Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
5,149
4,674
Wana JF

Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vya maji ya asili ikiwemo mito, mabwawa, maziwa, bahari, chemchem nk. Kutokana na vyanzo hivi tunapata samaki wa aina mbalimbali wakiwemo perege/sato, kambale, kambamiti (prawns), vibua, changu, kaa n.k.

Samaki ni chanzo cha lishe, kipato na ajira, tunaweza tukatengeneza vito kutokana na lulu wa chaza. Nimejaribu kuzungukia katika soko letu la fery pale nikagundua akina mama na wadau wengi wanafaidika sana na biashara ya samaki nadhani tunawaona mitaani kwetu lakini wanalalamika bei imekuwa juu na upatikanaji wake ni wa shida sana kulingana na msimu.

Nilijaribu kufuatilia kwa undani suala hili kwa wizara husika nikaelezwa ni kweli bei ya samaki iko juu na upatikanaji wake ni mgumu kutokana na samaki wamepungua kwa kiasi kikubwa na wanapungua kwa kasi ya ajabu...Hali hii inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, nguvu kubwa ya uvuvi iliyopo kwa mfano samaki sangara kutoka ziwa victoria wamepungua sana na wanaopatikana kwa sasa ni wadogo. Pia wizara ililazimika kufunga uvuvi wa prawns kwa meli kubwa kubwa kutokana na hali kuwa mbaya. Hata perege wanaopatikana ni wadogo na kwa uchache.

Ili kuokoa suala hili, njia pekee ni kuhamasisha UFUGAJI WA SAMAKI kwa ajili ya kipato, ajira na chakula. Nimevutiwa na suala hili nikaona niwashirikishe wana JF. Nchi za asia china, ufilipino, japan, indonesia fani hii imekuwa sana na wananchi wanajikwamua kiuchumi kutokana na ufugaji wa samaki.

Bado ninafanya ufuatiliaji wa karibu kuhusu suala hili la ufugaji samaki na jinsi tunavyoweza kufaidika nalo. Ninaamini tunaweza kufuga na kupata faida kubwa pia tukatunza mazingira yetu ya asili.

Wakati naendelea kufuatilia suala hili naomba mwenye taarifa basi tushirikiane hapa JF. Nitarudi tena kwa maada hii mara nitakapokusanya taarifa ndani ya siku chache.

Nawasilisha kwa michango yenu.

Nteko Vano Maputo

Penye nia pana njia

Uvuvi%2Bbusega%2B4.jpg

Tujifunze kuhusu ufugaji wa samaki wa kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vitu vingine vinavofanana na hivyo.

Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)

Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling(vifaranga) sehemu nyingine.

Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea na cement,kutandika plastic au kuchimba na kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/gradient)

Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African catfish) na wengine aina ya pangasius ambao hufugwa kwa wingi sana.
Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa.

Ukishachimba bwawa lako(aidha na kulijengea) unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi 2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming(kumwagia chokaa bwawa kabla ya kuweka maji ili kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji kwa kuchanganya na mbolea(kama ya ng'ombe na za viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi ili kuweka mazingira ya chakula asili(natural foood) kwa ajili ya samaki kujitengeneza,vyakula hivo hua katika hali ya mimea na viumbe wadogo(microorganisms)

Upatikanaji wa vifaranga vya samaki,hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua kuzalisha sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo under right conditions vifaranga vitaweza kua samaki wenye uzito wa kutosha(miezi 6 awe at least 500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana kwa bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa kifaranga kimoja.Wapo wazalishaji wengi wa mbegu za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research Institute(TAFIRI) Nyegezi,Mwanza(Nimefwatilia performance yao shambani).



Ulishaji wa vifaranga vyako ,chakula chao kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha ziada(supplement food),sababu cha asili amekipata kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100 vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50 kuwalisha.

Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au njia utayoona inakufaa.Samaki wengi wa kwenye mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au kumwaga maji yote nje ya bwawa.Masoko yake haya samaki ni pamoja na supermarkets, wafanyabiashara sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.

N:B
Wataalam wapo wengi humu naomba muongeze na mambo mengine niliyoyasahau au kuyakosea.

Ufugaji wa mabwawa umepitwa na wakati,sasa ufugaji wa samaki ni AQUAPHONIC hii ndio mwisho miezi minne tu una sato wa nusu kilo.just google aquaphonic and learn for your self.

Kwa watakaopenda kuona how Aquaphonic work.siku nzuri ni weekend so Mtam na wengine wote interested tuwasiliane ijumaa ili tupange kama iwe jumamos au jumapili mje muone.

Bagamoyo Pale Chuoni wana mambwawa ya kawaida na wanauza Vitoto vya sato shillingi 50 kimoja. Kambale pia wapo. Kama kuna anayependa kwenda pale Bagamoyo Mbegani for study tour pia twaweza kupanga ila wao wanatembelewa working days tu.so inabidi iwe kati ya jumatatu to ijumaa working hrs.sisi vitoto vya kuanzia tulinunua Bagamoyo,lakini katika vitoto hivyo tutapata wazazi wa mbegu siku zijazo.

Katika ufugaji wa samaki kuna vitu muhimu vya kuzingatia.Samaki wanaokuwa kwa haraka ni Madume.Je utapataje Madume watoto? Ipo Dawa ambayo unaiweka katika chakula cha samaki watoto,baada ya muda 99% ya hawa watoto samaki wanageuka Madume.Kisha wewe unaendelea kuwalisha kama kawaida.

Samaki anaweza kula mchanganyiko wa chakula cha kuku lakini awezi pata virutubisho vyote kwani vingine vitapotea katika maji.
Hili pia ni tatizo kubwa hapa kwetu Tanzania juu ya ulishaji samaki ili wakue haraka. Samaki ili wakue haraka na kwa faida ya mfugaji chakula chake kinatakiwa kiwe katika mfumo wa pallets (kama vigololi vidogo size ya ulezi,mtama au zaidi) hii inamfanya samaki akila chakula katika mfumo wa pallets kumeza all food contents (minerals,protein,starch etc).

Mashine zipo za kutengeneza fish food,nikipata muda wakati nikiwa na PC ntaweza weka some docs za fish food,fish sex convention (how to do it),Aquaphonic and modern fish keeping ,nna docs nyingi sana za haya maswala but at this time nipo Mobile so siwezi attach kwa sasa

UFUGAJI WA SAMAKI

Tasnia ya ufugaji wa samaki inajumuisha ukuzaji wa viumbe vya kwenye maji (bahari na maji baridi) katika mazingira tofauti na yale ya asili. Lengo kuu ni kukuza kwa muda mfupi ili kujipatia lishe, kipato na kutunza mazingira ya bahari, mito, maziwa nk.
Ufugaji unagusa viumbe vya kwenye maji kuanzia mimea kama vile mwani, samaki wasio na mapezi (kaa-crabs, kambamiti-prawns, chaza-oyster, majongoo bahari nk) na samaki wenye mapezi (perege/sato, kambale, kibua, trout, chewa nk).

Aina ya ufugaji

Zifuatazo ni aina/level za ufugaji ambazo mkulima anaweza kufanya kulingana na malengo na uwezo wake:

1. Huria (Extensive farming)

Idadi ya samaki wanaopandikizwa: samaki 2-3 kwa mita ya mraba
Samaki hutegemea chakula cha asili (mimea ya majini-phytoplankton, wadudu/viumbe vidogo vya majini-zooplankton)
Hauitaji ubadilishaji wa maji
Hauihitaji huduma ya ziada ya hewa

2. Kati ya huria na nusu shadidi (Modified extensive)  Idadi ya samaki, 4-7 kwa mita ya mraba

Chakula cha asili na chakula cha ziada huitajika
Maji hubadilishwa sentimenta 10-20 kila baada ya 3-4weeks kulingana na hali ya samaki na maji yako
Huduma ya hewa ya ziada sio ya ulazima

3. Nusu shadidi (Semi-intensive)

Idadi ya samaki kwa mita ya mraba ni 10-25
Chakula cha asili na cha ziada
Huduma ya hewa ya ziada lazima
Maji hubadilishwa kila siku au kila baada ya siku kadhaa (15-25 cm)

4. Shadidi (Intensive)

Idadi ya samaki ni zaidi ya 25 kwa mita ya mraba
100% chakula cha kutengenezwa
Maji ni kuingia na kutoka
Hewa ya ziada masaa yote
Eneo linalotumika ni dogo ukilinganisha na mifumo mingine

Miundombinu ya ufugaji

Samaki wanaweza kufugwa katika miundombinu mbalimbali kama ifuatayo:

Bwawa
Kina 0.8-1.5m
Ukubwa 100 mita za mraba- 1ha

Matanki

Umbo-mstatili au mviringo nk
Kina 1-1.5m
Kipenyo kwa lile la mduara 3-10m
Ukubwa kwa la mstatili inategemea na uwezo lakini lisiwe kubwa ili kuhimili nguvu ya maji
Materials: Plastic, cement, chuma nk
NB: Simtank linafaa( Faida inapatikana kama utalitumia kwa intensive system)

Vizimba (Fish cages)
Huwekwa katika maji ya asili kama vile ziwani, baharini au katika bwawa. Vipo vinavyoundwa kwa local materials kama mianzi na vipo vya aluminium.

Eneo linalofaa kwa ufugaji

Baadhi ya maeneo yanayofaa ni yale mashamba ya mpunga, na maeneo yaliyo karibu na vyanzo vya maji. Zifuatazo ni sifa za maeneo yanayofaa:

1. Udongo: Mfinyanzi husaidia kupunguza gharama za ujenzi wa bwawa na maji kwakuwa linaweza kutuamisha maji na kuruhusu maji yasipotee. Likiwa la kichanga bwawa ni lazima lijengewe au kuwekwa nylon sheet ili kuzuia upotevu wa maji. Unaweza ukahamisha udongo wa mfinyanzi kutoka sehemu moja hadi nyingine ili kuzuia upotevu wa maji (muone mtaalamu kwa ushauri zaidi juu ya mbinu ya kuhamisha udongo).

2. Chanzo cha maji ya uhakika
Eneo liwe na maji ya uhakika. Vyanzo vya maji ni kama vile mito, bahai, maziwa, chem chem., kisima, maji ya dawasco na mvua. Maji yasiwe na kemikali hatarishi kwa viumbe.

3. Miundombinu ya barabara: Inasaidia kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa na samaki wakati wa kuvuna.
4. Eneo lisiwe na historia ya mafuriko ili kuzuia athari za mafuriko kwa miundombinu yako. Utatumia gharama nyingi katika kuimarisha miundombinu yako.Jamii/aina ya samaki
5. Eneo lenye mwinuko wa wastani husaidia katika ujenzi wa bwawa.
6. Miundombinu ya umeme ni sifa ya ziada hususan kwa mkulima wa kati na wajuu kwa ajili ya kutumika katika kuendesha visambaza hewa.
7. Ulinzi muhimu

Note: Aina ya eneo lako ndilo linaweza kukufanya uchague muundombinu gani wa kufugia utumie

Aina ya samaki unaoweza kufuga Tanzania kwa sasa
Maji baridi

Sato/perege, Kambale, Kambamiti wa maji baridi na Trout (maeneo ya baridi kama vile Iringa, Kilimanjaro Arusha na Mbeya) na samaki wa mapambo.

Maji bahari

Kambamiti wa maji bahari, mwatiko, chewa, kaa, chaza wa lulu

Upatikanaji wa Vifaranga vya samaki husika

Vyanzo vya vifaranga ni kutoka katika mito, bahari, maziwa na wale wa kuzalishwa katika vituo vya kuzalishia vifaranga.

Sato na Kambale

Vituo vya serikali Utapata sato wa kike na kiume mixed sex). Kingolwira Morogoro, LuhiraSongea, Mbegani-Bagamoyo . Kifaranga huuzwa Tsh. 50-100 kwa kifaranga.

Vituo binafsi kama vile Faith aquaculture-Kibamba (DSM) (utapata monosex sato), PeramihoSongea (mixed sex). Monosex huuzwa Tsh. 200 kwa kifaranga, na mixed ni 100 kwa kifaranga.

Trout

Mayai huagizwa toka Marekani, Israel
Kambamiti wa baharini Alphakrust Mafia.

Chakula cha samaki

Chakula cha asili

Hurutubishwa kwa mbolea ya wanyama kama vile kuku, ngombe, mbuzi nk. Kwa kiwango cha 1000kg/ha. Mbolea ya kuku ni kali hivyo unaweza punguza ikawa 250-500kg/ha.

Chakula cha kutengeneza

Samaki huitaji protein ili akuwe na kila samaki ana mahitaji yake hivyo ni species specific. Formula zipo kwa wale wanaotaka kutengeneza. Tanzania hakuna kiwanda kinachotengeneza. Ingredients zake ni kama vile dagaa, pumba, soya, unga wa ngano, unga wa muhongo nk.

Uvunaji

Kwa kawaida ni miezi 4-6 amabapo unapata 250-400g kulingana na ulishaji wako. Kwa prawns ni miezi 3-6 wanafikia 30-50g ambayo ni ukubwa wa soko.

Tathmini ya uchumi

Perege/sato Mfano:

Ukubwa wa bwawa ni 20m by 30m= 600 mita za mraba
Idadi ya samaki (7 kwa mita ya mraba) kwa monosex tu= 600 x 7=4200 fish
Uzito hadi kuvuna (4-6months)- 250g= 4200 x 250g= 1050kg (Nimesha convert gram to kg) Bei kwa kilo ni 6000-8000 kulingana na mahali= 6milion-8milion.

Gharama unazoweza kutumia
Ujenzi wa bwawa
Kuchimba kwa vibarua ni 500,000-600,000
Kuchimba kwa machine ni 1,000,000-1,500,000 kulinganana mahali ulipo

Kama udongo ni kichanga itabidi ujengee (kujengea ni gharama na inaweza ikafika 3.5-4m kwa gharama zote kuanzia kuchimba hadi kujengea).

Chakula cha kutengeneza tani 1 inaweza kugharimu laki 7-9. Hapa ili uweze kuzalisha tani 1 ya samaki aina ya perege utahitaji tani 1-1.5 ya chakula.
Gharama ya vibarua 150,000-250,000 kwa mwezi.
Utakuwa na gharama ya chokaa kwa ajili ya kuua vidudu (laki 100,000-200,000), mbolea kuzalisha chakula cha asili (gharama ni 50,000).

Jinsi ya kuhudumia bwawa, kuandaa chakula nitaandaa tips zingine.
Ha Muji

[2/15, 3:51 PM] Martin Mhina: Somo la kwanza ufugaji samaki

1.Mambo yakuzingatia wakati wakuchagua eneo kwaajili ya ufugaji samaki.

I. Aina ya udogo: hili nijambo muhimu kwani aina ya udogo huathiri kwenye kuchagua aina gani ya bwawa litumike. Tambua kuwa kuna aina nyingi ya mabwawa kama bwawa la udogo tupu (earthen pond) na bwawa la zege (concrete pond). Bwawa la zege hutumia gharama nyingi kulijenga ukilinganisha na bwawa la udogo tu. Hivyo ili bwawa liwe la udogo ni lazima aina ya udogo wa eneo husika uwe na sifa ya kutunza maji.

II. Maji: samaki huishi kwenye maji hivyo nilazima uwahakikishie upatikanaji wa maji safi na salama kwa uhai wao. Maji yawe yanapatika kwa Wingi, Salama na yenye kuweza kuwekwa katika miundombinu sahihi kwaajili ya kutumika wakati wowote. Maji yanaweza kuwa ya kisima, mto, ziwa, chemchem,au bomba. Kila aina ya maji ina faida zake na changamoto zake. Kwa mfano wakati maji ya mto huwa yanaweza kupatikana kwa urahisi lakin yanachangamoto yakuweza kukuletea vijidudu vya magonjwa kama minyoo, typhoid na kipindupindu.

III. Vifaranga: usishangae! Ndiyo mbegu za samaki yaani samaki wadogo huitwa vifaranga. Nilazima ujihakikishie upatikanaji wa mbegu bora kwaajili ya matokeo mazuri. Mbegu duni huchukua muda mwingi kukuwa na hivyo kumuongezea mkulima gharama za ufugaji na kumpunguzia kipato.

IV. Chakula: ufugaji wa samaki kwaajili ya biashara humuitaji mkulima kuwapatia samaki chakula za ziada (supplementary feed) ili samaki wakue kwa haraka zaidi. Kumbuka ukuwaji wa samaki hutegemea UBORA WA MAJI + UBORA WA CHAKULA.

V. Ulinzi na usalama: ni vyema mkulima kuepukana na migogoro yeyote kama ya umiliki wa ardhi na matumizi ya maji ili kuondoa uwezekano kukuhujimiwa katika mradi wake.

VI. Usafiri: kwa nyakati tofauti mkulima atahitajika kusafirisha ima malighafi zitumikazo kwenye ufugaji au mazao ya ufugaji baada ya kuvuna. Hivyo ni muhimu kuzingatia uwezekano wa usafiri sahihi wakati wote. Usafiri siyo mtu awe na gari hapana ila uwepo wa miundombinu safi yaweza tosha.

VII.Soko: Mwisho wa ufugaji ni kuuza mazao yako kwa faida hivyo ni vyema mkulima akafanya tafiti za kupata soko la uhakika kwa mazao yake. Mkulima huweza tumia soko la karibu kama majirani na wafanyabiashara wa karibu. Pia anaweza kutumia soko la mbali.

Ufugaji wa samaki unalipa endapo tu mkulima atapata mtaalamu sahihi na akazingatia kanuni za ufugaji.

Tukutane siku nyingne UFUGAJI KWA MAENDELEO BY MARTIN MHINA

2. KWANINI NIFUGE SAMAKI WAKATI KUKU WA KISASA WANACHUKUA MUDA MFUPI ZAIDI NA WANALIPA?

Ni kweli kama tutalinganisha ufugaji wa kuku wa kisasa na ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku wa kisasa unalipa zaidi kwakuzingatia kuku wa kisasa wanachukua takriban wiki 6 mpaka kuingia sokoni ukilinganisha na samaki ambao wanatumia takriban miezi 6.

Ila ulinganishi huu hatokuwa sahihi sana kwasababu zifuatazo

I. Kuku wa "kisasa" ni Genetically Modified Organisms(G.M.O) yaani viumbe ambao mpangilio wao wa asili wa vinasaba (genes) umebadilishwa kulingana na mahitajio mahususi. Viumbe hawa (GMO) huwa na sifa nying nzuri kama kukua haraka, ustaamili mazingira magumu zaidi kuliko asili yao na mengne. Lakin pia huweza kuwa na changamoto mbali mbali kama kushambuliwa na magonjwa kwa urahisi kama ilivyo kwa kuku wa kisasa ambao huhitaji mfuatano wa dawa kibao ili kuwawezesha kuishi. Madawa ambayo mengine yanamadhara makubwa kwa mraji wa kuku.

Tukirudi katika mazingira ya kawaida natumai wengi tunajua kuwa kuku wa kienyeji anahitaji takriban miezi 7 mpaka aweze kuliwa. Kinyume na hivyo samaki wanaofugwa na wafugaji wa kitanzania ni samaki wa asili yaani siyo GMO hvyo hawasumburiwi na changamoto kama za GMO wa kuku.

II. Soko la walaji kwasasa linapendelea chakula safi na salama chakula ambacho ukila hauhitaji kutumia madawa bali chenyewe ni chakula na pia ni tiba. Jambo hili linalazimisha walaji kuogopa kutumia GMO kama kitoweo. Jambo hili linafanya ufugaji wa samaki uwe na soko lisilo na matabaka ukilinganisha na ufugaji wa kuku wa kisasa.

III. Katika gharama za ufugaji samaki wanauwezo mkubwa sana wakukibadilisha chakula duni kuwa virutubisho vya mwili wao. Jambo hili kitaalamu linajulikana kama FOOD CONVENTION RATIO (FCR) ambayo nikipimo cha kiasi cha chakula alichokula kiumbe ukilinganisha na ukuwaji (irreversible increase in body weight and size) ambao hupimwa kwa urefu na/au uzito.

Baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa samaki ana FCR ya 1:1 na kuku ana FCR ya 2.5:1 yaani samaki anauwezo wakula kilo 1 ya chakula na kuongezeka kilo 1 ya uzito (ukuwaji) na kuku anahitaji kilo 2na nusu za chakula ili aongezeke kilo 1ya uzito (ukuwaji). Hvyo mfugaji wa samaki atatumia chakula kidogo zaidi kumnenepesha samaki ukilinganisha na mfugaji wa kuku. Jambo hili huleta athari kwenye biashara ya kuku kwa kufanya uwiano wa faida na gharama za ufugaji kuwa chini ukikinganisha na biashara ya samaki.

Kwa mfano mfugaji kuku anaweza fuga kuku kwa wiki sita akatumia 1,500,000 kuwakiza na baada ya mauzo akapata 4,320,000. Faida ni 2,820,000 Uwiano. Wakati huo mfugaji wa samaki anaweza tumia 750,000 kukuzia samaki na akawauza kwa 3,790,000. Faida ikawa 3,040,000.
Ukilinganisha mradi upi umerejesha uwiano mkubwa wa faida utakuta ufugaji samaki unalipa zaidi.

Sababu ni nyingi lakn mwisho wa siku mfanyabiashara huchagua biashara ambayo anaona anaweza imudu na itamletea faida zaidi.

Tukutane tena wakati mwingine By Martin Mhina

3. JE UMRI WA VIFARANGA (MBEGU ZA SAMAKI ) UNAMCHANGO WOWOTE KWENYE MATOKEO YA UFUGAJI WA SAMAKI WAKO?

Vifaranga vya samaki vimegawanyika katika aina kuu mbili kulingana na hatua ya makuzi. Hatua ya mwanzo tu wakizaliwa kitaalamu huitwa "fry" na hatua ya pili huitwa "fingerlings".

FRY ni vifaranga wadogo mno na wanakuwa na umri wa kati ya wiki 1mpaka wiki 4. Na wanakuwa na uzito wa chini ya 5gram.

FINGERLINGS ni vifaranga wakubwa na wanakuwa na umri wa kati ya wiki 4 na wiki 8. Na wanakuwa na uzito wa kati ya 5gram na 15gram.

JE KUNA FAIDA IPI YA KUNUNUA FRY AU FINGERLINGS?

Vifaranga vya FRY nirahisi sana kushambuliwa na kiumbe yeyote mualibifu kama ataingia kwenye bwawa kwa mfano chura. Pia nirahisi kudhurika kama litatokea tatizo lolote wakati wa kuwa safirisha. Faida yake kubwa huwa wana matumizi madogo ya oxygen wakati wakusafirishwa na huwa hawatoi taka nyingi (excretory wastes).

Kwa upande mwingine vifaranga vya hatua ya FINGERLINGS huwa na uwezo mkubwa wa kujilinda na kumudu changamoto za kimazingira japokuwa wanamatumizi makubwa ya oxygen na hutoa takanyingi ukilinganisha na vifaranga vya hatua ya FRY.

Mfugaji atakayenunua vifaranga vya hatua ya FINGERLINGS atapata faida ya mwezi mmoja wa ziada ambao vifaranga vilikuwa vimelelewa kabla ya kuwanunua. Hivyo kama atawafuga kwa miezi sita vifaranga wake watakuwa na ziada ya mwezi mmoja ambao huchangia katika ukubwa wa samaki. Kwani samaki wa miezi sita na miezi saba hutofautiana katika uzito. Hivyo kumfanya mfugaji auze kwa bei nzuri na kupata faida kubwa.

Kwahyo jibu ni NDYO umri wa vifaranga unachangia katika kukupa matokeo mazuri ya ufugaji.

Tukutane tena siku nyingne By Martin Mhina

4. JE SAMAKI WANAUGUA MAGONJWA? NA NINI TIBA YAKE?
Naam! Samaki huugua magonjwa mbali mbali kama minyoo, fungus na kupatwa na chawa. Pia samaki wanaweza kubebe vimelea vya magonjwa kama typhoid na kipindupindu.

Ila tutazame magonjwa ya samaki katika namna ya chanzo cha ugonjwa. Kuna magonjwa ambayo yanatokana na chanzo maalum "point-source diseases" na kuna magonjwa ambayo hayana chanzo maalum "non-point-source diseases".
Magonjwa yenye chanzo maalum mara nyingi husababishwa na maji hususani maji ya mito. Kundi hili hujumuisha magonjwa kama minyoo, chawa, typhoid na kipindupindu.

MINYOO- Humuathiri samaki katika ukuwaji wake lakin sirahisi kwa mkulima kujua kama samaki wake wanaminyoo. Minyoo hujakubainika pindi samaki wanapokuwa wameshakomaa na umewavuna. Wakati wakuwaandaa samaki ndipo unapokuta minyoo mingi tumboni! Hii hali ikijitokeza lazima ukuondolee soko la samaki wako kwakiasi kikubwa. Kwani samaki mwenye minyoo licha yakuleta picha mbaya lakin asipo pikwa vizuri minyoo huweza kuhamia kwa mlaji.

CHAWA- Athari ya chawa kwenye bwawa mara nyingi huonekana kwa samaki wakubwa lakini inadhuru samaki wote. Ikitokea samaki wamekubwa na chawa utawaona wanarukaruka kwenye maji na kujipiga piga mpaka kufa kutokana na majeraha na kuchoka.

TYPHOID na KIPINDUPINDU- Haya humuathiri mlaji wa samaki kama samaki hawataandaliwa vizuri. Na madhara yake yanafahamika kwa binadamu inakuwaje mtu akipatwa na kipindu pindu au typhoid.

CHANZO CHA MAGONJWA HAYA HUWA NI KINYESI CHA MWANADAMU AMBACHO HUSABABISHWA NA WATU KUJISAIDI KWENYE VYANZO VYA MAJI. WAKATI MWINGINE HUSABABISHWA NA KINYESI CHA KUKU AU NG'OMBE KAMA MIFUGO HIYO ILIKUWA IMEATHIRIWA NA MAGONJWA HAYO.

Magonjwa yasiyo na chanzo maalum ni kama Fungus.
FUNGUS ni saprophytic feeders yaani wanakila vitu vilivyokifa au oza. Kwahyo ikitokea kwenye bwawa kuna mazingira yakuruhusu waokustawi basi humshambulia samaki na maranyingi samaki huyu huwa na vidonda au majera yanayoonekana kwenye kiwiliwili cha samaki. Na jambo hili huondoa mvuto wa samaki kwa mteja.

Orodha ya magonjwa kwakusema tujifunze tu ni ndefu mno LAKINI NI MARA CHACHE SANA KUKUTA SAMAKI KAUGUA YEYOTE KATI YA MAGONJWA HAYA KWA MKULIMA ALIYEPATA USHAURI SAHIHI NA AKAZINGATIA TARATIBU.

TIBA za magonjwa zipo za aina nyingi lakin inashauriwa kwa mfugaji kuchukua tahadhari wakati wa mwanzo wa mradi na wakati wautekelezaji ikikuepukana na mlipuko wa magonjwa katika bwawa kwani ugonjwa ukishaingia kwenye bwawa inahitaji umakini wa hali ya juu ili kuuondoa kabisa.

Naomba tutosheke na machache haya mpak wakati mwingne tena kwenye KARIBUNI TUFUGE KIBIASHARA By Martin Mhina

5. JE NAWEZAJE KUJUA IDADI YA SAMAKI WAKUWEKA KWENYE BWAWA LANGU?

Ni muhimu sana kwa mfugaji samaki kuweza kujua idadi sahihi ya vifaranga ambavyo anaweza kuweka kwenye bwawa lake kwaajili ya kupata matokeo mazuri kabisa kwenye bwawa lake (optimization of the pond productivity). Japokuwa kumekuwa na nadhari mbalimbali zinazoelezea idadi ya vifaranga vya kuweza kuwekwa kwenye bwawa (stocking density) nitajaribu kuelezea namna moja wapo ambayo nimeiona kuwa inafaa.

Kwanza tutambue mambo ambayo yanayokupelekea kwa mabwawa mawili yenye ukubwa sawa kutofautiana idadi ya vifaranga. Ndiyo, mabwawa yenye ukubwa sawa yanaweza kutofautiana idadi ya vifaranga. SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA KUTOFAUTIANA KWA IDADI YA VIFARANGA NI KAMA ZIFUATAVYO:

I. Aina ya mfumo wa ufugaji.

Katika ufugaji samaki kuna
A) Ufugaji wa samaki peke yake bila kuchanganya na shughuli nyingine kama ufugaji wa kuku au ng'ombe na ufugaji wa samaki wenye kuchanganya na shughuli nyingine kama ufugaji wa kuku au ng'ombe katika eneo moja.

Tafiti zimeonesha kwamba ufugaji wa samaki ukichanganywa na ufugaji labda wa kuku ambapo kinyesi cha kuku kinatumika kuongeza uzalishaji wa chakula cha asili ndani ya bwawa la samaki kunapelekea kuweza kuongeza idadi ya samaki wanaoweza kufugwa katika bwawa ukilinganisha na ufugaji usiochanganya mifugo.

B) Ufugaji wa samaki kulingana na malengo ya mfugaji yaani mfugaji amekusudia kufanya ufugaji wa biashara au wahali ya kawaida tu. Maamuzi haya yataathiri mtazamo na jitihada za mfugaji katika kuliendesha bwawa lake husisani katika suala zima la CHAKULA. Kwa ujumla hapa kuna namna tatu za ufigaji samaki nazo ni

*Ufugaji wa kawaida (subsistence farming or extensive farming)
Ufugaji huu unasifa kubwa moja nayo ni kuwaacha samaki wategemee CHAKULA CHA ASILI kwenye bwawa. Kutokana na upatikanaji wa chakula cha asili kuwa mgumu kwenye bwawa, aina hii ya ufugaji humuwezesha mfugaji kufuga samaki wachache sana kutoka na uhaba wa chakula na mara nyingi samaki huitaji muda mwingi kukua ndani ya bwawa.

Ufugaji huu unamruhusu mkulima kufuga samaki 3 KWA KILA MITA MOJA YA MRABA au chini ya hapo kulingana na uwezo wa bwawa kutengeneza chakula cha asili. Pia ufugaji huu huwa hauna tija kubwa kwa mfugaji

*Ufugaji wa kiwango cha kati ( semi-extensive or semi-intensive farming )
Aina hii ya ufugaji ni ile ambayo mfugaji anajishughulisha kuwapatia samaki chakula cha ziada (supplementary feed). Kwahyo hapa samaki watakuwa wanakula chakula cha asili kinachozalishwa kwenye bwawa na chakula cha ziada anachowapa mfugaji hivyo kupelekea samaki kukua kwa haraka zaidi kuliko kasi ya ukuaji katika ufugaji wa kawaida. Ufugaji huu pelekea kuongezeka kwa uwezo wa bwawa wa kukuza vifaranga mpaka kufikia kati ya VIFARANGA 4-7 KWA KILA MITA MOJA YA MRABA ya bwawa. Ufugaji huu unakuwa na tija ya wastani kwa mfugaji.

*Ufugaji wa kiwango cha juu (intensive farming)
Ufugaji huu unasifa moja kuu ambayo utegemezi wa samaki wa mahitaji yao yote ya chakula kutoka kwa mfugaji. Aina hii ya ufugaji hutumia pesa nyingi sana kuwekeza ili kuleta faida kubwa zaidi (unmatched investment for unmatched production). Teknolojia inayo tumika hapa pia huwa ni kubwa sana. Samaki huwa wanalishwa chakula chenye virutubisho vingi zaidi ili kuwafanya wakue ndani ya muda mfupi zaidi.

Aina hii ya ufugaji inatija kubwa sana kwa mfugaji na humuwezesha mfugaji kuwa na uhakika wakusambaza samaki mwaka mzima. IDADI YA VIFARANGA HUZIDI 8 KWA KILA MITA MOJA YA MRABA.

C) Ufugaji wa samaki wa aina moja (monoculture) na ufugaji wa samaki mchanganyiko (polyculture)
Ufugaji wa samaki aina ya Tilapia kama sato unachangamoto kubwa moja ya samaki kuzaliana kwa wingi kwenye bwawa hivyo kupelekea samaki kuzidi uwezo wa bwawa wa kukuza samaki hali hii hupelekea samaki kudumaa au kuchukua muda mwingi sana kukua kifikia kiwango cha sokoni (market size) kwahyo njia mbadala huwa kufanya ufugaji mchanganyiko ambapo tilapia na kambale huchanganywa kwenye bwawa moja. Kwa kawaida bwawa huanza kwa kuwekwa tilapia kisha baada ya yakriban mwezi mmoja na nusu huongezewa vifar

anga vya kambare (catfish). Kutokana na tabia ya kambare yakula karibia kila kitu hapa tabia yake hutusaidia katika kula vifaranga vitakavyozaliwa hivyo kufanya idadi ya samaki ndani ya bwawa kunakia kwa wastani ile ile. Ikumbukwe kuwa idadi ya tilapia katika ufugaji huu huwa ni mara 3 ya idadi ya kambare yaani uwiano wa kambare na tilapia huwa 1:3 respectively.

II. Jinsia ya samaki
Jambo jingin linaloweza kuathiri idadi ya vifaranga kwenye bwawa ni jinsia ya samaki wanaofugwa. Kwa kawaida ufugaji wa samaki mchanganyiko hupelekea samaki kuzaliana na kusababisha ushindani wa chakula. Hivyo basi ufugaji wa samaki madume tupu mara nyingi hupendelewa. Madume yanasifa yakukua haraka kuliko majike. Kutokana nakutokuwa na mazaliano samaki wa jinsia moja (mono-sex) huweza kukaa wengi zaidi kwenye bwawa moja kuliko kiwango cha samaki katika hali ya kawaida.

Pamoja na taarifa hizi bado ni muhimu kupata ushauri wakina kutoka kwa mtaalamu wako kabla hujaamua kujiingiza katika ufugaji wa samaki moja kwa moja.

Tukutane tena wakati mwingine By Martin Mhina Fuga kibiashara

6. JE NAWEZA KUFUGA SAMAKI HUKU NIKIWAPA CHAKULA CHA KISASA KAMA CHAKULA CHA ZIADA NA BADO SAMAKI WAKASHINDWA KUFIKIA UKUBWA WAKULIDHISHA?

Kutokana na ufugaji wa samaki kuwa jambo geni katika jamii nyingi za kiafrika, sekta hiyo pia bado haijaendelea kufikia kiwango cha kulidhisha kama ilivyokatika ufugaji mwingine. Swala la upatikanaji wa chakula bora kwa gharama nafuu bado ni changamoto! Na pale kinapopatikana basi huwa kinauzwa kwa gharama kubwa kutokana na uwepo wa watu wanaotumia mwanya huo kujipatia pesa "kiulaini ". Hili ni jambo ambalo linaweza kutatuliwa kiurahisi kama wafugaji wa samaki wataweza kuanzisha vyama vyao vya ushirika ili kuweza kuweka nguvu ya pamoja kwenye kutatua changamoto zinazo wakabili lasivyo tutaendelea kuwanufaisha wafanyabiashara wachache wanaotuuzia chakula kwa gharama isiyo linganishi!

Pamoja na changamoto hiyo lakini bado kumekuwa na tatizo kubwa la uzingatiaji wa kanuni za ulishaji samaki kwa kiwango sahihi kwenye mabwawa pale mtu anapoweza kumudu gharama hizo.

Kwa kawaida nimekuwa nikipata malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafugaji wakilalamika kuwa wameuziwa mbegu feki za samaki yaani hazikui kufikia kiwango cha hitajio la soko kwa muda husika. Baada yakuamua kulifuatilia suala hilo kwa kina ndipo nilipokuja kugundua kuwa wafugaji wengi hawazingatii taratibu za ulishaji. Wengiwao WANAWALISHA SAMAKI WAKUBWA CHAKULA CHA VIFARANGA (hivyo wanashindwa kunenepa). Na WANAOWAPA CHAKULA CHA KUNENEPESHEA HAWAWAPI KWA KIWANGO SAHIHI!!!! Unaweza kuta samaki badala yakupewa kilo sita za chakula kwa siku samaki wanapewa kilo moja mpaka moja na nusu. Sasa huyo samaki kama huko kushiba hashibi vipi atanenepa?

Kitaalamu samaki anatakiwa ale 10% ya uzito wake kwa siku. Na ndyo maana inashauriwa kuwapima samaki wako angalau baada ya miezi mitatu ili uje kama kiwango cha chakula unachowapa ni sahihi.

ILIKUWEZA KUJUA KIWANGO CHA CHAKULA CHAKUWALISHA SAMAKI FANYA IFUATAVYO:

Kwa bwawa lenye samaki 1000 na kila samaki baada ya miezi mitatu amefikia 120g

Samaki anakula 10% ya uzito wake kwahiyo kila samaki atakuwa anakula 12g.

Kwasamaki 1000= 12g*1000=12000g=12kg/siku

Mlo huo ili ulike vizuri inashauriwa uwalishe mara tatu kwa siku.

Pia unaweza kupunguza kiwango cha chakula cha kisasa kwa kuwalisha samaki mboga za majani kama spinach.

Usipozingatia lishe bora ya samaki hata mbegu iwenzuri namna gani huwezi kuza samaki ndani ya muda mfupi na wakafikia hitajio la soko.

Mpaka wakati mwingine tena Fuga kibiashara By Martin Mhina

SOMO LA SABA
7. JE KUNA TOFAUTI GANI KATI YA UFUGAJI WA KAMBALE NA SATO (TILAPIA)?

Kabla hatujaangalia tofauti zilizopo kati ya ufugaji wa kambale na tilapia kwanza tujikumbushe sifa chache zinapaswa kuzingatia kabla hauja chagua aina ya samaki wakufuga. vifuatazo ni baadhi ya vigezo vyakuzingatia wakati wakuchagua aina ya samaki wakufugwa:

1. Ukuwaji wa haraka
2.upatikanaji wa chakula bora
3. Kuhimili magonjwa
4. Mvuto wa samaki
5. Utamu
6. Kuwahi kukomaa
7. Uwezo mkubwa wakuzaliana
8. Uwezo wakustaamili aina nyingi za mazingira
9. Urahisi wakuzalisha na kulea vifaranga
10. Aisiwe na tabia ya kula aina nyingine na awe mpenzi wa kula chakula aina ya mimea
11. Itajio kubwa la soko na
12. Uwezo wakuishi na samaki aina nyingine.

Tunapoongelea tofauti kati ya ufugaji wa kambale na tilapia kwanza tuelewe samaki hawa wametofautiana kwenye sifa moja kubwa ambayo ni UWEZO WA TILAPIA KUZALIANA WENYEWE KWENYE BILA MFUGAJI KUWAINGILIA KATI WAKATI KAMBALE HAWAWEZI KUZALIANA WENYEWE WAKIWA KWENYE BWAWA. Jambo hili huwafanya kambale wabakie kwa idadi ile ile kwenye bwawa ambayo utawaweka (kama hakuna atakae kufa ) tofauti na tilapia ambao wanaweza kuzaliana na kuwa wengi kwenye bwawa!
Kuto kuweza kuzaliana kwa kambale kwenye bwawa kunaweza kuwa ni changamoto kwa mfugaji kwani atalazimika kila mara kununua vifaranga wapya baada ya kuvuna na kama sehemu aliyopo kuna uhaba wa vifaranga ufugaji unaweza kuwa mgumu. Kwa upande mwingine kutokuzaliana kwa kambale kwenye bwawa kuna wafanya wawetumia chakula chao karibia chote kwenye kujenga mwili hivyo kuwafanya wawe na uwezo wa kukuwa haraka mno kuliko tilapia ambao chakula hugawanywa kwaajili ya kuzaliana na kujenga mwili.

Tofauti nyingine kubwa kati ya kambale na tilapia ipo kwenye maumbile hususani mfumo wa upumuaji. Ukiangalia matamvua ya kambale utaona yapo kama maua fulani hivi tofauti na matamvua ya tilapia. Hali hiyo humfanya kambale aweze kuvuta hewa kavu na hewa ya kwenye maji. Na ndyo maana kambale anaweza kukaa nchikavu ukiwa umemvua hata masaa kumi na mbili inategemea na ukubwa wake. Pia jambo hili huwawezesha kambale kujichimbia chini kipindi cha kiangazi huku wakisubiria msimu mwingine wa mvua. Sifa hii yakimaumbile huwawezesha kambale kuvumilia mazingira magumu zaidi kuliko tilapia hivyo kumuwezesha mfugaji kuweza kuweka kambale wengi zaidi kwenye bwawa kuliko tilapia.

Tukiangalia kwa ujumla vigezo vyakuchagua samaki tunakuta kambale anachangamoto yakutokuwa na mvuto wa kimuonekano kwa walaji wengi hivyo kupelekea kufugwa na watu wachache kulingana na eneo na kutokuwa na soko kubwa kama tilapia. pia kambale wanatabia ya kula samaki wengine kama tilapia hivyo mfugaji inabidi awe makini sana kama atakusudia kuwa changanya samaki hawa kwenye bwawa moja.

kwa ufupi hizo ni tofauti chache zilizopo kati ya samaki aina ya kambale na samaki aina ya tilapia (sato)

Mpaka hapo siku nyingine FUGA KIBIASHARA By Martin Mhina
 
jambo moja Rahisi sana kwako juu ya mabwawa ya Uvuvi ni kwa wewe kuwasiliana na Idara ya Uvuvi kitengo cha ufugaji viumbe kwenye maji pale Vertinary Temeke, Wizara ya maendeleo ya Uvuvi na Mifugo watakuelimisha vyema maana wao wamesome hayo mambo kwa kina, wanauzoefu wa miaka mingi, watakushauri na mbegu ya kupanda .....kama upo Morogoro nenda kule Kingorwila wanakituo chao pia.

Ha Muji,
 
wazo zuri sana kufuga samaki kibiashara.
Mwaka jana nilianza utafiti jinsi ya kufuga,nashauri uende kunduchi,kuna kitengo cha ufugaji samaki,pia nina rafiki yangu ambaye ni mtaalamu wa samaki,ni PM ntakupa namba yake,na mpange jinsi ya kuonana awe anakupa ushauri.

Fuga samaki wa ziwa victoria-Sato etc kwani wateja ni wengi na pia utakuwa na gharama ya usafiri from kibaha to DAr,
wish u all the best in ur project
 
Kuna wakati nilieleza kuwa nilihudhuria semina ya ufugaji wa samaki kwa kweli nami nilivutiwa sana na waalimu ambao walikuwa wanatoa mada. Kweli kama mtu unataka kufanya biashara ya samaki lazima kweli uwe umedhamiria sana na kuipenda biashara hii (INTEREST).

kwani kama unataka kufuga samaki angalia mazingira yako kama ulivyosema.Umesema kuna maji mengi tu na ninaamini kuwa yanatuama ndio maana ulipochimba wakati wa kiangazi hayakukauka.kwa maana nyingine hapo kwenye eneo lako kuna udongo wa Mfinyanzi ambao unafaa sana kwa kilimo hiki cha samaki.Japo pia unaweza kulijengea vema tu cement na kwa utaalamu bado ukafuga.

Lakini pia unaweza kutengeneza bwawa lako katika vyanzo vya maji vya uhakika kama vijito,chemichemi au mifereji.Pia kwenye udongo unaofaa,eneo lenye mwinuko wa wastani pia lililo karibu na unakoishi kwani bwawa lako linatakiwa kuwa karibu na wewe ili uweze kulilinda na pia kuliangalia kwa namna nyingi kama kulisha chakula n.k pia liwe kwenye eneo lenye miti ili kuleta kivuli.

Hii ni kwa manufaa ya wengine. Kuna umuhimu sana wa kuhudhuria semina hizi zinazotolewa kwani Zinajenga sana na unaendelea kuwasiliana na waalimu wako siku zote.Hawa Africa Upendo Group ndio wanaoendesha semina hizi.kuna njia za kupima udongo kama unafaa.Pia kabla ya kuweka samaki unapaswa kurutubisha bwawa lako vema. yaani liwe na vyakula vya asili vya utosha.unarutubisha kwa kutumia vitu mbalimbali kama mbolea mimea n.k baada ya muda unaweza kupanda vifaranga vyako na kuwapa chakula na mbolea na kuleta ile rangi nzuri ya kijani katika maji na hewa.Samaki anakula vyakula vya kawaida sana ambavyo vinapatikana kirahisi na nikidogo tu bila gharama yoyote kubwa.Hata wadudu bado ni chakula kwao.

samaki hawatakiwi kuwekwa kwenye kina kirefu sana ni kama mita moja tu kwenda chini na inategemea unataka ukubwa gani kama 10 kwa 10 wanaweza kukaa hata samaki elfu kumi hata laki kutegemea na aina ya samaki.Nile-Tilapia ni mbegu nzuri sana kwa biashara hasa ukinzingatia leo kuwa wengi wa wafanya biashara hasa mahotelini wanahitaji gramu 250 ukiwa ndicho kipimo kizuri kwa wateja wengi katika mahotel.utalamu wa kufuga Cat fish au kambale ni tofauti sana kwani wale wanaishi ardhini na huzaana sana wakati wa mvua na mafuriko.Hwazai kabisa kama utawafuga kama hawa samaki wengine.
 
Yaani kambale ni samaki mtamu ajabu Malila umesema.Yaani usipime.

Umenikumbusha pasaka nilienda kwetu toka nimefika hadi naondoka ni supu ya asubuhi chakula cha mchana ama jioni lazima kambale pia awepo pembeni tena ukimpata mwenye mayai yake yaani we acha tu.Tulikula na ndugu zangu hata Nyama haikupata soko sana pasaka hii ni siku ile tu ya jumapili pilau kwa sana.

Ninachozungumzia hapa ni ufungaji wake na maongezeko kuzaliana ndio tatizo.Wanazaa sana na watoto wanatawanyika ama kufa kwa wingi wao lakini bado wanazaa sana.

Cha msingi ni kuwafahamu vema na jinsi ya kuwafunga kutegemeana na Mabwawa uyawekeje ili wazaane
 
Yaani kambale ni samaki mtamu ajabu Malila umesema.Yaani usipime .Umenikumbusha pasaka nilienda kwetu toka nimefika hadi naondoka ni supu ya asubuhi chakula cha mchana ama jioni lazima kambale pia awepo pembeni tena ukimpata mwenye mayai yake yaani we acha tu.Tulikula na ndugu zangu hata Nyama haikupata soko sana pasaka hii ni siku ile tu ya jumapili pilau kwa sana.

Ninachozungumzia hapa ni ufungaji wake na maongezeko kuzaliana ndio tatizo. Wanazaa sana na watot wanatawanyika ama kufa kwa wingi wao lakini bado wanazaa sana.Cha msingi ni kuwafahamu vema na jinsi ya kuwafunga kutegemeana na Mabwawa uyawekeje ili wazaane

Nimetangaza bingo kwa machalii fulani kwamba mtu akiniletea kambale hai hata kama ni mdogo vipi nampa buku tano. Nawatafuta sana hawa samaki. Nimepata sato ila kambale bado. Mategemeo ni makubwa,nikishindwa kuwapata mitaani, nitawafuata mbegani, wapo kule.
 
Shukurani Muanzisha mada, hii mada ni nzuri sana.

Mimi nilitaraji huu wakati hii serikali inaubiri ''kilimo kwanza'' ndio tungekuwa tunapata Makala mbali mbali za kilimo,ufugaji wa wanyama,samaki.lakini wapi TV lao la TBC ni siasa na redio zao zote ni siasa tu ili CCM ishinde. Ukienda kwenye chuo cha kilimo akuna ata sehemu unaweza pata makala za kilimo na ufugaji,yani mambo ayapo kama inavyotakiwa kwa kilimo kwanza.

Mimi nilitarajia wizara ya kilimo itakuwa ata na makala moja kila week kwenye magazeti yote kwa ajili ya kuamasisha na kufundisha watu juu ya kilimo lakini amna same to wizara ya Magufuli amna kitu. Wengine tunapenda kufuga lakini atuna elimu hiyo sasa aka kaela tulikonako kadogo tunaogopa tusijekingiza kwenye ufugaji ikala kwetu.:sick:
 
Mkuu unaendeleaje na samaki kama ulivyoelezea hapo juu. Nimevutiwa sana na moyo wa kushare na wengine vitu vyako.. it is so positive

Nisamehe sana,nilikuwa vijijini kwa muda mrefu kidogo kwa ajili ya mambo yetu haya ya kilimo. Miezi mitatu iliyopita niliweka sato 26 vifaranga,mpaka jana tumerecord sato mmoja kafa,kwa hiyo imenipa nguvu kwamba bwawa langu liko mahali sahihi kabisa kilichobaki ni maboresho,hasa aina ya chakula.

Mwezi juni nilipata Kambale 52,nimewaweka ktk visima vidogo,huku nasubiri bwawa jipya likae sawa,yaani lijijenge kupokea wageni. Kwa mwezi mzima sasa hakuna kambale aliyekufa. Nitakwenda Mbegani/ kunduchi nikachukue shule zaidi ili nifuge kwa wingi. Hapo nitapata mbegu ya kuuza. Mwaka jana kigogo mmoja alikosa mbegu ya kambale,tulitafuta sana bila mafanikio.

Pili,pale Kinguruila gerezani pana mbegu ya samaki inauzwa kwa bei nzuri sana,kifaranga kimoja Tsh 30/ sio 300 kama huku Mkuranga. Contact za mhusika nimepata,kwa aliye tayari aniambie nimpe.

Kwa ujumla ninafurahia kufaulu mtihani wa kwanza,yaani pilot trial niliyofanya.
 
Nimefurahi sana kupata changamoto na wadau katika sekta hii,Kwanza kabisa kuna vitu vya kuzingatia katika utengenezaji wa bwawa.

1.Aina ya Udongo lazima uwe wa Mfinyanzi
2.Maji means uhakika wa maji
3.Sehemu yenye muinuko kidogo
4.Mimea iliyozinguka eneo lako sbb kama kuna miti mingi ndege watakusumbua
5.Njia za mawasiliano means barabara ukizingatia hiyo ni bidhaa inayoharibikia haraka zaidi

BWAWA UNAWEZA KULICHIMBA LENYE UKUBWA TOFAUTITOFAUTI KULINGANA NA UKUBWA WA ENEO HUHUSIKA NA ENEO LAKO LILIVYO,ILA UNASHAURIWA KUCHIMBA BWAWA LENYE UMBO LA MSTATILI

Ni vyema ukamtafuta mtaalamu wa maswala ya uvuvi Makao makuu DSM,NA MIKOANI PIA WAPO WATAALAM WA UVUVI ili uambatane naye kwenye eneo husika sbb vipimo vitabadilika kulingana na eneo.

USHAURI HYUWA NI BURE HAKUNA GHARAMA YOYOTE SSB HILO NI ENEO LAKE LA KAZI
 
Nashukuru kwa msaada wa material hizi, ni lazima tubobee ktk shughuli hizi lakini tukiwa na maarifa na elimu juu ya jambo tunalotaka kubobea nalo. Natumia makala hizi kurekebisha makosa madogo madogo ya kazi ambazo mimi nimefanya tayari na jamaa zangu nitawasaidia wasifanye makosa ( kwa mfano,kujua shughuli za jirani yako ili zisije kukuharibia quality ya samaki nk).

Kabla hatujaingia ktk ujenzi wa bwawa ni vizuri pia utuambie aina ya samaki unaotaka kuwafuga ndugu( Nile perch,Tilapia, kambale, sato, kitoga au blackbassa) Kuna samaki hawataki matope wanataka clear water na wengine wanaweza kuishi ktk tope, pili lazima ujue PH ya hapo unapotaka kujenga bwawa,vinginevyo utajenga na samaki hawatazaliana. Angalia udongo wenyewe kama una capilarity kubwa au la.

Mwisho ni kwamba angalia aina ya samaki unaotaka kuwafuga growthrate yake ikoje na mwisho ni soko la samaki hao. Ukikamilisha utafiti huo rudi tukupe nondo mkuu.
 
Mkuu, tupo wote kwenye ukulima. Nimepata eneo kubwa linaofaa sana kwa ufungaji wa samaki, lipo kijiji cha Mwanzo Mgumu, nipo kwenye matayarisho, nikianza nitakutafuta. Bado nina wasiwasi kama tunao wataalamu wa kilimo cha samaki, kama wapo uzoefu utakuwa ni mdogo kwani hakuna wafugaji wakubwa.

Watalaam wapo kibao,ila wanakaa ofisini tu. Wengine wapo pale Temeke ofisi za kilimo,wengine Kunduchi chuoni pale, wengine wapo pale Kinguluira magereza ( hawa hata mbegu wanayo), wengine wapo SUA morogoro.

Mwanzo mgumu si baada ya kupita Chanika kwa mbele kidogo unaingia kushoto unaiacha njia ya kwenda Nzasa? Ni maeneo mazuri sana kwa kilimo. Mimi niko Marogoro/Mfuru mwambao/Msorwa.

Ni vizuri tukiwa na utamaduni wa kutembeleana,unaweza kujifunza zaidi kwa kuona wengine wanafanya nini. Nitakwenda Kinguluira kufuata mbegu ya pelege.
 
Mkuu Malila, hongera sana. Napenda sana mindset yako... najitayarisha, nikiwa tayari nitakutafuta.

Hii nchi ni ya ajabu sana,

week jana nilikwenda ktk kituo cha elimu ya ufugaji samaki Kinguruila sio chuo cha samaki pale SUA, kipo kinguruila. Wapo wataalamu wa kutosha vibaya,elimu bure. Nilitumia muda wa saa sita hivi pale kituoni. Nikanunua na mbegu ya kambale Clarius hybrid. Kituo kina aina mbili tu za vifaranga.sato na kambale. Jamaa ni wakarimu hadi raha.

Ila vifaranga vya Kambale ni haba sana kwa sababu vinasakwa na wengi, mimi nilitaka kununua vyote,wakanikatalia, ikabidi niwaachie kidogo. Vinginevyo ufugaji wa samamki uko vizuri,nilikutana na mkulima mmoja toka Maneromango,yy alinunua vifaranga 500 aina ya sato.
 
Malila

Asante kwa taarifa, Kinguruila kama sikosei ipo Morogoro lakini sikumbuki ni katika barabara ya Iringa au Dodoma. Santo ni aina ya samaki ambaye anakuwa kwa kasi ya ajabu na wanapatikana kwa wingi sana kwenye mto Kilombero.

Kinguluira iko Morogoro barabara ya Dsm, ukishapita Moro junior Seminary kama unakuja DSM toka Moro,kuna kimji kinafuata, unapomaliza kimji kushoto na kulia yanaanza mashamba ya mkonge. Sasa linapoanza shamba la kushoto kwako kuna njia inaingia kushoto na kuna kibao kimeandikwa kituo cha samaki au uliza wale madogo wa pikipiki,kwamba nataka kwenda FAO, ni buku moja kwa pikipiki.

Niliahidi huko nyuma kuwa nitatoa feedback ya jaribio la ufugaji. Nilianza jaribio may 2010, na sasa ni miezi sita imefika. Niliwaweka sato ktk fishpond isiyo na outlet wala inlet. Wamekuwa na kufikia kiwango cha kuliwa na wamezaliana vizuri sana.

Pamoja na kwamba nilipata darasa la kutosha toka Kinguluira,sikubadilisha mazingira ya bwawa lile. Desemba nitakwenda Kinguluira ili nichukue mbegu bora na nifugie ktk mazingira yanayokubalika kitalaam, lakini bwawa lingine nitaendelea kutumia mbegu niliyozalisha pale kwangu ili nione matokeo baada ya miezi sita mingine, hawa ni sato sio Kambale.

Nawatia shime,mwenye nafasi afuge samaki, mbegu zipo nyingi.
 
niliwahi kusikia kwamba unatakiwa kupanda samaki wawili kila mita 1kwa 1mean kwa mita 10 unatakiwa upandikize samaki 20 je mpaka unakuja kuvuna ikiwa utafuata ushauri wa kitaalamu unaweza kuvuna samaki wangapi?

Na je eneo lenye mchanganyiko wa mfinyanzi na kichanga linafaa?
 
je? Bwawa la cement halifai.na je hao samaki wakufugwa wanachukua muda gani mpaka kufaa kuvuliwa?
 
je? Bwawa la cement halifai.na je hao samaki wakufugwa wanachukua muda gani mpaka kufaa kuvuliwa?

Samaki wa biashara mara nyingi hufikia market size ktk kipindi cha miezi sita (sato zaidi). Kimsingi unatakiwa kuangalia ukuaji wa samaki wako kila wakati ili wafikie market size, sato wanaweza kufikia size hiyo bila taabu sana ukilinganisha na kambale, nikipata muda wa kambale nitauweka hapa. Kama unafuga kwa matumizi binafsi,size inayopendeza macho yako ndio nzuri.


Bwawa la saruji unaweza kulitumia kwa kufugia samaki pia,lakini sharti uwaone watalaam ili wawe na wewe kuanzia ktk hatua za ujenzi. Kumbuka virutubisho toka ardhini haviwezi kuwafikia samaki kirahisi kupitia kuta za saruji.
 
Samaki wa biashara mara nyingi hufikia market size ktk kipindi cha miezi sita (sato zaidi). Kimsingi unatakiwa kuangalia ukuaji wa samaki wako kila wakati ili wafikie market size....
Nilishakuwa na plan ya kufuga samaki ila nikawa nashindwa kufahamu costs involved na hata ivo sikuwa vyema kibajeti ingawa shamba la kuweza kufanyia hiyo buisness lipo.

Eneo langu ni shamba la kawaida lakini vilevile lina bonde ambalo maji huwa yanatiririka seasonally hasa masika. huwa nalima mpunga katika bonge hili na wakati wa masika kwa kweli maji huwa yanafurika sana ingawa mvua zinapoisha, kiasi cha maji hupungua na kubakia kama vijisima vidogovidogo.

Swali,..Je naweza kutengeneza fish pond katika eneo la namna hiyo? I mean humohumo bondeni au niweke hiyo fish pond pembeni kidogo ya hilo bonde ingawa slope inakaribia 5%. vilevile eneo hilo hakuna source ingine ya maji zaidi ya hicho kijibonde ambacho ni seasonal ingawa ukichimba unaweza kupata plenty of water kwa chini. Ni feasible kuweza kutumia maji ya ku-pump kutoka ardhini kwa kutumia waterpump?

Naombeni ushauri katika hili,....JF is great.....
 
Nilishakuwa na plan ya kufuga samaki ila nikawa nashindwa kufahamu costs involved na hata ivo sikuwa vyema kibajeti ingawa shamba la kuweza kufanyia hiyo buisness lipo. Eneo langu ni shamba la kawaida lakini vilevile lina bonde ambalo maji huwa yanatiririka seasonally hasa masika. huwa nalima mpunga katika bonge hili na wakati wa masika kwa kweli maji huwa yanafurika sana ingawa mvua zinapoisha, kiasi cha maji hupungua na kubakia kama vijisima vidogovidogo.

Swali,..Je naweza kutengeneza fish pond katika eneo la namna hiyo? I mean humohumo bondeni au niweke hiyo fish pond pembeni kidogo ya hilo bonde ingawa slope inakaribia 5%. vilevile eneo hilo hakuna source ingine ya maji zaidi ya hicho kijibonde ambacho ni seasonal ingawa ukichimba unaweza kupata plenty of water kwa chini.

Ni feasible kuweza kutumia maji ya ku-pump kutoka ardhini kwa kutumia waterpump?

Naombeni ushauri katika hili, JF is great.
 

Similar Discussions

34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom