Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TandaleOne, Aug 7, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  From: Ali Rashid <alirashid121@yahoo.co.uk>
  To: "slaa@chadema.or.tz" <slaa@chadema.or.tz>
  Cc: "zitto@chadema.or.tz" <zitto@chadema.or.tz>; "johnbukuku@gmail.com" <johnbukuku@gmail.com>; "saidarfi@chadema.or.tz" <saidarfi@chadema.or.tz>; "issamichuzi@gmail.com" <issamichuzi@gmail.com>; "mjengwamaggid@gmail.com" <mjengwamaggid@gmail.com>; "balozi@tanzania-online.gov.uk" <balozi@tanzania-online.gov.uk>
  Sent: Tuesday, 7 August 2012, 15:33
  Subject: : Yah: Uzinduzi wa Tawi la Chadema-London Kwenye Bar(Pub).  Kwako Mheshimiwa Katibu Mkuu wa Chadema Bwana Slaa.

  Napenda kuleta kwako maoni yangu na Waislam wenzangu waliopo hapa Uingereza kwa kitendo cha Chama chako kuamua kufungua Tawi lake hapa UK Ndani ya bar ikiwa ni kipindi cha Mwezi wa Ramadhani.
  .
  Ni Jambo jema na zuri kwa chama chako kuwa na Matawi nje ya nchi kama ulivyofanya hivi karibuni nchini marekani lakini kwa hapa Uingereza ambapo uzinduzi wake utafanyika Leo majira ya saa mbili usiku takriban masaa saba kuanzia muda huu.

  Kuna Mambo kadhaa ambayo yanatuweka kwenye wakati mgumu hasa sisi Waislam ambao tuko kwenye Mwezi mtukufu wa Ramadhani kwani shughuli yenyewe inafanyika Bar na hata muda wa kufuturu kwa wale tuliofunga ndio muda huo huo ambao shughuli hiyo itakuwa ikifanyika Kwenye Bar ya Thatched House maeneo ya East london.

  Mheshimiwa Katibu mkuu kama nilivyosema kuwa kitendo cha chadema kuwa na tawi hapa uingereza ni hatua kubwa katika maendeleo ya demokrasia ya nchi yetu.lakini ingekuwa vizuri zaidi kama Chama chako kingejaribu kuwatizama watanzania wote bila kujali dini zao au sehemu ya Muungano wa nchi yetu wanaotoka.

  Waislam hatuna tatizo kwenda kushiriki uzinduzi wa chama cha Chadema ndani ya Mwezi wa Ramadhan ikiwa tu muda wa shughuli uwe muafaka(Convenience)usiingiliane na masuala kama haya ya kufuturu. watendaji wako walikuwa na fursa ya kutafuta ukumbi hata wa pound hamsini au pound mia moja lakini kwenye neutral ground ambapo hakuna pombe na kumbi za namna hiyo ziko nyingi East london.

  Mwezi huu wa Ramadhani kwa huku Uingereza sisi tuliofunga tunafuturu kuanzia saa mbili na dakika 40 na kuendelea za usiku.Hapo ndipo linapokuja tatizo la muda wa shughuli hii ambayo ni muhimu kwa kila Mtanzania mpenda demokrasia kama ambavyo chadema yenyewe imekuwa ikijipembejea(ikijinasibu) kuwa ni chama cha demokrasia. kutengwa kwa baadhi ya Watanzania kwenye kushiriki demokrasia ya nchi yetu ni kitendo ambacho hakikutegemewa kupewa nafasi na Chama makini kama chadema.

  Mheshimiwa Slaa ni vyema nikupe taarifa kuwa Watanzania wengi tuliopo hapa Uingereza wanaotoka visiwa vya Zanzibar ni wengi kwa idadi kubwa na ni washiriki wazuri wa Siasa za nchi yetu waswahili wana msemo wao "Wengi wape" na hiyo ndio demokrasia. Eneo hilo la East london watanzania wengi wao wanaoishi hapo ni Wazanzibar kuanzia barking,East Ham, Upton Park,Ilford na Dagenham wingi wao kiasi cha kuweza kununua Msikiti wao, Hapo utakapofanyika mkutano wa chadema eneo la Barking ni hatua chache sana kuna msikitiki wa Watanzania(walking distance), wamenunua Bar na kuifanya kuwa msikiti siku kama ya ijumaa huswaliwa swala tatu kutokana na wengi wao. Kitendo cha kuwa na msikiti wao eneo ni kukuthibitishia idadi kubwa ya Watanzania waislam wanaishi eneo hilo kwa hali yeyote ile ilitakiwa chadema watazame hali za Watanzania wenzi wao.

  Mheshimiwa Slaa katiba ya Nchi yetu imekataza ubaguzi wa kidini au kijiografia na wewe hili unalitambua.Nchi hii ya Uingereza masiala ya equal opportunity policy ni ya lazima kwa kila taasisi ambayo inafanya shughuli zake hapa uingereza na ukija kwenye discrimination nalo ni jambo ambalo halivumiliki kuna sheria nyingi za kulinda haki na hadhi ya binadamu wote.

  Mimi siamini kuwa Watanzania wawe toka kisiwani au wawe wa dini ya kikristo,waislam au wanaomini jadi wasiwe na mchango wowote kwenye kuleta demokrasia kwenye siasa ya nchi yetu.Wewe mwenyewe kuna Mambo mengi ya siasa utakuwa umejifunza kwa Wanasiasa wenzi wako kama mheshimiwa Hamad Rashid,mheshimiwa Jussa,Mabare Marando,James Mapalala,Austine Mrema,Hamad Rashid ambaye alikuwa kiongozi wako wa Kambi ya upinzani bungeni na kabla yake alikuwepo Mama Fatma Maghimbi kama kiongozi wako, nina imani hao viongozi wamekupa ujasiri na muongozo mkubwa.

  Mheshimiwa Slaa nakuandikia wewe nikijua ndiye mtendaji mkuu wa Chama hivyo una uwezo wa kulihamisha zoezi kutoka kwenye Bar ya Thatched na kutafuta neutral ground hata pale kwenye msikiti wa Watanzania kuna ukumbi ambao unakodishwa kwa bei ndogo. lakini ili kulifanya zoezi lifanikiwe vizuri kuna Community Halls ziko nyingi na unaweza kupata wakati wowote na kutumia ukumbi wa msikiti nako itakuwa ni kuwabagua wasio waislam. muda ulipo wa masaa haya saba unatosha au si vibaya hata kulifanya zoezi hili kwa weekend.

  Mheshimiwa Slaaa unaweza kutizama Blog za Mjengwa.blogspot.com au jestina George ukaona tangazo la chama chako kufanya shughuli hii muhimu na ya kihistoria lakini kwa bahati mbaya ndani ya BAR. hata imagine ya chama inaharibika kwa tukio muhimu la kihistoria kufanyikia Bar. inaonekana hamkuwa serious au hamko serious, mara nyinyi chadema mmekuwa mkija kwenye mikutano ya Chama cha Conservative cha hapa na Cuf wamekuwa wakija kwenye mikutano ya liberal Dem. hapa Uingereza hakuna mikutano inayofanyika bar huwa kwenye kumbi mbali mbali.

  Kwa heshima kubwa naomba nikurejeshe kwenye Tangazo la chama liliko kwenye blog mbali mbali.
  "Chadema inapenda kuwatangazia watanzania wote waishio London na sehemu za jirani kuwa kutakuwa na mkutano wa ufunguzi wa Tawi la Chadema london,Tawi ambalo litafunguliwa na mheshimiwa Godless Lema,ufunguzi huo utafanyika Thatched house Pub iliyopo Barking siku ya leo 7/08/2012 saa 20.00 mbili usiku Mawasiliano chris lukosi 07404279633,07903828119"

  Mheshimiwa Slaa nina amini una uwezo mkubwa wa kurekebisha kasoro hii ambayo ina misingi ya udini na ubaguzi wa kijiografia ya nchi yetu na kinyume na katiba ya nchi yetu.

  nina imani nawe kama mtu makini na Muadilifu,hatuwezi kuwasiliana na Bwana Lema kwa vile tayari mahakama kuu imekutana na hatia ya ubaguzi wa kidini kiasi cha kuvuliwa ubunge wake, mtu ambaye amewabagua Watu wa Arusha kwa dini na jinsia akileta ubaguzi huo huku ughaibuni ambako sisi Watanzania tunategemeana kwenye shida na raha, yeye ataondoka baada ya siku kadhaa huku nyuma kishatugawa na kuondoa umoja wetu wa watanzania.Hapa Uingereza kuna chama kikongwe kabisa kwa siasa za nje Cuf ambacho kina matawi Marekani na Canada na sehemu nyingine lakini hakijawahi kuwabagua watanzania walio nje mikutano yao yote hufanya kwenye kumbi ambazo mtu yeyote anaingia.halikadhalika CCM nao wana Tawi lao hapa mikutano yao haijafanyika bar katika kipindi kama hichi cha Mwezi wa Ramadhani.

  Mwisho naomba nikukumbushe maoni ya mzee Mtei muasisi wa chadema pale ilipoundwa tume ya Katiba alilalamika sana kuwa tume ina wajumbe wengi wenye majina ya kiislam hasa waliotoka Zanzibar akahisi kuwa Haki hakufuatwa na akakosa raha kabisa.

  .kitendo cha kuzindua chama Bar ni kuwakimbiza waislam wasiombe au wasishiriki nafasi za uongozi. ingekuwa Mwezi wa kawaida ambao si kama huu Ramadhai wapo waislam wanaokwenda bar lakini wengi wao ukifika mwezi mtukufu hawaendi Bar, jee watashiriki vipi kwenye Chama chako?usisahau minong'ono mingi kuwa chadema ni Chama chenye mlengo wa kikristu,kwa matendo haya ya Lema ni kuthibitisha shutuma au hisia hizo.

  Mheshimiwa Dr.Slaa samahani kwa kukuchosha ila kwa heshima na taadhima naomba kuwasilisha kilio cha Waislam watanzania waliopo Uingereza dhidi ya vitendo vya ubaguzi wa wazi unaofanywa na chama chako.

  Nakutakia kazi njema na natarajia ya kuwa utalifanyia kazi ombi letu sisi Waislam wa Uingereza.
  Ni mimi mpenda demokrasia na Maendeleo.


  From: Ali Rashid <alirashid121@yahoo.co.uk>
  To: "slaa@chadema.or.tz" <slaa@chadema.or.tz>
  Cc: "zitto@chadema.or.tz" <zitto@chadema.or.tz>; "johnbukuku@gmail.com" <johnbukuku@gmail.com>; "saidarfi@chadema.or.tz" <saidarfi@chadema.or.tz>; "issamichuzi@gmail.com" <issamichuzi@gmail.com>; "mjengwamaggid@gmail.com" <mjengwamaggid@gmail.com>; "balozi@tanzania-online.gov.uk" <balozi@tanzania-online.gov.uk>
  Sent: Tuesday, 7 August 2012, 15:33
  Subject: : Yah: Uzinduzi wa Tawi la Chadema-London Kwenye Bar(Pub).
   
 2. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  nijuavyo mimi mzee wetu dkt Slaa nimwelewa sana wa mambo. sitaki kuamini kama hili lilifanywa pasipo kujali matokeo yake yatakuwaje, nadhani pengine wahusika wakuu wa maandalizi ya hafla hii ya ufunguzi wa hapo Londoni walipitiwa tu. ila ngoja tusikilize ujumbe kutoka kwa katibu wetu mkuu dkt.Slaa atasema nini. lakini hili kosa moja tuombe kuvumiliana kwani changamoto zilizo mbele yetu zinatuhitaji kuwa wamoja katika misingi ya kuheshimiana na kuvumiliana kulingana na tofauti zetu za kiimani.
   
 3. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Uzinduzi wa Tawi la Chadema-London Kwenye Bar mwezi mtukufu wa Ramadhani unatoa tafsir gani kwa watanzania wenye IMAN ya dini ya KIISLAMU juu ya kitendo hiki cha Chama Kikuu cha Upinzani Hapa nchini.?


  Waislamu ambao wanaamini kuwa mwezi huu ni mtukufu kwao na hivyo wanauheshimu na kuutukuza kwa kuacha matendo yote yaliyo mabaya lakini pia wanajizuia na kwenda maeneo yenye kutoa ushawishi wa kufanya mabaya kama sehemu zinazouzwa vilevi.


  Kwa kitendo chao hiko waislamu waishio london wameamua kumuandikia barua katibu mkuu wa chama hicho kuwasilisha madai yao hayo ambapo pia wameuandikia ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza wakilaani kitendo hiko cha CHADEMA.
   
 4. K

  Kwayu JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Zitto kazini!
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Aliyeleta huu uzi ni kibaraka mwaminifu wa Magamba.Nimeamini CDM imewashika pabaya.M4C Forever
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mwanachama gani wa CDM ataandika ujinga kama huu halafu awakopi ubalozi na michuzi asimkopi Mbowe? Huu ni ukichaa wa Magamba.
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Waisla si wajinga kama unavyodhani bwana Magamba.
   
 8. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Inatia uvivu kusoma......kama hii taarifa ilitolewa mapema ni kwanini hukufikisha malalamiko yako sehemu husika(huko London)kwa waandalizi wa hii shughuli ili uone kama wangeweza kubadilisha au vipi. Sasa kwanini unatoa malalamiko leo siku ya tukio?????tena sio siku ni masaa mawili kabla......sidhani kama una jema wewe.
   
 9. M

  Molemo JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Siyo Zitto mkuu wangu ni vibaraka wa Magamba wameona ile Chopa wakachanganyikiwa.Nimeamini hakuna wa kumzuia Dr Slaa kuingia Ikulu
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Halafu huyu magamba anamkopi Michuzi,Mjengwa na ubalozi anamwacha Mbowe.Kweli M4C imewashika
   
 11. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,199
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Sasa wakihamishia Msiktini si utaomba Lema asije? Maana umeshamhukumu kwammba ni mbaguzi wa dini?
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu wala usihangaike,huyo Magamba anadhani propaganda ya udini bado ina nguvu.
   
 13. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwa nini asingetaarifu mapema. Mwezake Habib Mnyaa pale Bungeni wiki jana kamkatalia SPika kuendeleza vipindi vya bunge hadi kufanya wabunge wawe Dodoma hadi siku ya tarajiwa ya Ramadhani kulingana na muandamo wa mwezi.

  Habib alifiksha hoja yake vizuri na hakuonyesha elements zozote za kubaguliwa waislamu.

  Sasa, kuhusu unajisi wa sehemu sijui tunasemaje. Kwani hata wangepanga mkutano ufanyikie hotelini, ni hotel gani humu duniani ambayo haina bar lounge?

  tena afdhali hata bar watu wanakunywa na kuondoka. Hotel zote duniani zinaongoza kwa shughuli ya kutiana tena ikibidi kinyume na maumbile. Hivyo, kuna uchafu mwingi kwenye hotel kuliko hizo bar.

  Tena kwa mwislamu hakuna hotel duniani ambayo haipiki nguruwe japo huku uswahili mnakiita kitimoto. Sasa wangefanyia wapi kama ulikuwa mtu wa visa lazima ungepata kisa tu cha kulinganisha na uislam.

  Kwa nini huyu jamaa hakuwakataza wachezaji wa ligi ya Tanzania kutovaa jezi za Breweries ambako ni dhahiri ku-promote pombe.

  Mimi ni mkristo na nimefurahi sana baadhi ya wakristo wenzangu kukataa ile desturi tuliyowadekeza wenzetu waislamu kwamba eti ukiwa na sikukuu lazima umwite mwislam aje akuchinjie kuku au ng'ombe.

  Sasa, kama si mbinu na uchochezi, kuvuliwa ubunge wa Lema kule Arusha kunahusiana vipi na ubaguzi wa waislam. Inabidi ifike mahala tuone kwamba kama waislam hawapendi chama fulani hapa nchi tuache kuwabembeleza wafanya watakalo tujue tumeshawapoteza.

  Kuliko leo kuna kuchoma makanisa, kesho kuna kukataa muungano, lesho kuna tujiunge na OIC. Tuwaache waamue wanavyotaka na jikitie na kukabiliana na hali hiyo.
   
 14. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ni wehu, kama hutaki usiende siyo kuandika porojo kibaooooooo. Mbona tunao waislamu wengi tunaenda nao party ndani ya Mwezi Mtukufu? Tena kwenye BAR?. Kwa jinsi ulivyoandika siyo kama unataka kwenda ili ushiriki lakini umeandika kifitina..Nanusa harufu ya U-CUF hapa..Hya basi..ili uridhike waalike MSIKITINI. Kichwa maji
   
 15. Kambaku

  Kambaku JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 1,987
  Likes Received: 2,891
  Trophy Points: 280

  Mkuu najua una hasira labda au umekereka kutokana na mtoa hoja ila sio kama umetumia maneno makali sana kumjibu? Tena kwa kuzingatia hoja yenyewe iko jukwaa la kila mtu
   
 16. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #16
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Inawezekana kuwa kuna wanaokwazika kama shughuli itafanyika kwenye pub, lakini huyo mwandishi ana akili timamu kumtuhumu Lema kama vile Lema ndiye mwandaaji wa shughuli hiyo! Yeye na wenzake walioko London wanaolalamika wameshiriki vipi kuijenga Chadema huko waliko? Siku zote wako kimya na hila zao, wanategea tu kuona vihitilafu vya ajabuajabu ili wadandie kama nzi na kung'ang'ania hapo na makelele kibao! Hata kama mkutano huo ungefanyikia sehemu na mda tofauti bado wasingekosa sababu na visingizio vya kipuuzi, angalia kumbe kwao Lema ni mbaguzi wa kidini!!! Nilidhani mwezi huu watu wanaacha unafiki na chuki za kijinga, kumbe... uzao wa nyoka haubadiliki.
   
 17. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #17
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Thread za kichonganishi hizi za kutengenezea ofisini kwa wakina nape wakishirikiana na rejao na ritz
   
 18. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #18
  Aug 7, 2012
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Aliyowahi kuandika tandale one ....unaweza ukamjua ni nani ,  Urais 2015, Rushwa vyaitesa CHADEMA.

  Started by TandaleOne, Today 13:53 2 Pages &#8226; 1 2
  • Replies: 37
  • Views: 371
  Last Post By: Last Post: Today 19:19 by Wamunzengo [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa

  [h=3]Ufunguzi wa tawi la chadema uk leo,waislam wamwandikia barua dr slaa kulalamika.[/h] Started by TandaleOne, Today 18:10


  • Replies: 15
  • Views: 124
  Last Post By: Last Post: Today 19:26 by punainen-red [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]Kikwete: Utekelezaji wa ahadi zangu umeshaanza![/h] Started by TandaleOne, 23rd July 2012 17:56 2 Pages &#8226; 1 2


  • Replies: 33
  • Views: 590
  Last Post By: Last Post: 30th July 2012 13:31 by Mr Rocky [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]Tetesi: Baada ya kuimaliza NCCR, Marando sasa aanza na CHADEMA[/h] Started by TandaleOne, 27th July 2012 17:15 5 Pages &#8226; 1 2 3 4 5


  • Replies: 95
  • Views: 2,074
  Last Post By: Last Post: 29th July 2012 16:37 by Young Tanzanian [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]NAPE anaunguruma Viwanja vya Shule ya Kashaulini Mpanda sasa hivi.[/h] Started by TandaleOne, 15th July 2012 17:04 2 Pages &#8226; 1 2


  • Replies: 27
  • Views: 336
  Last Post By: Last Post: 15th July 2012 21:29 by dudus [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]Nape atoa angalizo hali ya Uchumi; awaponda CHADEMA[/h] Started by TandaleOne, 14th June 2012 14:25 3 Pages &#8226; 1 2 3


  • Replies: 50
  • Views: 1,019
  Last Post By: Last Post: 15th June 2012 08:26 by cerezo [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]Dr Slaa Jibu tuhuma hizi...![/h] Started by TandaleOne, 5th March 2012 13:24 11 Pages &#8226; 1 2 3 4 5 ... 11 [​IMG]


  • Replies: 209
  • Views: 7,330
  Last Post By: Last Post: 11th June 2012 21:46 by christine ibrahim [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]Ni msimu wa kalamu au kalamu za msimu (tofauti ya wahariri na uhariri)[/h] Started by TandaleOne, 9th June 2012 19:04


  • Replies: 1
  • Views: 110
  Last Post By: Last Post: 9th June 2012 19:24 by the horse [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]Ufafanuzi wa hotuba ya "upotoshaji" ya Zitto kwa watanzania waishio Marekani[/h] Started by TandaleOne, 30th May 2012 12:40 7 Pages &#8226; 1 2 3 4 5 ... 7


  • Replies: 137
  • Views: 2,957
  Last Post By: Last Post: 31st May 2012 10:58 by ndinga [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]Asili ya mfumo wa serikali mbili.[/h] Started by TandaleOne, 30th May 2012 08:52


  • Replies:
  • Views: 71
  Last Post By: Last Post: 30th May 2012 08:52 by TandaleOne [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]Tetesi: Kwa haya, Utaifa wa chadema una walakini...![/h] Started by TandaleOne, 27th April 2012 13:46 4 Pages &#8226; 1 2 3 4


  • Replies: 72
  • Views: 1,855
  Last Post By: Last Post: 29th April 2012 15:34 by pinguli [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]"..Ushupavu wa Uongozi.." na mgomo wa madaktari - Mheshimiwa Benjamin W. Mkapa[/h] Started by TandaleOne, 9th March 2012 09:59


  • Replies: 6
  • Views: 629
  Last Post By: Last Post: 9th March 2012 11:36 by Nteko Vano [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]Salamu za Rambi rambi kutoka kwa NAPE...![/h] Started by TandaleOne, 23rd December 2011 09:04


  • Replies:
  • Views: 167
  Last Post By: Last Post: 23rd December 2011 09:04 by TandaleOne [​IMG] Forum:
  Habari na Hoja mchanganyiko  [h=3]CHADEMA na Utata wa kimantiki[/h] Started by TandaleOne, 22nd November 2011 09:27 2 Pages &#8226; 1 2


  • Replies: 27
  • Views: 887
  Last Post By: Last Post: 22nd November 2011 20:17 by mtz flani [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]CHADEMA ni kama CCM..,ama mbaya kuliko CCM...![/h] Started by TandaleOne, 10th November 2011 10:40 2 Pages &#8226; 1 2 [​IMG]


  • Replies: 33
  • Views: 969
  Last Post By: Last Post: 12th November 2011 12:25 by MTAZAMO [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]Ripoti ya "ajabu" ya NAPE huko Houston...![/h] Started by TandaleOne, 31st October 2011 11:39 5 Pages &#8226; 1 2 3 4 5


  • Replies: 94
  • Views: 3,411
  Last Post By: Last Post: 3rd November 2011 23:56 by George Kahangwa [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]Salva Rweyemamu maneno haya ni yako?[/h] Started by TandaleOne, 25th October 2011 21:57 4 Pages &#8226; 1 2 3 4 [​IMG]


  • Replies: 60
  • Views: 1,711
  Last Post By: Last Post: 26th October 2011 16:04 by Never give up [​IMG] Forum:
  Habari na Hoja mchanganyiko  [h=3]The democracy of the party for democracy and progress (cdm)[/h] Started by TandaleOne, 25th October 2011 12:37


  • Replies: 4
  • Views: 131
  Last Post By: Last Post: 25th October 2011 18:47 by afroPianist [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]JK's Popularity On Twitter[/h] Started by TandaleOne, 29th April 2011 14:00 2 Pages &#8226; 1 2


  • Replies: 20
  • Views: 1,100
  Last Post By: Last Post: 1st May 2011 03:41 by afrodenzi [​IMG] Forum:
  Celebrities Forum  [h=3]Yu wapi mgombea mwenza wa CHADEMA?[/h] Started by TandaleOne, 25th September 2010 02:50 3 Pages &#8226; 1 2 3 [​IMG]


  • Replies: 56
  • Views: 1,789
  Last Post By: Last Post: 21st October 2010 16:41 by Mwishowao [​IMG] Forum:
  Tanzania 2010-2015  [h=3]News alert:Mgombea urais NCCR- Mageuzi Azomewa[/h] Started by TandaleOne, 16th October 2010 08:49


  • Replies: 5
  • Views: 428
  Last Post By: Last Post: 17th October 2010 03:44 by Kibunango [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]Rangi Hii Ina Maana Gani?[/h] Started by TandaleOne, 16th October 2010 09:33


  • Replies: 10
  • Views: 506
  Last Post By: Last Post: 16th October 2010 13:54 by sijui nini [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]Hawa ni hatari zaidi kwa taifa letu[/h] Started by TandaleOne, 16th October 2010 08:47


  • Replies: 6
  • Views: 553
  Last Post By: Last Post: 16th October 2010 12:01 by lebabu11 [​IMG] Forum:
  Tanzania 2010-2015  [h=3]Nani mmiliki wa Alba Apartments alipokuwa akiishi Dr.Slaa?[/h] Started by TandaleOne, 8th October 2010 14:48 2 Pages &#8226; 1 2 [​IMG]


  • Replies: 35
  • Views: 1,395
  Last Post By: Last Post: 10th October 2010 10:56 by grandpa [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]Dr.Slaa Vs Jean-Bertrand Aristide(The prophet of deception)[/h] Started by TandaleOne, 9th October 2010 20:09 [​IMG]


  • Replies: 19
  • Views: 471
  Last Post By: Last Post: 10th October 2010 09:41 by MartinDavid [​IMG] Forum:
  Tanzania 2010-2015  [h=3]Is Media In East Africa Ignoring Tanzania Elections?[/h] Started by TandaleOne, 8th October 2010 18:40


  • Replies: 6
  • Views: 325
  Last Post By: Last Post: 8th October 2010 23:33 by Mwafrika [​IMG] Forum:
  Tanzania 2010-2015  [h=3]Hivi ni kweli hawa wanaota ndoto?[/h] Started by TandaleOne, 8th October 2010 14:43


  • Replies: 18
  • Views: 509
  Last Post By: Last Post: 8th October 2010 17:50 by Kibunango [​IMG] Forum:
  Tanzania 2010-2015  [h=3]EU observers in Tanzania for polls[/h] Started by TandaleOne, 8th October 2010 14:33


  • Replies: 4
  • Views: 179
  Last Post By: Last Post: 8th October 2010 17:20 by Mshirazi [​IMG] Forum:
  Tanzania 2010-2015  [h=3]Kompyuta milioni moja kusambazwa kwa wanafunzi[/h] Started by TandaleOne, 1st October 2010 20:53 [​IMG]


  • Replies: 11
  • Views: 420
  Last Post By: Last Post: 3rd October 2010 02:26 by Bigirita [​IMG] Forum:
  Jukwaa la Siasa  [h=3]Hawa ni wakwepa kodi wakubwa?[/h] Started by TandaleOne, 1st October 2010 20:47
   
 19. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #19
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  pole sana mleta mada.......
  m4c imewashika pabaya sana
   
 20. d

  danizzo JF-Expert Member

  #20
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli cdm imekosea. Sielewi kwanini wanachama wengi wapo upande mmoja[ukristo] haileti picha nzuri. Pengine ule msemo wa padri unaukweli ndani yake WAISLAM AMKEN HAMNA CHENU APO
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...