Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,606
- 696,720
Je ni kweli kutakuwa na mwisho wa dunia?
Je utimilifu wa dahari ni upi? Ninini?
Je kuna kikomo cha wakati...
Kitabu cha ufunuo kina mambo mengi ambayo bado wengi hatujaweza kuyang'amua... Ni magumu na yako complicated sana
Kwa mujibu wa kitabu hicho mwisho wa dunia upo na utakuwa mbaya kwa baadhi yetu... Kuna habari za kutiwa muhuri nk
Kuna kitu kinaitwa utimilifu wa dahari...! Je ni upi huo? Kwamba kutakuwa hakuna mwendelezo wa chochote tena! Kila kitu kitakomea hapo.. Chochote ulichokuwa unafanya utasimama hapohapo na ndio kutakuwa na kikomo cha nyakati...
Kuna mkanganyiko mkubwa kuhusu nyakati zinazozungumziwa kwenye maandiko na nyakati tunazomaanisha sisi... Lakini hili tulipe muda na kuangalia milango michache ya kitabu cha ufunuo inasemaje... Kikubwa hapa ni hii namba SABA... Kuna siri kubwa sana hapa
Ufunuo wa siku za mwisho unaandikiwa kwenda makanisa SABA yaliyoko Asia.... Mbele ya roho SABA zinazozunguka kiti cha enzi..
Makanisa hayo SABA ni
Efeso
Smirna
Pergamo
Thiakira
Sard
Filadelfia
Laodikia
Hapo kuna vinara SABA vya taa za dhahabu na kuna mtu mwenye nyota SABA mkono wake wa kuume... Siri ya nyota hizo SABA na vinara SABA vya dhahabu ni hii hapa..
Nyota SABA ni malaika wa yale makanisa SABA na vinara SABA ni yale makanisa SABA.... Lakini pia huko kuna vitu 24 vinavyokizunguka kiti cha enzi chenye taa SABA zikiwaka ambazo ndio roho SABA za Mungu
Pembezoni mwake kuna wazee wanne wamejaa macho mbele na nyuma.. Wazee hao ni
. Mwenye uhai wa kwanza mfano wa Simba
. Mwenye uhai wa pili mfano wa nyama
. Mwenye uhai wa tatu mfano wa mwanadamu
. Mwenye uhai wa NNE mfano wa tai arukaye.
Katikati ya kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne kuna mwanakondoo ana pembe SABA, macho SABA ambazo ni roho saba za Mungu...
Kuna mada tulijadili kuhusu Mbingu SABA na nguvu ya namba SABA... Na hata kwenye uumbaji tumeona ulimwengu uliumbwa kwa siku sita na siku ya SABA akapumzika!
Hapo juu nilijaribu kuchukua mistari yote kuanzia mlango wa kwanza hadi wa tano inayozungumzia namba SABA
Hii inatoa tafsiri gani? Ni kwamba namba SABA ndio namba ya ukamilifu na utimilifu na ndio iliyobeba siri ya uumbaji na mwisho wa utimilifu wa dahari....
Tumeona pia kumbe Mungu ana roho SABA kwahiyo kila alichokiumba kwa siku yake kilibeba roho moja.... Tutakuja kuona huko mbele jinsi makanisa SABA yanavyopewa maagizo na mapigo saba yatakayoiteketeza dunia... Lakini lile pigo la SABA likiitwa kama SIRI KUU
Kwahiyo basi kuna uwezekano mkubwa kabisa dunia itaishi kwa nyakati SABA na utakapotimia wakati wa SABA ndio utakuwa kikomo /kiama?
Nimeona nianze na hili la namba hii SABA kisha tutaendelea na uchambuzi wa kitabu hiki cha ufunuo katika mada zijazo....!
Making six years of being JF member!
Sent using Jamii Forums mobile app