Ufupisho wa kitabu cha the school money by olumi

friendfx

JF-Expert Member
Oct 16, 2017
246
250
Hatua ya 15; Kitabu - The School of Money by Olumide Emmanuel

Ukurasa wa 14; ( ACTIVATING MULTIPLE STREAMS OF INCOME ) 219~ 228

Amsha Mifereji mingi ya Vipato

Maziwa na Bahari haikaushi maji yake sababu ya kuendelea kupokea maji toka vyanzo mbalimbali kama mito inayoendelea kutiririsha maji katika maziwa na bahari. Na hii ndivyo pia kwa maisha ya watu walio na utajiri kutokuwa na chanzo kimoja tu cha mapato yao. Hata kama ni biashara lakini ni biashara yenye vyanzo tofauti vya mapato.

Kila mtu mwenye ndoto yakutaka utajiri lazima afikirie kuwa na vyanzo vingi vya mapato. Kama ilivyo siri ya bahari kutokauka sababu ya vyanzo vya maji toka sehemu mbalimbali ndivyo maisha ya utajiri yanataka Kuwa na VYANZO VINGI VYA MAPATO.

Kuna aina 3 ya viwango vya Mifereji au Vyanzo vya Mapato ( 3 Dimensions of Streams in Wealth Creation )

1. Kipato Kimoja kwa Wakati ( One time stream )

Hivi ni aina ya vyanzo vya mapato ambavyo mtu hupata fedha Mara moja pindi tu afanyapo kazi, hivyo inampa aendelee kufanya kazi ili alipwe. Mfano mikataba na mishahara ni makundi ya watu wanaopata aina hii ya chanzo cha mapato. Angalia wewe upo wapi ?

2. Kipato kimoja kwa wakati na Mara nyingi ( Once and always )

Ni aina ya mfereji wa kipato unayofanya kazi Mara moja tu na baada ya hapo huhitaji tena kufanya kazi , hivyo kinachofuata ni kuendelea kulipwa. Mfano Uandishi wa vitabu, CDs, Kupangisha nyumba, Biashara ya magari nk.

3. Kipo Muda wote ( Free flow )

Hiki ni chanzo cha mapato ambacho fedha inakufanyia kazi mfano Hisa.

Kwanini uwe na Mifereji mingi ya Vipato ?

1. Ni jambo la Busara na Hekima

2. Inakuza uwezo wako wa kupata fedha

3. Inapunguza hatari ya kipato kimoja kufa

4. Inakupa Usalama zaidi

5. Ni siri ya Utajiri usoisha

Mapato ya nchi yanapatikana katika maeneo yafuatayo kwa uchachewe;

1. Kodi
2. Ushuru na forodha
3. Thamani ya Vipande na Hisa
4. Utalii
5. Miundo mbinu
6. Mashirika ya kifedha
7. Madini
8. Mikopo
9. Orodha ni ndefu inaendelea

Mikakati ya Utajiri kutengenezwa kutoka na Mifereji ya kifedha

1. Jua Mfereji wako wa sasa na unaotumika sana

2. Tumia Ufahamu wa Kifedha na Fikra za Kiwekezaji kuendeleza Vyanzo vingine vya Mapato

3. Imarisha kila mfereji na kuza

Mifereji ya Vipato mikondo na Milango yake ( MULTIPLE INCOME CHANNELS AND DOORWAYS )

Katika kuwekeza kuna mikondo 15 unayoweza kuanza nayo kufikiria njia ya kuwekeza kwa tumia milango 7 ambayo utatumia kuweza kufikia mikondo hii 15 ambayo inakupa nafasi ya kuwa Vyanzo vya njia ya kujipatia Mapato.

Mikondo 15 ya kiuwekezaji katika sekta kuzifanyia tafiti ni kazi yako

1. Chakula
2. Mavazi
3. Malazi
4. Mawasiliano
5. Usafiri
6. Elimu
7. Fedha
8. Habari na teknolojia
9. Usalama na Ulinzi
10. Dini na Maadili
11. Hakimiliki za kazi za kitaaluma
12. Viwanda na uzalishaji
13. Nishati na Madini
14. Burudani
15. Michezo

Milango 7 yakuweza kuingia kwa hii mikondo 15 ni Kama ifuatavyo;

1. Uwe na Malighafi
2. Kuchakata
3. Kupaki ( packaging )
4. Usambazaji na Usafirishaji
5. Matangazo
6. Mauzo na Masoko
7. Taratibu na utawala

Tulia na kisha tafakari kwa kina kuona namna gani haya Mwandishi Olumide Emmanuel ka kushirikisha ili uyatumie na kisha upige hatua kubwa siku hadi siku. Nakutakia ufanikiwe Katika hatua zako
 
Niongezee tu kuwa kabla hujafungua mifereji mingi utambue kuwa mifereji ya pesa lazima ijengwe vizuri na kuimarika vizuri ili kutiririsha pesa kwa ufanisi zaidi.

Mifereji ina kawaida ya kuziba baada ya mda fulani kutokana na uchafu kujaa humo na kuwa kikwazo cha pesa kutokutiririka vizuri, hivyo basi tenga muda wa kufanyia ukarabati mfereji wako.
 
Niongezee tu kuwa kabla hujafungua mifereji mingi utambue kuwa mifereji ya pesa lazima ijengwe vizuri na kuimarika vizuri ili kutiririsha pesa kwa ufanisi zaidi.

Mifereji ina kawaida ya kuziba baada ya mda fulani kutokana na uchafu kujaa humo na kuwa kikwazo cha pesa kutokutiririka vizuri, hivyo basi tenga muda wa kufanyia ukarabati mfereji wako.


Ni muhimu sana kuwa na maarifa sahihi kabla ya kufungua biashara sahihi
Wengi ukimbilia kuanza biashara bila tena kwa fedha za kukopa benki
 
Back
Top Bottom