Ugaidi: Ufafanuzi wa kisheria na hatari iliyopo juu ya mashtaka ya ugaidi dhidi ya Freeman Mbowe na wengine (3)

Emekha Ikhe

Member
Jul 14, 2021
43
62
UGAIDI: UFAFANUZI WA KISHERIA NA HATARI ILIYOPO JUU YA MASHTAKA YA UGAIDI DHIDI YA MH. FREEMAN MBOWE NA WENGINE (3).

Na. Alphonce Lusako (Human Rights-Lawyer)

Andiko Hili litajikita Katika Mambo Makuu yafuatayo
  • UTANGULIZI- KESI YA UGAIDI (ECONOMIC CRIME NO. 63 OF 2020).​
  • NINI KINAUNDA KOSA LA UGAIDI (TERRORISM ACT).​
  • UFAFANUZI NA KASORO ZA HATI YA MASHTAKA YA UGAIDI DHIDI YA WATUHUMIWA.​
  • HATARI ITAYOMKUMBA MH.FREEMAN MBOWE NA WENGINE (3), CHADEMA NA TAIFA KAMA DHAMIRA YA WALIOMSHTAKI ITATIMIA.​
  • UTANGULIZI –KESI YA UGAIDI (ECONOMIC CRIME NO. 63 OF 2020)
Andiko hii, limejaribu kufafanua tuhuma hizi alizounganishwa nazo Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani, (CHADEMA), Mh. Freeman Elkael Mbowe kwa Lugha rahisi ya Kisheria ili hata mtu wa kawaida apate kujua undani wa Mashtaka husika, Hatari na Madhara ambayo yatamkumba Mh. Freeman Mbowe (Binafsi), CHADEMA na Taifa, Vile Vile, Madhara katika Utulivu wa Taifa tulionao ambao kwa kweli Utulivu huu Unalindwa na Mitutu ya Bunduki.

Mh. Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani (CHADEMA), Katika Waraka wake wa hivi Karibuni aliandika kuhusu Mashtaka ya Kuchongwa dhidi yake ili Kumuogopesha kufanya harakati za Kudai Katiba ya Wananchi na Kuwaogopesha Wananchi na Wadau wa Katiba katika Kudai Katiba Mpya. Alisisitiza yeye binafsi haogopi Kufungwa na kuwashawishi Watanzania Kuendeleza Mapambano ya Kupigania Katiba Mpya hata kama yeye atafungwa Miaka Mingi Gerezani, alisisitiza Kwamba Yupo Tayari Kukikabili Kifo akiwa Gerezani au Kifungo katika Gereza kama dhamira ya Waliochonga Mashtaka husika itapewa Baraka na Mahakama Kuliko kuacha harakati za Kudai Katiba Mpya.

Kutokana na namna alivyokamatwa Usiku wa Manane na Vyombo Vya Dola akiwa Mwanza akijiandaa na Kongamano la Katiba lililoandaliwa na BARAZA LA VIJANA LA CHADEMA (BAVICHA). Napenda kutoa ufafanuzi wa Kina juu ya haya Mashtaka ambayo kwa kinywa chake alikili ni Mashtaka ya Kuchongwa lakini pili napenda kutoa ufafanuzi wa Hatari itayo Mkumba Mh. Freeman Mbowe yeye binafsi, CHADEMA, na Taifa kwa Ujumbla wake Kama Mashtaka husika yatafanikiwa Kumtia hatiani.​
  • NINI KINAUNDA KOSA LA UGAIDI
  • Nia Ovu ya Kutenda Ugaidi (Terrorist Intention)
  • Kitendo cha Ugaidi (Terrorist act).
Kwa Mujibu wa Sheria ya Kuzuia Ugaidi, imefafanua kwa kina juu ya Kosa la Ugaidi, Kwa kifupi, Kifungu cha 3, na Kifungu cha 4 kifungu kidogo cha (1), (2) na cha (3) Cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi, Sura ya 21 ya Mwaka 2002 kimeeleza vitu viwili ambavyo Vinaunda kosa la Ugaidi.

Kitu cha Kwanza ni Dhamira au Nia Ovu ya Kutenda Ugaidi (Terrorist Intention) kitu cha Pili Kitendo cha Ugaidi (Terrorist act). Hivyo ili Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) aruhusu shauri lolote la Jinai dhidi ya Mtuhumiwa wa Kosa la jinai Kama Mh.Freeman Mbowe na Wenzake, anapaswa kujiridhisha juu ya mambo makuu mawili kama yametendeka (Dhamira/Nia Ovu ya Kutenda Ugaidi na Kitendo cha Ugaidi) ambacho kimelenga Kutisha watu, Kumdhuru Mtu, Kuhatarisha maisha ya Mtu/Watu, Kuishurutisha Serikali Kutenda jambo fulani, Kuharibu mali ya mtu au ya umma kwa kutumia milipuko na vile vile Kuvunja amani na Utulivu wa Nchi, nk...

Ukisoma Hati ya Mashtaka ambayo Mh. Freeman Mbowe ameunganishwa, Inaelezea tu Tuhuma za Uwezeshaji wa Mh. Freeman Mbowe ambao sio wa moja kwa moja (Inderectly) kwa Halfa Hassan na wengine Wawili (2) waliotuhumiwa kufanya Ugaidi wa Kulipua Vituo Vya Mafuta ambavyo havifahamiki kwa Kuwa hakuna hata kituo Kimoja Kilichotajwa katika Hati ya Mashtaka. Mwendesha Mashtaka (DPP) alipaswa kujiridhisha na mambo haya Makuu Mawili (Terrorist act &Terrorist Intention) kama yote yameonekana ili kuunda kosa la Ugaidi kama takwa la Sheria linavyohitaji.

Katika Uandishi wa Hati ya Mashtaka yoyote ambayo Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) anapaswa kujiridhisha kikamilifu ni sehemu ya Kiini cha Hati ya Mashtaka (Body of the Charge Sheet). Hii ni sehemu ya kiufundi (Techical Party) inayohusisha, Mosi, Maelezo ya Kosa (Statement of Offence) na pili, Ufafanuzu wa Maelezo ya Kosa (Particulars of Offence) ambayo Kwa Kweli yanapaswa kuwa na Sifa zilizoainishwa katika Kifungu cha 135 (f) Cha Sheria ya Mienendo ya Makosa ya jinai, Sura Na 20 iliyorejewa Mwaka 2019 kama itavyofafanuliwa hapo chini.

UFAFANUZI NA KASORO ZA HATI YA MASHTAKA YA UGAIDI DHIDI YA MH.MBOWE NA WENGINE (3)

Nimeona nijadili kwa lugha rahisi na Kwa maoni yangu kuhusu Hati ya Mashtaka iliyoandikwa kwa Ufundi wa Sheria ili msomaji (Ambaye Si Mwanasheria) apate picha kamili ya hili sakata Linalomkumba Mh. Freeman Mbowe. Baada ya Kusoma Hati ya Mashtaka kuna madhaifu kadhaa ambayo yanapaswa kupingwa na Mawakili Wataosimama Kumtetea Mh.Freeman Mbowe Mahakamani Kwani Hati Husika imekosa sifa ya Kuwa Hati ya Mashtaka Kwa Jicho la Kisheria (Defective Charge sheet).

Msingi wa Mapingamizi haya ni Kutokana na takwa la Kifungu cha 135(f) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura Na. 20 iliyorejewa Mwaka 2019. Kwakuwa “Kuthibitisha pasi na Shaka-Prove beyond reasonable dought” ni moja ya Kanuni kuu katika Mashtaka ya Makosa/kosa la Jinai dhidi ya Mtuhumiwa yeyote. Msomaji wa Hati ya Mashtaka ambaye anaufahamu na uelewa kidogo kuhusu uundwaji wa Hati ya Mashtaka katika Kesi za Jinai ataikosoa Hati ya Mashtaka kwa kuwa inakosa sifa ya kuwa Hati ya Mashtaka katika Jicho la Kisheria (Defective Charge sheet)

Ni takwa la Kifungu cha 135 (f) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, sura Na.20 kwamba, Hati ya Mashtaka dhidi ya Mtenda/Watenda inapaswa kuonyesha Mtenda/Watenda wa Kosa lililotendeka (Who), Kosa lililotendeka (What), Muda wa kosa lilipotendeka (When/Time) na Mahala kosa lilipotendeka (Where/Place).

Tuhuma dhidi ya Mh.Freeman Mbowe na Wenzake zimekuwa tuhuma tata ambazo kwakweli ni za Kuhisia na Jumuishi. Tuhuma husika zinamtuhumu Mh. Freeman Mbowe Kwa nyakati tofauti kati ya tar. 01 May 2020 na tar. 1 August 2020 Kufanya njama (Conspiracy) ya Kutenda kosa la Ugaidi kwa kumtuhumu Mh. Freeman Mbowe kutoa fedha (Inderectly-Bila kuhusika Moja kwa Moja) kwenda kwa Halfan Bwire Hassan na wengine wawili(2) ambao walikamatwa kwa tuhuma za Kufanya njama za Ugaidi Mwaka 2020. Hati ya Mashtaka inafafanua kwamba Uwezeshaji wa Mh. Freeman Mbowe kwa hao wanaodhaniwa kwamba ni Watuhumia wa Ugaidi haukuwa wa moja kwa moja kutoka kwa Mh. Freema Mbowe na ulikuwa unalengo la kulipua Vituo vya Mafuta (Petrol Station) ambavyo havifahamiki kwani havijatajwa katika Hati ya Mashtaka.

Aidha, Hati ya Mashtaka inatamka kwamba, Njama husika zilifanywa katika Hoteli ya AISHI iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro na Maeneo Mengine ndani ya Dar es Salaam (Hayafahamiki), Morogoro (Maeneo Hayafahamiki) na Arusha (Maeneo Hayafahamiki) lakini haitaji Kitendo hicho cha Ugaidi kilitarajiwa kufanyika katika Vituo Vya Mafuta vipi ndani ya Maeneo tajwa hapo juu. Ukichambua Hati hii ya Mashtaka unagundua kwamba, Hizi ni tuhuma hewa kwa kuwa hata katika Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Arusha, Hati ya Mashtaka haija-ainisha mahala gani ndani ya mikoa husika ambapo vikao vya kula njama (Conspiracy) vilifanyika.

Aidha, Hati ya Mashtaka katika Sehemu ya Ufafanuzi wa Maelezo ya Kosa (Particulars of Offence) haijachambua na kuonyesha kosa lilitendeka wapi na nani alidhurika na kosa husika, Mali gani ziliharibiwa, Amani ipi iliharibika kutokana na hicho wanachotuhumu kwamba ni kitendo cha Ugaidi,

Kwa Ujumla, Hati ya Mashtaka inakosa sifa ya Kuwa Hati ya Mashtaka kwa kuwa inakiuka Matakwa ya Kifungu cha 135(f) cha Sheria ya Muenendo wa Makosa ya Jinai Sura Na. 20 iliyorejewa Mwaka 2019.

HATARI ITAYOMKUMBA MH. FREEMAN MBOWE NA WENGINE (3) KAMA DHAMIRA YA WALIOMSHTAKI ITATIMIA.

KIFUNGO GEREZANI KATI YA MIAKA 20-30

Kwa mujibu wa Kifungu cha 60(2) na Kifungu cha 60 (7) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura Na.200 iliyorejewa Mwaka 2019, Mh.Freeman Mbowe na Wenzake akitiwa hatiani na Mahakama, atatakiwa Kufungwa Miaka zaidi ya 20 lakini chini ya Miaka Thelasini (30), kwa kifupi (Kati ya Miaka 20 na 30). Msisitizo zaidi umekaziwa katika Kifungu cha 60 (7) Cha Sheria husika Kwamba, Kama Mahakama itathibitisha Kosa Husika kwamba, Kosa Alilolifanya Mh. Freeman Mbowe limeharibu Uchumi wa Taifa au Mali za Umma atatakiwa afungwe kifungo kikubwa zaidi ambacho kwa tafsiri ni Miaka 30.

MADHARA KWA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

Kutiwa hatiani kwa Mh. Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani (CHADEMA) kitahalalisha zile tuhuma ambazo mara zote baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi na serikali yake, wamekuwa wakituhumu kwamba CHADEMA ni Chama Cha Kigaidi hivyo hukumu itathibitisha kwamba chama hiki kimejishughulisha na Masuala ya Kigaidi hivyo kimefanya shughuli ambazo zipo Kinyume na Sheria za nchi na kuamriwa Kufutwa katika Uso wa Dunia ya Tanzania. Ikumbukwe Jaribio la kukituhumu chama hiki kwa makosa ya Ugaidi haijaanza leo, Nadhani Mtakumbuka huko nyuma Ndugu Lwakatare alivyosota Jela Kwa miezi kadhaa kwa tuhuma hizi hizi za Ugaidi.

Kwa kuwa Wanachama wa CHADEMA na Watanzania wengi wakiwemo wana-CCM bado wapo Gizani na hawaamini kama ambavyo hawajaamini Mh. Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzai chenye Wanachama zaidi ya Million 7 (7000,000,+) Kushitakiwa kwa Kosa la Ugaidi, Na kwa Kuwa Kikundi cha Watu wanaotaka kutekeleza adhima ya Kuhakikisha Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe na Wenzake hawajui madhara yake kwa taifa na kwa kweli hawajui gharama ya kuja kutuliza umma wakati watu wakidai haki. Kitendawili hiki tukipe muda maana kitateguliwa na muda wenyewe japo ni hatari sana kwa Utulivu wa Taifa letu.

MADHARA: NYUFA ZA ITIKADI ZA VYAMA VYA SIASA

Kwa Muda mrefu sasa, Wenye Macho wameshuhudia kwamba Chama Kimoja (CCM) ndicho chama chenye haki ya Kufanya Shughuli za Kisiasa dhidi ya Vyama Vingine, Kwa Muda sasa watu wa Upinzani wao wamekuwa wakishurutishwa, Wakilia, Wakishitakiwa na Makosa ya Kuchonga, Wakifungwa, Wakitekwa, Wakiuwawa na Wengine kulazimishwa Kuunga Juhudi kwa nguvu kwa muda wote. Vyama Vya Upinzani silaha yao Imekuwa ni Majukwaa ya Siasa na Kusemelea Kuonewa kwa kwa wananchi. Wakati huu hata hizo nafasi za kutema nyongo katika Majukwaa zimezibwa kwa Mtutu wa Bunduki(Ni hatari inatengenezwa bila kujua kinachopandwa-Tuogope kesho).

Ni ngumu kutabili lini Uvumilivu huu utashindwa kuvumilika ila huko ndiko tuelekeako. Mnaodhani Mnapanda Mbegu ya Kujilinda ninyi na Maslahi yenu ya baadae hamjui Mlitendalo. Hakuna atakayekuwa salama kama Diplomasia hazitachukua nafasi yake kwa udharura wake ili kulirudisha taifa hili katika Muafaka wa Pamoja haswa Kupitia Katiba Mpya #KatibaYaWananchi

MWISHO: AMANI NA UTULIVU WA NCHI NI TUNDA LA HAKI

Chonde Chonde kwa Intelejensia ya Nchi yetu, Viongozi wa Dini ambao kwa kweli ninyi ndio mnakibali cha kusikilizwa na Mamlaka za Nchi, Kwa nafasi mliyonayo kabla Umma hujafikia hatua ya kuyatumia mamlaka yao kama yalivyowekwa katika Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tafadhari Shauruni Mamlaka zijitafakari upya katika kuhakikisha Taifa linaziba Nyufa kubwa hizi (1. Mpasuko wa Kubaguana Kiitikadi, 2, Kukua Kwa Tabaka la Wenyenacho na Wasionacho) ambazo kwa sasa zimeshamea kwa kiwango tulichonacho. Ni Muhimu Kuziba ufa katika wakati wa sasa kuliko kuja Kujenga Ukuta.

Mawasiliano:

Alphonce Lusako M (Human Rights-Lawyer)

alusako@gmail.com

Makala nzuri sana.

Aluta continua
 
Amendment of charge?????Section Section 234(1) CPA charge inaweza kufanyiwa marekebisho muda wowote kabla ya kufunga ushahidi pande zote. Sasa si watabadilisha? Mnwapa mwanga wa kufanya marekebisho kwa uongo wao!
 
Nachukia sana serikali zenye elements za ki communist. Sina tu la kufanya
 
Andiko refuu lakini ni utopolo tupu halafu unajiita Lawyer!! Nilitegemea uandike facts za kisheria tupu lakini umejaza na utopolo wa kisiasa ndani yake!! Hongera!
 
Mkuu,umewavua nguo kabisa CCM na Serikali yao,sasa imebaki huyu mama tumvue kufuri,maana anatuletea mipasho tu,
 
Andiko refuu lakini ni utopolo tupu halafu unajiita Lawyer!! Nilitegemea uandike facts za kisheria tupu lakini umejaza na utopolo wa kisiasa ndani yake!! Hongera!
hivi kumbe inaruhusiwa kujadili shauri la jinai lililopo mahakamani,niliwahi kusikia zamani ilikuwa hairusiwi kujadili (public) shauri lililopo mahakamani kumbe itakuwa ni mabush lawyer wamenidanganya!
 
Vipi sheria inasemaje kuhusu MDUDE aliyesema atamnyoa mama yetu kipenzi kama alivyomnyoa JPM,
Ni ugaidi au sio ugaidi? Kama vipi na yeye aungane na wenziwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkenya yuko wapi kenge wewe ?! Au tuwaite humu akina MK254 waitetee Kenya yao ?!

Hehehe!! Wachana na huyo magu2016 mbaguzi anafikiria kila jina lisilo la Kisukuma sio la Kitanzania, anakosa kuelewa wazungu walipochora mipaka na kubuni Tanzania, kuna baadhi ya makabila yaligawanyishwa kati, wengine wakabaki kwetu huku na wengine huko.
Aisei hilo jina Odhiambo itakua hukupa tabu sana kutoka kwa viumbe wabaguzi kama huyu jamaa, ambaye hajasoma historia na kufahamu hata hao Wasukuma asili yao kule misitu ya Congo.
 
Umenena vizuri mkuu ila huyu Odhiambo namfahamu vizuri sana wakati niko Kenya Westland alikuwa mlinzi kwenye ofisi zetu.
 
Back
Top Bottom