Ufunuo wa Mchungaji! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufunuo wa Mchungaji!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Oct 22, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kila mara naisikia sauti ya Nyani Ngabu Julius ikisema Miafrika Ndivyo Tulivyo. Kisha kwa mbali Bob Mkandara hunguruma watu na mazingira. Kisha FMES humalizia kwa kusema viongozi wetu ni image yetu wenyewe.

  Kwa wiki tatu, kauli hizo nimezithibitisha tena kuwa ni sahihi na kwa masikitiko makubwa nikakubali kuwa ndio hali halisi.

  1. Kwanza, Watanzania wengi sana ni Mafisadi kwa namna yao.
  2. Pili, Watanzania wengi sana wameridhika na dhiki, kero, shida na umasikini na wanaita ni hali halisi!
  3. Tatu, Watanzania wengi wamenogewa na kutegemea misaada na kupewa.
  4. Nne, Rushwa na Takrima si uhalifu tena, bali ni haki na halali ili mtu apate haki yake au atimiliziwwe mahitaji.
  5. Tano, Sheria, Kanuni na Taratibu zipo, tena nyingi sana, lakini kila mtu anajifanyia analotaka bila kujali matokeo ya yeye kukiuka Sheria au kanuni na wale walio na majukumu na wajibu wa kuhakikisha kuwa Sheria zinafuatwa na zinafanya kazi inavyopaswa, hawafanyi kazi zao na wanafumbia macho kwa makusudi ukiukwaji na kuvunjwa kwa sheria.
  6. Sita, hakuna Uongozi na Viongozi. Kila mtu na lwake na Serikali iko Likizo.
  Kuna vitu kadhaa ambavyo nitavigusia kwa undani kuhitimisha au kuainisha maono ya Mchungaji.

  Shida ya Umeme, Uhaba wa Maji, Foleni za Magari, Takataka na Mazingira Machafu.

  Hivi vitu nilivyovitaja hapo juu, ni vitu tosha kabisa kuelewa Tanzania ni Taifa la namna gani na Watanzania ni watu wa namna gani.

  Jiji la Dar Es Salaam, kila siku kuna foleni ya magari inayoanzia saa 11 asubuhi. Ukitoka Kibaha, kwenda Pale Askari Monument, jiandae kutumia si chini ya masaa matatu, iwe ni alfajiri au hata jioni tena ile ya kuondoka mjini saa 2 usiku.

  Sehemu nyingi za mji wa Dar Es Salaam, hazina maji ya kutosha au kuaminika kuwa kutakuwa na maji. Dawasco wamekata mabomba ya watu, wakidai kuna maji ya Mchina, halafu Dawasco hao hao hufuata raia na kuwauzia maji.

  Umeme ni tatizo sugu, kila siku kuna shida ya umeme, iwe ni viwandani, maofisini na majumbani. Unajiuliza, kama Dar ndio kinara cha uzalishaji wa nchi yetu ina shida kubwa namna hii ya Umeme, ni lini tutapata maendeleo?

  Takataka ni kila kona, na kila mtu anajitupia takataka anapopenda. Kila baada ya mita 500, kuna kijilima cha matakataka yaliyozagaa, iwe ni Masaki, Chang'ombe, Manzese au Kariakoo.

  Sasa kilichonishangaza na kuniudhi ni ile tabia ya Watu wa Dar Es Salaam, kuonekana kuwa ama wameridhika na hali hiyo ya kukosa Umeme, Maji, Foleni na Takataka au basi wamekubali kuwa hawana jinsi yoyote ile bali kuikubali hali halisi.

  Wananchi wanasema "what's a big deal about it" na Serikali nayo inasema "what's the big deal about it"!

  Sasa kutokana na tabia hizi, kinachotokea Dar ni vurugu tupu-Chaos, Disorder and Disorganization.

  Watu wa Dar ambao ndipo mtu ungetegemea pangekuwa ndio chimbuko la kuiwajibisha Serikali kwa kutaka Serikali itumikie wananchi, wamekaa kana kwamba wao wanamilikiwa na Serikali (very passive and submissive) na hawana sauti.

  Matokeo yake, kila mtu anafanya analotaka na thubutu umuulize.

  Mfano kwenye foleni za magari, kila mtu anavunja sheria na kanuni za uendeshaji magari ili kuhakikisha anawahi anakotaka kwenda. Lakini ukimuuliza haraka hii ya nini au ina manufaa gani hakupi jibu kama vile anachelewa kazini, anatumia mafuta mengi kwa umbali mdogo au kuwa ni ameudhika kutokana na matuta yaliyojazwa barabarani au udogo wa barabara.

  Hali kadhalika kila mtu mwenye pesa yake anajijengea anavyotaka, bila hati, bila kufuata mipango miji tena mbaya zaidi ni Wasomi ndio wanaoongoza kwa hili.

  Tabia ya kuombaomba na kutegemea imekuwa sana. Zaidi inakera kuwa watu wanaomba hongo bila woga na si ili wakusaidie upate kitu, bali wanakuambia tupatie chakula. Ukimkatalia anakubeza! Watu kutegemea kupewa pesa au misaada ni uonjwa sugu na donda dugu, na hili si la Dar pekee, nenda mpaka vijijini, watu wanasuiri mfadhili.

  Nguvu ziliniishia siku moja nilipoona kwenye gazeti picha ya shule fulani na tamko la uongozi wa shule lililosema kuwa linaomba wafadhili wawajengee Waalimu choo. Sasa mfadili awe ni Mzungu au Mchungaji Kishoka, ni vipi mpaka choo kitushinde kuchimba tusubiri ufadhili?

  Serikali ipo, lakini imelala usingizi mzito kabisa na kukoroma. Haijigusi wala kujiuliza kuwa huu mfukuto wa kero , mwisho wake ni mlipuko mkubwa kuliko yale mabumo ya Mbagala.

  Hakuna Sauti yenye kutoa agizo wala amri. Hakuna nahodha wa kuonyesha dira au kuongoza Merikebu inavyopaswa.

  Lakini Serikali yetu, jamani inajua kuzichuma, ukiangalia nyumba za wakubwa na magari wanayotumia yale ya kifahari, unajiuliza, je hawa ni watumishi wa umma au umma unawatumikia?

  Sasa kwa kuwa Ufisadi ni mfumo ulioshamiri na kukubalika kirahisi na kila mtu kama ndio njia sahihi ya kujipatia mahitaji ili kuondokana na kero, basi vita ya kumkaba koo Jeetu Patel, Chenge na Rostam itakuwa ngumu mno na hata zile kauli za Sitta na Mwakyembe nilizozilaani waliposema wapiga kura wakihongwa wachukue hizo pesa na kuzila, inaonyesha kuwa Rushwa, Takrima na Hongo ni kitu cha ulazima na cha kawaida katika maisha ya Mtanzania.

  Nikirudi kwenye uongozi, nilichobakiwa nacho ni masononeko. Mfumo mzima wa Uongozi na Kiutawala unabidi kubadilika na kubadilishwa, lakini kazi hiyo ni ngumu kwa kuwa ni wananchi wenyewe ndio wanapaswa kubadilika kwanza.

  Kama watu wa Dar wameridhika na dhiki, kero na shida za kila siku na wala Serikali na chama tawala wala havisumbuki au kuhofia kupoteza japo kiti cha Udiwani au Ubunge, je Upinzani Tanzania una kazi gani na manufaa gani?

  Waliojitahidi kuonyesha kukerwa ni wale Wanafunzi wa Kibasila na pale Kimara kwa Msuguri ambao walizuia magari yasipite, wenzao walipogongwa na magari na kupoteza maisha.

  Kwa unyonge tena mkubwa nakubali, Ndivyo Tulivyo!
   
 2. K

  Koba JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  Tungeanza na kuwaondoa CCM!
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Oct 22, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Rev., wow..just wow! Nina mengi ya kusema na unajua jinsi hili jambo la Ndivyo Tulivyo lilivyo near and dear to my heart. Lakini hicho nilichonukuu hapo juu kimenigusa kidogo.

  Ni kweli Watanzania ni mafisadi unique. Hata wale wasio mafisadi kwa matendo ni mafisadi wa kimawazo. Nitoe mfano mmoja tu.

  Kuna huyu jamaa mwizi aliyefungwa jela huko UK, Mponjoli or whatever his name is. Juzi juzi tu hapa head negro in charge aka Invisible alianzisha mada inayomhusu huyo mwizi. Kulikuwa na range of opinions kuhusu matendo na hiyo tabia yake ya wizi.

  Kilichonishangaza na kunisikitisha ni kwamba kuna watu ambao bado wanaona alichokuwa anakifanya (wizi) ni sawa. Wengine walikuwa waki condone. Tuliolaani hiyo tabia yake tulionekana tuna wivu na hayo ni maisha yake kwa hiyo hata tusilaani alichokuwa anakifanya.

  Tendo la baadhi ya watu kuunga mkono alichokuwa anakifanya huyo jamaa kiliniacha kuhitimisha kuwa bado tuna safari ndefu sana dhidi ya hii vita ya mafisadi. Hatutaweza kupigana effectively hii vita kama bado kuna segment kubwa ya watu wenye attitudes za kifisadi.

  We have a serious attitudinal problem here. Mpaka hapo tutakapobadilisha fikra zetu hii vita dhidi ya ufisadi haitafanikiwa. Na kubadilisha fikra jumuia za watu si kid's play na si kitu kinachotokea overnight. Inasononesha kwa kweli.
   
 4. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Na huu ni category gani ya ufisadi??!!!
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Labda tuongeze kuwa watanzania wote wanaumwa ugonjwa wa kuomba uomba. The dependence syndrom is killing us.

  Sauti watu wanazo ila hawajui kama wanazo. Huwa nasikitika kusikia kila mtu kuanzia Rais hadi Matonya wote wanalia shida na kulalamikia vitu ambavyo vingi viko ndani ya uwezo wao. Tuna safari ndefu sana na tuombe Mungu walau tuone mabadiliko kidogo tu kabla ya muda wetu wa kuwepo hapa duniani haujahitimishwa. Very sad in deed!
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Oct 22, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Heck...ain't no rules here. So you can make up your own category...
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kuna kimoja sikukigusia na nilikisahau.

  Serikali inafanya mambo na kuruhusu kuwepo kwa chaos na disorder na hata hili suala la Umeme, Maji, Foleni na Takataka as if kusema inawakomoa Wananchi.

  Badala ya Wananchi ku-react, na wacha Serikali ilete FFU, wananchi wanakubali kuburuzwa na Serikali na vitisho kama vya Dawasco au Tanesco.

  Mambo yanafanywa kwa hiari ya wenye nguvu au kujiamulia na si kuheshimu sauti na umma ambao ndio umetoa dhamana ya kuwepo Serikali tuliyonayo!

  Hivyo Serikali indirectly au directly ina condone kule kukomolewa kwa Raia wake na jibu linabaki kuwa "what's the big deal about it"

  Sasa kama haya ni ya Dar na Upinzani hauna uwezo kuliteka Jiji la Dar na Mkoa wa Dar, iweje tutegemee Upiinzani utaongezeka Bungeni 2010 kwa kupita viti vya vijijini ambao wao hata maji ya bomba na umeme ni kuyasikia Redioni?
   
 8. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  What do we do?!.... haki ya nani tena this country needs some sort of a dikteta lenye mwono na uchu wa maendeleo. Mwendo huu kidemokrasia naona kama hautufai vile...
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  For the time being nothing. Tutabaki kulia lia na kupiga kelele kwa wale wenye roho ya paka kama baadhi ya wachangiaji wa jamvi hili.

  Tatizo la nchi ni KATIBA ambayo inatutengenezea Mungu wetu anayepewa cheo cha Urais. Maadamu hatujapata Rais anayetaka tuishi kama watu huru, basi kazi inabaki mikononi mwa wananchi kufurukuta ili kumlazimisha Mungu wetu atupatie mkate wetu wa kila siku. Hii siyo rahisi hata kidogo kwa sababu huyu Mungu amezungukwa na midude ya kutisha sana kama vile TISS (soma post ya Invicible hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/41767-usalama-wa-taifa-ni-kina-nani-haswa.html). Natamani kutegeneza movie ya kuelezea hii scenario. Very pathetic.

  Tunahitaji neema ya Mungu aliyejuu ili tuweze kujikomboa toka kwenye makucha ya huyu Mungu wetu wa Tz (tena ambaye kalala usingizi na kuwaacha ibirisi watambe). Ipo siku tunaweza kuonja furaha ya kuitwa watu huru!
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkuu, huoni hii kitu ndiyo inayotufanya tuwe wazubaifu na watu wa kugandamizwa?! Mungu wa kweli (kwa waaminio) ametupatia macho, masikio, akili na mikono, n.k. ili tuweze kujimudu. "So I say to you, ask, and it will be given to you; seek, and you will find; knock, and it will be opened to you." (Luke 11:9)

  Mi nasema hivi; ni sisi wa "kuugonga huo mlango", ili watoto na wajukuu zetu wapate kuingia bila kupata adha ya kugonga. I think it is high time for these sacrifices.
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Steve,

  Unasema kweli. Ila watu ambao wanaugonga au wako tayari kuugonga huo mlango ni wachache sana kama wapo. Na hii ndiyo tofauti yetu na majirani zetu kama Kenya. No one is ready (or very few people are willing) to die (even a little) so that others can survive.
   
 12. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  We kuna mtu kaja hapa macho makavu kabisa analalamika kwa nini wasukuma hatuna mafisadi wengi kama proportion ya kabila kwenye population?

  I am proud of this, if indeed it is a fact, lakini huyu bwana kaona hili baya.

  Kuna thread hapa kuhusu watu wa Dar wanavyofaidika na ufisadi na jinsi gani watapata pigo kama ufisadi ukiisha .

  System yenyewe imekaa in such a way mtu hawezi kuishi kwa mshahara, mfanyabiashara analipa zaidi ya nusu ya mapato yake kwenye kodi etc.Inaonekana kama serikali ina institutionalize ufisadi.

  And then watu wengine wanashangaa kwa nini watu hawataki kurudi!
   
 13. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  Naamini Mchungaji Kishoka uko nje. Mimi niko hapa Dar. Hakika huku ni mvurugano mtupu. Taifa hata halionekani linakoelekea. Basi ni mauzauza tu.

  Nimekuwa Morogoro majuzi. Nikakuta watu wanamjadili Lowasa. Kwamba ndiye anayefaa kuwa raisi. Ni raia wa kawaida tu wa mtaani. Nikabaki kinywa wazi. Nikaenda Mzumbe University. Nikakuta maandalizi ya ufunguzi wa bweni la wasichana. Wasomi wa pale wakawa wanapongeza juhudi za Lowasa kufanikisha uchangishaji wa pesa kwa ajili ya ujenzi wa bweni lile. Wali-conclude kitu fulani juu ya huyo bwana. Malizia mwenyewe.

  Raia wana uwezo wa kuleta mabadiliko. Ila kuna kitu kinawazuia/kinawakwamisha kufanya hivyo. Ni nini?
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Malizia utabiri wako basi tukusikie!
   
 15. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Juzi John Mnyika alipendekeza maandamano kuhusu tatizo la umeme akaishia kupigwa madongo humu JF.
   
 16. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo unachosema ni kwamba na wewe Rev. Kishoka!! ni fisadi wa aina fulani...kazi kwelikweli....
  Tanzania iko nafuu (lakini ni mgonjwa ukilinganisha na zambia) labda ungelinganisha na nchi yeyote ndio ingekuwa balanced information
  Kuna watanzania wengi si mafisadi (wengi sana) ila wanakubali kudanganyika (hapo sawa sawa) ..elimu ya uraia (intensive) will change the minds and behaviour
   
 17. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #17
  Oct 22, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Wapi amesema hivyo?!

  ?????
   
 18. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #18
  Oct 22, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Yeye ni Mtanzania au si Mtanzania maana anasema watanzania ni mafisadi wa aina fulani?
   
 19. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #19
  Oct 22, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hajasema hivyo. Labda ukirudia kusoma ujumbe wake utamwelewa fasaha.
   
 20. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #20
  Oct 22, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kweli watz tuna wakati mgumu sana tumejitune akili zetu au kujiendekeza sana kwenye starehe kuliko kazi. wakuu ufisadi umeanzia ngazi ya family. ukimpa mwanao pesa ya kununua kiatu daftari, nguo atatafuta ya bei rahisi ambayo obvious ya low quality anunue ili abakiwe na pesa ya kutanua nayo skuli. mke na mume acha hausigeli akienda sokoni anavyobana chenji, mama akipewa pesa ya mwezi atabana bajeti mpaka abaki na pesa ya saluni wengine pesa ya mchezo, kuna mwanaume aliombwa na mkewe amsaidie kuagiza gari, jamaa alifanya alichofanya gari ya milioni 7 ikawa kumi mke akaja kushtuka late kabisa.makanisani kuna ndugu zangu fulani miaka ya mwanzo ya tisini walikuwa wanagombania uaskofu wa kanda ya kusini wa anglican church mpaka kwa waganga kisa pesa za misaada toka nje, mpaka hapo utaona kuanzia kwenye roots kumeoza ufisadi tumeuhalalisha kwa maneno matamu eti dili.vijana wanaiba sana kwenye makampuni sasa hivi halafu watu wanawasifia, kuna mtu nilimsaidia kupata kazi 2002 yeye ni mtu wa stores, wiki imepita tulikuwa tunakumbushana jinsi ilivyokuwa rahisi kupata kazi miaka hiyo kwenye kampuni nakofanyia nikawa nawaambia watu nilileta cv mbili mojawapo ya huyu jamaa wa stores wote wakapata kazi basi kulikuwa na dada moja akasema mwenzio ana bonge la nyumba mbezi wewe una nini, tayari huko stores jamaa keshauza mali ya kampuni anasifiwa jamani kazi tunayo
   
Loading...