X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,610
- 1,809
Ugali Kwa Mchuzi Wa Nyama, Mchicha, Maharage Na Chatini.
Vipimo Vya Mchuzi Wa Nyama
Nyama ya ngombe vipande vidogo............... 1kg
Nyanya............... 1
Kitunguu Kilichoktwa katwa............... 1
Mafuta............... 2 vijiko vya supu
Paprika (bizari ya masala ya rangi)............... ½ kijiko cha chai
Kidonge cha supu............... 1 (Royco au mchuzi mix)
Chumvi............... Kiasi
Ndimu............... Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Nyama
1 Osha nyama kwa chungio ili itoke maji.
2 Kwenye sufuria, weka mafuta na ukaange vitunguu mpaka viwe rangi ya hudhurungi.
3 Kisha tia nyama na kidonge cha supu uwachie moto mdogo mpaka iwive.
4 Halafu tia nyanya na paprika ufunike sufuria na uiwache motoni mpaka ikauke, kamulia ndimu na itakuwa tayari.
Vipimo Vya Mboga
Mchicha ulio katwa katwa............... 400 gm
Nyanya............... 1
Kitunguu kilicho katwa............... 1
Nazi ya unga............... kiasi
Pilipili mbichi............... 2
Mafuta............... ½ kijiko cha supu
Chumvi............... kiasi
Namna Ya Kutayarisha na Kupika
1 Osha mboga vizuri mpaka iwe haina mchanga.
2 Katika sufuria, kaanga vitungu hadi viwe laini.
3 Tia nyanya, mboga, pilipili na chumvi ikisha toa maji utatia nazi na utaiwacha motoni mpaka ikauke kiasi na itakuwa tayari.
Vipimo Vya Maharage
Maharage............... 1 kopo
Kitunguu 1
Nazi............... 1 Kikombe cha robo lita
Nyanya (itowe maganda)............... 1 kiasi
Pilipili mbichi............... 2
Mafuta............... 1 kijiko cha supu
Chumvi............... kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na kupika
1 Tia mafuta katika sufuria na ukaanga vitungu mpaka vilainike.
2 kisha tia nyanya na pilipili na ukaange kidogo.
3 Tia chumvi, maharage na nazi uwachie moto mdogo mpaka iwe nzito kiasi na itakuwa tayari.
Vipimo Vya chatini Ya Pilipili mbichi
Pilipili mbichi............... 5
Kotmiri (coriander)............... 1 Kijiko cha supu
Ndimu............... kiasi
Thomu............... 1 chembe
Mafuta ya zaituni............... 2 vijiko Vya supu
Chumvi............... kiasi
Namna Ya Kutayarisha
1 Kwenye blender, tia vipimo vyote na usage isipokuwa chumvi tia mwisho kwa juu kwenye bakuli na itakuwa tayari kwa kuliwa.
Vipimo Vya ugali
Maji............... 4 Vikombe kiasi inategemea na unga
Unga wa sembe............... 2 vikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Tia maji kiasi katika sufuria, weka motoni, yakipata moto korogea unga wa sembe kiasi na ufanye uji mzito uache uchemke vizuri huku ukikoroga.
Chota kibakuli kimoja cha uji huo weka pembeni kisha mimina unga wote uliobaki upigepige uchanganyike vizuri kwenye uji huo mpaka ushikamane.
Punguza moto anza kuusonga taratibu huku ukiongeza ule uji ulioweka pembeni kidogo kidogo mpaka uone sasa umeshikamana vizuri na hauna mabuja.
Endelea kusonga mpaka ulainike kisha mimina kwenye bakuli au sahani na itakuwa tayari kwa kuliwa na mchuzi wa nyama, maharage, mboga na chatini.