Ufugaji wa sungura na njiwa wenye tija

Hii thread imenipa hamasa kubwa. Hapa na pakia na kupakua data nikianza ufugaji ni non stop. Wajuvi endeleeni kutupa ujuzi zaidi. Hongereni sana
 
siku moja nilikuwa naangalia citizen ya kenya walisema kwamba kilo moja ya nyama ya sungura inafika 8,000 kwa pesa za tz . wao walikuwa wanafuga sungura wanaoweza fikia kilo 10. pia walisema bei ya ngozi yake iko juu mno. walisema pia demand ya nyama inazidi supply. unaweza fuga na ukaenda mabucha kadhaa ya ng'ombe mkaelewana ukawa unauzia hapo nyama.
sungura kilo kumi mhhh huyo ni yule sungura wa sizitaki mbichi hizi wa kwenye kitabu cha enzi zile
 
Mama timmy

nina vitabu vidogo viwili raising and keeping rabbits part 1&2 ... nilipewa na mtu mmoja wa FAO telefood program .... maelezo yote from A to Z utayapata in very simple and understanding language

kama unahitaji do not hesitate to contact by pm ...

available free of charge
Naweza pata pia hivyo vitabu? Pia nahitaji jike na dume naweza pata?
 
Jamani ni member mpya kabisa, nawashukuru wote na uongozi kwa ujumla kuweza kuniruhusu kujiunga hapa, na pia nilikuwa natafuta sana taarifa za kufuga sungura na njiwa wa biashara yenye tija kwani napenda sana ujasiriamali na nikiwa mdogo nilifuga sana hawa sungura, njiwa.

Nimefurahi sana kupata taarifa kwa BLUETOOTH na msinichoke jamani ndio nataka kuanza ufugaji huu wa sungura. Naomba kama kuna mtu mwenye taarifa ya hawa njiwa wa kisasa nipate kujuwa ufafanuzi wake na bei zake, ulaji wake na soko lake.

Nawashukuruni sana jamani pamoja tutajenga taifa na pamoja tunaweza, pia naomba kama kuna mtu mwenye namba ya simu ya hawa SUA KITENGO CHA SUNGURA iili niweze kufanya order au kama kun mdau mwingine mwenye hiyo mbegu ya SUA tupeane number tuwasiliane mara moja.

Shukrani sana..
 
awwadau wote nashukuruni sana kwa taarifa za sungura na njiwa ila naomba bwana MOHAMED SHOSSI mimi naishi DAR sijui wewe uko wapi ningependa nipate mawasiliano yako ya karibu nimevutiwa sana na hao njiwamimi nina hoby sana na njiwa pia napenda nifuge kibiashara aks
 
Mama timmy labda tu nikueleze kwa ufupi
Kuhusu utunzaji wa watoto hiyo inategemea na aina ya Sungura.. sungura wa kienyeji (mara nyingi huwa wana mabaka) ni wavumilivu sana, huwa wanazaa watoto wengi na kuwatunza vizuri i.e anaweza asiue mtoto hata mmoja lakini hawa wakisasa kama wale weupe wenye macho mekundu (tuwaaita mchina) ni wasumbufu na wakizaa huwa hawawajali watoto wao .. anaweza kuzaa watoto 7 watano wakafa ndani ya wiki 1..

sungura anapenda sana kuishi sehemu isiyo na sakafu na yenye giza giza.. huwa wanachimba mashimo marefu sana na kuzaa humo humo.. watoto wakishaota manyoya anawatoa nje (njia hii ni hatari sana c'se wanaweza kuangusha nyumba)... kama una ardhi ndogo unawaweza kuwajengea mabanda ya mbao ya ghorofa yenye cuts nyingi halafu chini ukawekea udongo/maranda/pumba za mpunga iliwapate mazingira yao ya asili na joto vinginevyo wakizalia juu ya mbao au sakafu watoto ni lazima wafe

magonjwa: sijawahi kumuona sungura wangu aumwe lakini papasi huwa wanawapenda sana kwahiyo inakubidi uwe unapulizia dawa kwenye banda lao mara kwa mara au uwe unawapaka dawa ya unga (nzuri zaidi).. bila kusahau kuchoma moto yale madongo/pumba wanazolalilia baada ya wiki kadhaa
 
Hallo brother nimependa information yako kuhusu hao sungura, Kaka Mimi ninao wachache wa kienyeji sasa nitapataje wa kisasa maana wanasema wa kisasa huwa anafika mpaka kilo 9, kama unao Kaka mail yangu ni bmopia@yahoo.com
 
Habari wanajamii? Mimi ninafuga Sungura na Njiwa kwa kuwa nawapenda sana ila nafahamu kwamba nikipata elimu ya namna ya kuwafuga kitaalamu au kwa mtu mwenye uzoefu nao naomba anielekeze namna mabanda yao yajengwe na namna ya kufanya sungura wangu watunze watoto wao ili wasife.
Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa kuwahudumia wanyama waha, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura wanahitaji uangalizi na hassa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafuMABANDAKna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda wote bila kutoka nje na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza kutoka nje kwenye ua maalum, katika aina zote mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura.UFUGAJI WA NDANI1 - Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha2 - Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura hana uwezo wa kuzimeng'enya na kuisha mwilini mwake, siku ukimchinja atabakia na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa3 - Ukubwa wa banda usipungue mita 4 * 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa kubwa zaidi ni vizuri4 - Chini kuwekewe matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini maranda yatokanbayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi hayafai, wawekee kipande cha blanket au taulo la zamani kwa ajili ya kulalia na kujifungulia hasa kwa wazazi5 - Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara wanapohisi hatari, unaweza kutumia mbao, box gumu au plastikiUFUGAJI WA NJE1 - Sehemu yote izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama paka, mbwa, mwewe nk2 - Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwa ajili ya sungura kupumzika3 - Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali4 - Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuulia wadudu au mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu (waone wataalamu wakushauri au ng'oa yote)MAJITumia mabakuli ya kigae, plastiki au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku na vyombo visafishwe kila sikuCHAKULAWapewe majani, mabaki ya mboga za jikoni baada ya kuchambuliwa, pia unaweza kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers mash) kwenye vyombo maalum kama chakula chenye virutubisho (concentrates)USAFIKila siku jaribu kuondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika, na kinyesi kilichoganda kwenya matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau mara moja kwa wiki, manyoya ya sungura mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia kujifungua watotoMENOWakati mwingine meno ya mbele hukua sana na kumsababishia usumbufu wakati wa kula, waone wataalam ukiona ni marefu zaidi na yanahitaji kupunguzwa, dalili kuu ni sungura kushindwa kula kwa zaidi ya masaa 12MIGUUMiguu ya sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake zimefunikwa kwa manyoya, angalia ukiona yananyonyoka kuna tatizo chunguza, kucha zake nazi huhitaji kupunguzwa zikikua sanaUBEBAJIUsimbebe kwa kutumia masiki yake huwa wanaumia sana, shika ngozi nyuma ya shingo kama paka ukitaka kumbebaDAWAWapewe dawa ya minyoo kama piperazine kila baada ya miezi mitatu, dawa za wadudu kama akheri powdeer zinyunyuziwe kwenya mabanda yao kuzuia viroboto, usiwape dawa nyingine bila ushauri wa kitaalamu, antibiotics ndio usijaribu kabisa kama nilivyosema mwanzo
 
Ufugaji huu utakuwa na tija hapo baadae hapahapa Tanzania.Nimejifunza vitu vingi hapa,nilishawahi kufuga sungura na njiwa miaka ya nyuma sana na niliwafuga kwa hobbies tu na nilikuwa nawapenda sana kiasi kwamba sikuwahi kula hata nyama yao hadi leo sijui ladha ya njiwa wala sungura
 
Mama timmy

nina vitabu vidogo viwili raising and keeping rabbits part 1&2 ... nilipewa na mtu mmoja wa FAO telefood program .... maelezo yote from A to Z utayapata in very simple and understanding language

kama unahitaji do not hesitate to contact by pm ...

available free of charge
Habari ndgu mimi ntapataje ivo vitabu vya ufugaji wa sungura
 
Habari wanajamii? Mimi ninafuga Sungura na Njiwa kwa kuwa nawapenda sana ila nafahamu kwamba nikipata elimu ya namna ya kuwafuga kitaalamu au kwa mtu mwenye uzoefu nao naomba anielekeze namna mabanda yao yajengwe na namna ya kufanya sungura wangu watunze watoto wao ili wasife.
Habari dada jimekuja pm n
 
Habari wanajamii? Mimi ninafuga Sungura na Njiwa kwa kuwa nawapenda sana ila nafahamu kwamba nikipata elimu ya namna ya kuwafuga kitaalamu au kwa mtu mwenye uzoefu nao naomba anielekeze namna mabanda yao yajengwe na namna ya kufanya sungura wangu watunze watoto wao ili wasife.
Mama timmy nimkuja pm naomba unitafute.
Naamini utakuwa ushajifunza mengi mpaka sasa toka 2013 na upombali.
 
Njiwa unaofuga ni njiwa koko au species tofauti? Mimi nina njiwa wa kutoka nchi tofauti tofauti kama american fantail pigeons, nun pigeons, african owl pigeons, chinese owl pigeons, king pigeons na nun pigeons. Hawa nafuga kama hobby na biashara kwa kuwa pair moja inacost kati ya laki mbili mpaka laki saba. Kesho nitapost bandalangu la njiwa.



Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Habari kiongozi? Samahani hii post ni ya muda mrefu ila nahitaji kukutafuta. Ninauzoefu Wa kufuga njiwa koko kwa muda mrefu ila niliwaachia wadogo zangu wasiwajali wakatoroka. Sasa nimeanza tena japo nia yangu ni kufuga kama hao Wa kwako ili kupata uzoefu zaidi. Naomba nikutafute in box
 
Njiwa unaofuga ni njiwa koko au species tofauti? Mimi nina njiwa wa kutoka nchi tofauti tofauti kama american fantail pigeons, nun pigeons, african owl pigeons, chinese owl pigeons, king pigeons na nun pigeons. Hawa nafuga kama hobby na biashara kwa kuwa pair moja inacost kati ya laki mbili mpaka laki saba. Kesho nitapost bandalangu la njiwa.



Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Mkuu kwema ? Naomba upost picha za hao njiwa na majina
 
Back
Top Bottom