Ufugaji wa sungura ni dili ukiachana na longolongo za wababaishaji

Nyaru-sare

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
3,721
2,000
hu
Ni kweli ni gharama nafuu sana kufug sungura. Gharama kubwa iko kwenye miundombinu. Kwa maana ya banda la kisasa. Ni vyema kama umekusudia kufuga ukagema na mkojo.

Ni mradi mnzuri kama utaunganisha na mradi wa bustani au kilimo.

Kuhusu soko ni kweli watu wengi hawali nyama ya sungura. Sio kuhusu mazoea. Wanakula kile kinachopatikana kwa wingi na kwa bei nzuri.

Inahitaji ubunifu kidogo tuu kuiingiza nyama ya sungura sokoni. Unaiongezea thamani. Kwa mfano unaweza tengeneza Sosage, sambusa, au kuuza kama nyama ya kusaga yenye viungo. Mradi tu usiwe na lengo la kupata utajiri wa haraka kwa kudhani utauza kwa malaki ya pesa utaumia.
huo mkojo unazalisha umeme?
 

AbouZakariya

JF-Expert Member
Mar 19, 2013
1,325
2,000
Hana kwato, basi hata punda muislamu ale maana ana kwato moja.Mnyama wa kuliwa anatakiwa awe na kwato kama ya ngo'mbe au mbuzi
Elimu elimu elimu, rudi kasome kaka, japo huu uzi hauna mahusiano ma habari za dini lakini namwomba samahani mleta uzi kwa kuingiza vionjo vyenye uhusiano na dini.
Mkuu Tangantika, hebu nambie kifungu gani katika kitabu gani kimemzuia muislam asile Sungura na mr Kaambali?, maana nisolijua mimi yawezekana wenzangu mwalijua nifahamisheni.
 

Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,762
2,000
Elimu elimu elimu, rudi kasome kaka, japo huu uzi hauna mahusiano ma habari za dini lakini namwomba samahani mleta uzi kwa kuingiza vionjo vyenye uhusiano na dini.
Mkuu Tangantika, hebu nambie kifungu gani katika kitabu gani kimemzuia muislam asile Sungura na mr Kaambali?, maana nisolijua mimi yawezekana wenzangu mwalijua nifahamisheni.
Kwa nini huli nguruwe kama mwislamu ? Ukinjibu hilo ntakujibu swali lako maana sababu za kutomla nguruwe zinataka kufanana na za sungura.
 

Niite Profesa

Member
Jun 19, 2015
41
125
Feasibility study hasa upande wa masoko ni jambo la msingi sana kabla hujashawishiwa kuwekeza kwenye inayoitwa fursa.

Njia nyepesi ya kufanya hii study ni kujiuliza basic questions yafuatayo.

1. Je, wewe na familia yako ni walaji wa sungura?

2. If yes, mara ya mwisho umekula sungura lini?

3. Katika kipindi cha mwezi mmoja, unakula sungura mara ngapi kama kitoweo?

4. Jirani zako ninwalaji wa sungura?

5. Wanakula sungura kiasi gan kwa mwezi.

Mteja wa Kwanza wa bidhaa ni wewe na familia yako. Mteja wa pili ni majirani wanaokuzunguka.
Mteja wa watu ni ndugu wa karibu.

Ukishawamudu hawa nenda kwa wateja wa maduka na super markets.

Ukiona unashawishiwa kufanya biashara ambayo wewe na jirani zako sio wateja, usitegemee kupata wateja sokoni.

Swala la pili. Kuna dhana mbili za biashara za ufugaji kwa sasa, dhana ya kwanza na B2B..business to business....au biashara toka kwa mfugaji kwenda kwa mfugaji. Hii inalipa zaidi, na imejikita kwenye kuuza mbegu zaidi ili mwingine akafuge. Bidhaa zinazoangukia kwenye kundi hili ni ile mifugo inayofugwa kwaajili ya mapambo au isiyo na mzubguko mkubwa sana sokoni. Mfano bata mzinga, kanga, bukini, kware, hata sungura wanaangukia kwenye kundi hili.

Wengi wanaofanya biashara katika dhana hii, wamejikita kutangaza kuuza mbegu na kuhimiza ujasiriamali. Mf. Kuna mkulima anapromote zaidi kilimo cha papai, ila yeye biashara yake si kuuza papai bali kuuza miche. Shamban kwake hana papai hata moja analoweza peleka sokoni kwani anaelewa risks za kulima papai nyingi bila kuwa na mteja ..huaribika kirahisi.

Dhana ya pili ya biashara ya kilimo ni B2C..business to customers...(toka kwa mfugaji kwenda kwa mlaji)...hii ndio yenye demand kubwa zaidi, kwan bidhaa inayozalishwa hapa ni ile yenye demand sokoni kwa walaji. Mfano kuku wa kisasa/kienyeji. Mahindi, ,haya yanalika moja kwa moja na mteja.

Nachoweza washauri ndugu zangu ni kufanya feasibility kabla ya kuingia katika uwekezaji wa aina yoyote.

NB.
Maoni yangu yanalengo la kuelimisha na hayana uhusiano na hoja za mleta mada.
JF Sihami Maana kila siku najifunza kitu kipya🙏🙏🙏
 

FURY BORN

JF-Expert Member
Jul 11, 2020
460
1,000
Kuna mtu anasema alijikuta amekua master wa kuchinja, kuchuna na kula sungura baada ya soko kukaa tenge.
Kuna mmoja huko Kenya alichinja mpaka akachoka akaamua kwenda kuwatupa porini, lakini kila akiondoka wanamfuata.
Vitu vingine tutafakari jamani Hilo soko linaongelewa liko wapi? Kwa nchi za wenzetu Huko Sawa lakini bongo mtihani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom