Ufukarishaji unaoendelea Kiteto

Msengi Kiula

Senior Member
Jan 10, 2008
167
63
Watawala wamewaondoa watu kwenye makazi ya wakulima Kisima, Changarawe/Mlyongima, kwa Magere/Butiama, kwa Rama, Pori kwa Pori # 2, Milima 3 nk kwa hila na kuumba tatizo la wakimbizi wa ndani(IDP's) kimya kimya.

Watu wamevunjiwa makazi yao, wameswagwa na kurundikwa Pori kwa pori #1 kwa nguvu za dola bila msaada ukiwa ni umbali wa takribani km 15 --25 kutoka walipokuwa wamelima na mazao kustawi.

Sasa hivi mashamba yao ni malisho ya wafugaji. Mtu kwenda kuhami shamba ni uadui.

Tunakwenda wapi? Ipo wapi hekima?

Kisima palikuwa na msikiti, nyumba ya mchungaji wa Anglikana, makazi ya kudumu na shule ilishaanza kujengwa!

Swali: Dar es salaam si ilianza kama kambi ya wavuvi?

Hoja: Nimeona kwenye taarifa za habari Mkuu amehalalisha wavamizi wa kiwanja cha serikali kule Kahama. Hawa tunaowazungumzia hapa siyo wavamizi, ni wachakarikaji- wakulima na mnyororo wa watoa huduma mbalimbali.

Tume ya Pinda iliyoongozwa na viongozi wa dini ilifanya kazi nzuri. Nini kimetokea ghafla kimya kimya na Lukuvi kupotoshwa?

Mbunge naona amezidiwa nguvu na aibu hii iliyotekea hakuna wa kuwasemea; ni ubabe ubabe tu!

Maendeleo yanaletwa na wananchi. Hali ya kulundikwa, imeleta matatizo mengine kabisaaa! Yepi hayo?

Kwa vile uwazi na ukweli unahitajika ,CCM liangalieni hili kwenye vikao vyenu muone serikali yenu ilivyofanya Kiteto. Mtagundua mengi! Kuna "ATM's" mahali zinazopotosha haki?

Jambo hili halijaripotiwa mahali popote kwenye vyombo vya habari hapa nchini. Amkeni! !
 
Srikali hii inawajali sana wanyonge. Kwa kuwafukuza hivo ndiyo wataufikia uchumi wa viwanda.
 
Hili limenishangaza sana.

Mbona Mbeli, na Mbigiri hawafukuzwi?

Ila kwa Rama bado kuna watu wanaishi hapo, japo umedai wanatimuliwa.

Nilibishana na mtu kisheria kuhusu uhalali la fukuza fukuza hii na kumwambia si halali kabisa ila akabisha
 
Kwa awamu hii hizi ni kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji labda miujiza itokee.
 
Kitu kinachofanyika hapo kiteto wafugaji(wamasai) wanahonga viongozi wa serekali na kuumba migogoro na hatimae kuja na hoja kwamba hayoo maeneo ni hifadhi. Hivyoo wakulima wote waondolewe ili wafugaji(wamasai) wapate maeneo makubwa ya malisho.


Hili swala linamuhusu kingwangala na lukuvi LAKINI MPKA WAKAOMBE KIBALI Kwa MNYETI asije akatengeu maamuzi yao.
 
Back
Top Bottom