Ufugaji wa sungura na njiwa wenye tija

Mama timmy

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
656
209
Habari wanajamii?

Mimi ninafuga Sungura na Njiwa kwa kuwa nawapenda sana ila nafahamu kwamba nikipata elimu ya namna ya kuwafuga kitaalamu au kwa mtu mwenye uzoefu nao naomba anielekeze namna mabanda yao yajengwe na namna ya kufanya sungura wangu watunze watoto wao ili wasife.
 
Habari wanajamii?mimi ninafuga sungura na njiwa kwa kuwa nawapenda sana ila nafahamu kwamba nikipata elimu ya namna ya kuwa fugu kit salami au kwa mtu Mwenyezi useful nao naomba anielekeze namna mabanda Yao yajengwe na namna ya kufanya sungura wangu watunze watoto wao ili wasife.
Ni vyema pia ukatupa kaujuzi kidogo kwa namna ulipofikia katika ufugaji hususani kwa Sungura, kwa mfano;

1/Sungura huwa wanakula vyakula gani?

2/Wanazaana kwa mpango upi?

3/Ukuaji wa sungura ukoje(Toka anazaliwa mpaka anakuwa mkubwa anachukua muda gani?)

4/Soko lao kibiashara likoje kama utataka kufuga ili uuze(Bei, soko nk)
 
Kwa kweli sungura wanazaliana sana kwani sungura anazaa kuanzia watoto Sita mpaka kumi na mbili.wanakula majani hasa mchunga majani ya kabichi,mboga zote za majani wanakula.pia wanakula maganda ya viazi na pumba za mahindi.sungura wanakua haraka sana .sungura wanatofautiana ukubwa kutokana na mbegu.kuhusu soko sijafanya utafiti ila kwa namna watu wanavyokuja hapa home na kutaka niwauzie sungura naamini soko lipo vzr,na hii ndiyo sababu kubwa ya kuomba ushauri hapa.ninaomba kwa mwenye utaalamu juu ya sungura hasa mabanda Yao na magonjwa na dawa zao
 
Bado ninahangaika kupata elimu sahihi juu ya hawa sungura na njiwa.kama kuna mtu anaufahamu nao hata kidogo naomba anisaidie.
 
Mama timmy

nina vitabu vidogo viwili raising and keeping rabbits part 1&2 ... nilipewa na mtu mmoja wa FAO telefood program .... maelezo yote from A to Z utayapata in very simple and understanding language

kama unahitaji do not hesitate to contact by pm ...

available free of charge
 
Last edited by a moderator:
Mama timmy labda tu nikueleze kwa ufupi
Kuhusu utunzaji wa watoto hiyo inategemea na aina ya Sungura.. sungura wa kienyeji (mara nyingi huwa wana mabaka) ni wavumilivu sana, huwa wanazaa watoto wengi na kuwatunza vizuri i.e anaweza asiue mtoto hata mmoja lakini hawa wakisasa kama wale weupe wenye macho mekundu (tuwaaita mchina) ni wasumbufu na wakizaa huwa hawawajali watoto wao .. anaweza kuzaa watoto 7 watano wakafa ndani ya wiki 1..

sungura anapenda sana kuishi sehemu isiyo na sakafu na yenye giza giza.. huwa wanachimba mashimo marefu sana na kuzaa humo humo.. watoto wakishaota manyoya anawatoa nje (njia hii ni hatari sana c'se wanaweza kuangusha nyumba)... kama una ardhi ndogo unawaweza kuwajengea mabanda ya mbao ya ghorofa yenye cuts nyingi halafu chini ukawekea udongo/maranda/pumba za mpunga iliwapate mazingira yao ya asili na joto vinginevyo wakizalia juu ya mbao au sakafu watoto ni lazima wafe

magonjwa: sijawahi kumuona sungura wangu aumwe lakini papasi huwa wanawapenda sana kwahiyo inakubidi uwe unapulizia dawa kwenye banda lao mara kwa mara au uwe unawapaka dawa ya unga (nzuri zaidi).. bila kusahau kuchoma moto yale madongo/pumba wanazolalilia baada ya wiki kadhaa
 
available free of charge[/QUOT
 
Narubongo nashukuru sana kwa maelezo yako.je sungura wako ni wa kienyeji au wakisasa?na vp naweza kupata mbegu kubwa kwako?
 
Njiwa unaofuga ni njiwa koko au species tofauti? Mimi nina njiwa wa kutoka nchi tofauti tofauti kama american fantail pigeons, nun pigeons, african owl pigeons, chinese owl pigeons, king pigeons na nun pigeons. Hawa nafuga kama hobby na biashara kwa kuwa pair moja inacost kati ya laki mbili mpaka laki saba. Kesho nitapost bandalangu la njiwa.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Mama timmy labda tu nikueleze kwa ufupi
Kuhusu utunzaji wa watoto hiyo inategemea na aina ya Sungura.. sungura wa kienyeji (mara nyingi huwa wana mabaka) ni wavumilivu sana, huwa wanazaa watoto wengi na kuwatunza vizuri i.e anaweza asiue mtoto hata mmoja lakini hawa wakisasa kama wale weupe wenye macho mekundu (tuwaaita mchina) ni wasumbufu na wakizaa huwa hawawajali watoto wao .. anaweza kuzaa watoto 7 watano wakafa ndani ya wiki 1..

sungura anapenda sana kuishi sehemu isiyo na sakafu na yenye giza giza.. huwa wanachimba mashimo marefu sana na kuzaa humo humo.. watoto wakishaota manyoya anawatoa nje (njia hii ni hatari sana c'se wanaweza kuangusha nyumba)... kama una ardhi ndogo unawaweza kuwajengea mabanda ya mbao ya ghorofa yenye cuts nyingi halafu chini ukawekea udongo/maranda/pumba za mpunga iliwapate mazingira yao ya asili na joto vinginevyo wakizalia juu ya mbao au sakafu watoto ni lazima wafe

magonjwa: sijawahi kumuona sungura wangu aumwe lakini papasi huwa wanawapenda sana kwahiyo inakubidi uwe unapulizia dawa kwenye banda lao mara kwa mara au uwe unawapaka dawa ya unga (nzuri zaidi).. bila kusahau kuchoma moto yale madongo/pumba wanazolalilia baada ya wiki kadhaa
Sungura huliwa sana Misri hupimwa kwa kilo wakiwa hai,huuzwa kama kuku sokoni,unaweza ukanunua watatu wakapimwa kwenye mzani na wakachinjwa hapo hapo ,kisha ukaweka kwenye rambo tayari kwa kupika ,wao hudai ni white meat,eti nyama yao ni kama ya kuku,da mie siwezi kula sungura nawaona kama paka vile
 
Kumbe Misri wanakula sungura, nilisikia kuwa hawali wanyama wenye kucha na kwamba ni haram.
 
most arabs wanapenda na wanatumia sana nyama ya sungura .... hapa Dar nyama hii inapatikana sehemu inaitwa oceanic resort ipo mbweni ... wanatengeneza vizuri sana yaani inachomwa na moto wa mbali grilled .... whole rabbit anauzwa Tsh 32,000
 
Njiwa unaofuga ni njiwa koko au species tofauti? Mimi nina njiwa wa kutoka nchi tofauti tofauti kama american fantail pigeons, nun pigeons, african owl pigeons, chinese owl pigeons, king pigeons na nun pigeons. Hawa nafuga kama hobby na biashara kwa kuwa pair moja inacost kati ya laki mbili mpaka laki saba. Kesho nitapost bandalangu la njiwa.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Njiwa nilionao ni wa kawaida na pea mbili za njiwa tausi.naomba utakapopost picha za Banda Lako uweke na picha za hao njiwa waziri ulionao kaka yangu
 
Narubongo naomba uniambie Kama unasungura mbegu kubwa au Kama kuna yeyote mwenye sungura mbegu kubwa anifahamishe ndugu zangu.
 
Njiwa nilionao ni wa kawaida na pea mbili za njiwa tausi.naomba utakapopost picha za Banda Lako uweke na picha za hao njiwa waziri ulionao kaka yangu

Hao ni baadhi ya njiwa na banda nililonalo nyumbani
 
Attachments

  • 756px-Crested_helmet_pigeon.jpg
    756px-Crested_helmet_pigeon.jpg
    70 KB · Views: 1,782
  • ChineseOwl01146.jpg
    ChineseOwl01146.jpg
    13.8 KB · Views: 1,447
  • Dar es Salaam-20121215-00062.jpg
    Dar es Salaam-20121215-00062.jpg
    34.4 KB · Views: 1,810
  • Dar es Salaam-20121219-00616.jpg
    Dar es Salaam-20121219-00616.jpg
    619.8 KB · Views: 2,614
  • Dar es Salaam-20121227-00670.jpg
    Dar es Salaam-20121227-00670.jpg
    167.5 KB · Views: 1,745
  • Jacobin Pigeon 8.jpg
    Jacobin Pigeon 8.jpg
    20.4 KB · Views: 1,329
Back
Top Bottom