoea ugali tunahangaika sana. Na mpaka tupo tayari kama tuona mtu ana supply ugali wa kopo tuweze kupasha na kula tu. Hivyo nikafikiria kwa mazingira kama haya lakini siyo kwa mtu ambaye ana nafasi of course
 
Sio ugali wa kopo tu, vile vile kungekuwa na ugali ambao upo frozen unafungwa vizuri kwenye makaratasi ya plastic then mtu akitaka kula ni kuweka tu kwenye microwave kama dk 5 tayari kwa kula.
 
sio ugali wa kopo tu, vile vile kungekuwa na ugali ambao upo frozen unafungwa vizuri kwenye makaratasi ya plastic then mtu akitaka kula ni kuweka tu kwenye microwave kama dk 5 tayari kwa kula.

microwave ni hatari mno kwa afya....
Utapata cancer.....
 
Sio ugali wa kopo tu, vile vile kungekuwa na ugali ambao upo frozen unafungwa vizuri kwenye makaratasi ya plastic then mtu akitaka kula ni kuweka tu kwenye microwave kama dk 5 tayari kwa kula.
Ndiyo hicho ninafikiria Pretty.
 
huo ugali ukauzwe huko huko kwenu ''ulaya,amerika na asia''!sisi tutasonga na kuula ulio fresh
 
Hamjambo wana JF. Nimekumbuka kuna kipindi nilifanya kazi mazingira ambayo ilikuwa vigumu kupata unga na kusonga ugali bali tuliweza kununua vyakula vingi vya makopo kama nyama, samaki, maharage sasa ikawa vyakula hivyo tunakula na mikate. sasa nikafikiria hivi hamna uwezekano wa kutengeneza ugali wa makopo? Na hiyo ikawa biashara nzuri hasa kwa hapa nchini?
why not?
miaka ya nyuma sie tuliokulia mikoani hatukua na unga wa azam,hivyo tulikuwa tunaandaa mahindi wenyewe.unanunua mahindi,unapeleka mashine kukoboa,kisha unayaosha kabla ya kusaga kupata unga.wakati huo ukimwambia mtu kwamba kutakuwa na unga tayari kwa matumizi madukani,atakucheka....
 
huo ugali ukauzwe huko huko kwenu ''ulaya,amerika na asia''!sisi tutasonga na kuula ulio fresh

Fresh? Huo unga wenyewe unafahamu ulikotoka? Inawezekana maji ya kulowekea mahindi walinyeshwea kwanza ng'ombe na yaliyobaki ndiyo wakaloweka mahindi.

Mfuko wenyewe waliotumia kubebea mahindi, jana yake walibebana mzobwe mzobwe na kuutumia kufanya kamchezo ka Wahaya.....

Kama upo Dar wala usiseme wala FRESH. Fresh tunakula sisi huku vijijini maana Mahindi twalima wenyewe, tunakuja hadi kutengeneza unga na kusonga ugali wa kwenye chungu. Na mbona inakuwa Nswalu na Mchwa.
 
Ugali mnaujue nyie?
....mkuu testi zali unaweza kuuza, ila mim sigusi! ugali wa kwenye "hotipoti" tu unanikera! ije kuwa kwenye kopo?!!!!!! huo MKATE
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom