Ufunguo wa furaha katika ndoa ni kumpenda mume kuliko watoto?

Kumpenda mume si kula wala kupika. Na kuna tofauti kati ya kumpenda mtu na kumuogopa. Naona hapa watu wanazungumzia wanawake wanaowaogopa waume zao.

Baba akiingia ndani watu mbio....

Huu mbona ni upuuzi wa mwaka 47!
Kwanza mtu mzima haitaji kula kiviiile maana keshakua..anachohitaji ni ukarabati wa afya na kujiweka hai tu.
Watoto ndio wanahitaji kula zaidi tena vyakula kama maziwa, nyama etc.
Kumlea baba kama mtoto ni uzembe.
Halafu jamani, kwani upendo ni chakula?
 
Mnakosea sasa! Vitabu vya dini, samahani kwa nitakaemkwaza, vinasema 'mwanaume ampende mkewe' tena kwa 'akili'. Mwanamke anapaswa kutii tu yale yanayofaa kutii. Watoto wanapaswa kulindwa na kufundishwa na wazazi wote. Sasa wanawake siku hizi tunajipa jukumu la 'kupenda' tena hadi kutunza familia. Ndo maana vilio havituishi. Mi nimeamua nitulie tuliii nipendwe tu
NB: msiniwakie sana, nnakuwaga na moyo,lol
Wanaume wangapi wanatimiza majukumu yao kibiblia?
Wasipotimoza wanawake wakae tu huku wakilalamika?Just asking.
 
Formulae inaanzia kwa mwanaume kumpenda mwanamke. Sasa ukipendwa automatikale unajikuta unatii. Si ndo kutulia nako inakuja automatikale pia? Well,jokes aside; watoto ni muhimu kupendwa na wazazi wote wawili. Manake kuna wabab utadhani walibakwaga!
Hebu tupe hiyo formula yako ya kukaa tuliii upendwe.Inakuwaje mwenzetu?

Kumpenda mume si kula wala kupika. Na kuna tofauti kati ya kumpenda mtu na kumuogopa. Naona hapa watu wanazungumzia wanawake wanaowaogopa waume zao.

Baba akiingia ndani watu mbio....

Si ndio hapo sasa! Tatizo liko hapo... wengine husema " the way to a man's heart is through his stomach' sijui huwa inamaanisha nini.
 
Formulae inaanzia kwa mwanaume kumpenda mwanamke. Sasa ukipendwa automatikale unajikuta unatii. Si ndo kutulia nako inakuja automatikale pia? Well,jokes aside; watoto ni muhimu kupendwa na wazazi wote wawili. Manake kuna wabab utadhani walibakwaga!

Sasa Shosti,
wengi wa hao wanaume hawanaga mapenzi..utasbiri wee upendwe..wapi!
Ila wangejua kuwa wakipenda wake zao automatically wake watawatii ile mbaya.
 
Si ndio hapo sasa! Tatizo liko hapo... wengine husema " the way to a man's heart is through his stomach' sijui huwa inamaanisha nini.

saafi kabisa Tausi...ndoa kupendana na upendo kwa baba haumaanishi eti kumgwaya kama simba na vile vile upendo kwa watoto ni muhimu japo vitu vinatofautiana
 
Biblia inakataza kabisaa kulalamika. Tena inaongelea juu ya ndugu akikosea muonye kwa upendo, ikishindikana muitie wazee. Na pale mwenzio yuko weak u can be strong, bila kuzidisha. Wanawake wa siku hizi tunajivalisha sarawili,dunia yote kama tumeibeba mabegani!lol, leo nimekunywa madhiwa akili sijui imekaaje hehehe
Wanaume wangapi wanatimiza majukumu yao kibiblia?
Wasipotimoza wanawake wakae tu huku wakilalamika?Just asking.
 
Si ndio hapo sasa! Tatizo liko hapo... wengine husema " the way to a man's heart is through his stomach' sijui huwa inamaanisha nini.

Good food.

Wengine wanawapenda wake zao ila hua wanakwepa kula nyumbani.Sasa huo muda wa kukwepa mlo angekua anaharakisha nyumbani kwasababu mkewe kapika chakula kizuri anachokipenda huoni "quality time " yao ingeongezeka?
 
Utakuwa una maana kuwa mwanamke anayejua sana kupika automatically atakuwa na mume anayempenda. Ngoja tufanye research maana in rela life situation sija experience hii kitu. Nawajua wengi ambao hawakooi mume huyo na hawajuhi hata jiko linafananaje; ni good managers tu wa wafanyakazi wa ndani.

Si ndio hapo sasa! Tatizo liko hapo... wengine husema " the way to a man's heart is through his stomach' sijui huwa inamaanisha nini.
 
Biblia inakataza kabisaa kulalamika. Tena inaongelea juu ya ndugu akikosea muonye kwa upendo, ikishindikana muitie wazee. Na pale mwenzio yuko weak u can be strong, bila kuzidisha. Wanawake wa siku hizi tunajivalisha sarawili,dunia yote kama tumeibeba mabegani!lol, leo nimekunywa madhiwa akili sijui imekaaje hehehe

Unakuwaje strong bila kuzidisha ikiwa situation inakulazimu?
 
Chakula cha nyumbani kuwa kitamu si lazima kiwe kimepikwa na wife.; kwani huko anakokula kapika nani?
Good food.

Wengine wanawapenda wake zao ila hua wanakwepa kula nyumbani.Sasa huo muda wa kukwepa mlo angekua anaharakisha nyumbani kwasababu mkewe kapika chakula kizuri anachokipenda huoni "quality time " yao ingeongezeka?
 
Chakula cha nyumbani kuwa kitamu si lazima kiwe kimepikwa na wife.; kwani huko anakokula kapika nani?
Wewe kweli Nyumba Kubwa! Si mchezo!
Hata yule Sous Chef siyo lazima apike.....wako wapishi wasaidizi na chakula kinatoka bomba!
Siku akiingia mwenyewe jikoni....kila mtu hachezi mbali maana wanajua mipigo ilivyo! Kama ulivyosema kwenye post yako nyingine mama anaweza kusimamia siyo lazima kuutwa kushinda jikoni.
 
Huu mbona ni upuuzi wa mwaka 47!
Kwanza mtu mzima haitaji kula kiviiile maana keshakua..anachohitaji ni ukarabati wa afya na kujiweka hai tu.
Watoto ndio wanahitaji kula zaidi tena vyakula
kama maziwa, nyama etc.

Kumlea baba kama mtoto ni uzembe.
Halafu jamani, kwani upendo ni chakula?

Hapana upendo si chakula ila ni mfano tu wa jinsi mke alivyoweka concetration kwa mwanaume na kusahau watoto, we angalia kwenye mafundisho ya ndoa including kitchen party ni mara ngapi mwanamke anapata mafundisho ya kulea watoto hakuna ni kumfurahisha mwanaume tu.
 
Asilimia kubwa ya wadada wanakuja hawajuhi kupika kwa kuwa wametokea familia masikini hivyo chakula anachojua ni cha kuchemsha tu.

Unachopaswa kufanya kama wife ni kumpiga shule huyo dada basi, baada ya muda anakuwa na yeye mwalimu.

Nina dada yangu yeye ma house girl wake anawapeleka kozi kabisa ya kupika na anasema itawasaidia hata mkiacha kazi.

NK sio wote wana bahati ya kupata wadada wanaojua kupika chakula kizuri.
 
Back
Top Bottom