Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 3,529
- 3,432
Licha ya Nchi ya Tanzania kuwa katika ukanda wenye hali ya hewa inayoruhusu uwepo na ukuaji wa viumbe wengi wakiwemo wadudu na mimea bado uwekezaji kwenye kilimo cha ufugaji wa wadudu lishe unaonekana kuwa wa chini sana ukilinganisha na nchi nyingine Duniani. Tanzania inaonekana kuwa nyuma sana katika uwekezaji kwenye kilimo cha ufugaji wa wadudu licha ya tafiti nyingi kuonesha uhitaji mkubwa wa wadudu lishe ambao wanaweza kuwa chanzo kikubwa cha protini.
Watanzania wengi leo wanachukulia kilimo cha ufugaji wa wadudu kwa ajili ya chakula cha binadamu na mifugo kama jambo la kustaajabisha na lenye nafasi ndogo sana katika sekta ya kiliimo licha ya Tafiti nyingi za Shirika la chakula Duniani kuonesha muelekeo wa dunia kwenda kwenye uhitaji wa protini na virutubisho vingine vinavyotokana na wadudu.
Wakulima wengi nchini wanawachukulia wadudu kama viumbe waharibifu na wasiweza kuwa sehemu ya fursa. Ni sehemu ndogo sana ya wakulima wanaoweza kuona thamani ya wadudu na kuwekeza katika kilimo hicho. Wakulima wanaowekeza kwenye kilimo cha ufugaji wa wadudu huonekana mara kadhaa kama watu wa kustaajabisha.
Ufugaji wa wadudu Tanzania unafanyika kwa kiasi kidogo sana na ni katika maeneo machache mfano katika vyuo kama Chuo cha kilimo cha Sokoine na vyuo vingine vya kilimo huku wakulima wengine wakibaki katika ombwe la kukosa maarifa na elimu pana juu ya kilimo cha ufugaji wa wadudu. Siyo jambo la kushangaza kuwakuta wanajamii wengi nchini wakielezea wadudu kama sehemu ya chakula walichotumia wazazi wao na siyo sehemu ya kilimo kinachohitaji uwekezaji kama kilimo cha ufugaji wa viumbe wengine na sehemu ndogo sana ya jamii nchini ndiyo inayoendeleza utamaduni wa kutumia wadudu lishe lakini haijawekeza kwa dhati katika kilimo hicho.
Ufugaji wa wadudu ni kilimo kinachoweza kuwa sehemu ya kupunguza wimbi la vijana wanaokosa ajira nchini na hivyo kuliongezea taifa pato. Hali halisi inaonesha kilimo ni uwanja mpana ambao Tanzania kama mchezaji bado inachezea nusu ya uwanja.