Ufuta unawafanya watu wawe na viburi mjini hapa

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
4,978
2,000
Habari za asubuhi mabibi na Mabwana,

Naendelea na uchunguzi sehemu mbali mbali unaweza ukafanya nini kwenye vijiji vyetu vilivyobarikiwa na Mungu wakati sisi vijana woote tunataka tuishi mjini huku tukiendesha mikoko mikali

Ni hivi

Huku bwana ni wakati wa mavuno, aseee watu wanapiga pesaa balaaa, hiki kijiji masemi hayakauki si kubeba mpunga (gunia limepanda hadi 50,000), mahindi nayo yanabebwa si utani, yaani Wasukuma wana pesa chafu sahivi, ikifika jioni ni ngomaa tu mpaka asubuji wanaenda kunywa supu.

Ufuta, ufuta ufuta hapa ndio funga kazi, mazee unafatwa shambani kwako au store kwako wazee wanataka ufuta, kuna mazee mmoja yeye anauza 260k kwa gunia, ila wazee wamefika 255k amegoma na hataki maelezo, mzee anagunia zake 40 za 80kg kila moja.

Jamaa mmoja amejenga ghala la kuhifadhi ufuta asee, hakuna ujinga kama Bachelor degree kwa kweli, ndani ya wiki moja tu pesa anayotengeneza anajua Mungu tu

Ghala halikai na mzigo, ni lulu jamani zao hili.

Nawasilisha tu kwa wakuu humu, mwenye masikio na asikie.
 
myplusbee

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
3,643
2,000
Semeni ukweli, hasara ipo. Ufuta hautaki mvua kwa mfano ukishakauka. Umepanga kwenda kuvuna kesho leo mvua imenyesha unakuwa mweusi....una faida?
Na probability ya kunyesha mvua msimu wa mavuno ni asilimia ngapi japo kwa makisio?!
 
Tattoo

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
2,816
2,000
Mambo mengine ni ya kujiongeza tu kwa sababu hakuna biashara hata moja duniani isiyo na changamoto!
Nyanya, vitunguu, ufugaji hasa wa kuku, matikiti....sasa mmehamia ufuta. Waambieni waje tu kwa fujo with heada full of expectations.

Mi nalima ufuta mwaka wa 4 huu najua michezo yote na najua hasara pia. Kwahiyo mtu hanitishi kwa lolote.
 
msukuma fekero

JF-Expert Member
Aug 12, 2017
1,040
2,000
Nyanya, vitunguu, ufugaji hasa wa kuku, matikiti....sasa mmehamia ufuta. Waambieni waje tu kwa fujo with heada full of expectations.

Mi nalima ufuta mwaka wa 4 huu najua michezo yote na najua hasara pia. Kwahiyo mtu hanitishi kwa lolote.
Mwambie kama anapata faida kubwa hivyo wanunue trekta waongezee mashamba full stop
 
Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
4,978
2,000
Nyanya, vitunguu, ufugaji hasa wa kuku, matikiti....sasa mmehamia ufuta. Waambieni waje tu kwa fujo with heada full of expectations.

Mi nalima ufuta mwaka wa 4 huu najua michezo yote na najua hasara pia. Kwahiyo mtu hanitishi kwa lolote.
Brother upo siriaz wewe?? Unamtishia nani kwa kulima ufuta mwaka wa 4?? Eti unavuna kesho mvua inanyesha leo?? Hivi hiyo ndio sababu yako kubwa???

Nilipo hapa watu wanajaza ghala na ghala na wanatafuta ufuta kwa hali na mali unadangabya watu

Wewe ndio unalima kwa hasara

Hapa ndio zao laoo kuu pamoja na mahindi na mpunga
 
myplusbee

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
3,643
2,000
Nyanya, vitunguu, ufugaji hasa wa kuku, matikiti....sasa mmehamia ufuta. Waambieni waje tu kwa fujo with heada full of expectations.

Mi nalima ufuta mwaka wa 4 huu najua michezo yote na najua hasara pia. Kwahiyo mtu hanitishi kwa lolote.
Yote hayo yanatoka wapi Mheshimiwa?! Mleta mada kazungumza anachokijua! Na kila mmoja anazungumza anachokijua! Na binafsi yangu hakuna popote niliposema nalima ufuta au kuwahamasisha watu wakalime ufuta! Mimi nimezungumzia uzoefu wa ndugu zangu ambao wamejikita kwenye hilo zao! Na unlike mikoa mingine, mikoa niliyotaja mimi ni ile ambayo ufuta ni kama zao lao la asili! Hata wakati ufuta hauna pesa, watu walikuwa wanalima; kwa sababu wamekuta babu zao wanalima hata kabla Nyerere hajaipatia Tanganyika uhuru!!

That being said, watu niliowazungumzia mimi huwezi kuwatisha eti sijui mvua, mara upupu kwa sababu ufuta ni zao la asili! Na ndio maana nikakuuliza hata probability ya mvua msimu wa mavuno kwa sababu, kwa kawaida yale maeneo ya asili kwa kilimo cha ufuta, majira ya mavuno yanakuwa hayana mvua!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom