Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Nataka kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki hasa mkoa wa Dodoma. Najua kuna changamoto ya maji lakini naomba ushauri, maji yenye chumvi kidogo yanafaa kufuga samaki.

Nataka kuchimbwa bwana pia, naomba minimum estimates za kutengeneza just a local pond kwa ajili ya samaki (Sato) 1,000 au kambale 500
Maji yenye chumvi kidogo hiyo yanafaa kwa ufugaji, ni kama maji ya wafugaji wangu wa wilaya ya Same maji ni ya chumvi kiasi, lakini samaki wanakua tu.

Hao sato 1000 unafuga kibiashara au kwa ajili ya matumizi ya nyumbani?
ili kujua gharama halisi ya bwawa ni lazima mtaalam auhusike, ili kuona je udongo wako una hitaji aina ipi ya bwawa, kulingana na budget yako mkuu.
 
Bei zimechangamka sana. Nilipata powder Mwanza 43000/= mfuko wa kilo 10. Jumlisha usafiri 5000/=

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngoma ndio huwa iko hapo, japo kitaalam vyakula vya kiwandani vinafanya vizuri sana kwa samaki.

Unaweza kutengeneza hata Local fish foods, kwa kutafuta mchanganyiko wa materials kutoka kwa wataalam mbalimbali.
 
Mimi ningependa kujua mikoa gani inajihusisha na fisheries most??

bee keeping???

Forestry??

livestock keeping?

msaada wadau,nimegoogle naona research za watu tuu..hakuna jibu la moja kwa moja
 
Ngoma ndio huwa iko hapo, japo kitaalam vyakula vya kiwandani vinafanya vizuri sana kwa samaki,
Unaweza kutengeneza hata Local fish foods, kwa kutafuta mchanganyiko wa materials kutoka kwa wataalam mbalimbali.
Uko sahihi. Ila nataka wakiwa wadogo angalau niwape formula ya kiwandani kwa mwezi mmoja halafu ndio nianze kutengeneza mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimetangaza bingo kwa machalii fulani kwamba mtu akiniletea kambale hai hata kama ni mdogo vipi nampa buku tano. Nawatafuta sana hawa samaki. Nimepata sato ila kambale bado. Mategemeo ni makubwa,nikishindwa kuwapata mitaani, nitawafuata mbegani, wapo kule.
Mkuu kambale ninao Tena wako live wako wengi Sana mmoja ntakuuzia buku jero Ni wakubwa Sana sema unahitaji wangapi shamba linapatikana Mkata -Tanga 0657999034
 
Mimi ningependa kujua mikoa gani inajihusisha na fisheries most??

bee keeping???

Forestry??

livestock keeping?

msaada wadau,nimegoogle naona research za watu tuu..hakuna jibu la moja kwa moja

Fisheries kwa maana ya ufugaji was kwenye mabwawa ya kuchimba?
Mikoa ya pwani, ruvuma, mwanza
Bee keeping mikoa mingi ila maarufu ni tabora na singida.

Forestry Kuna misitu asili na ya kupanda, mikoa ya nyanda za juu kusini, Tanga.

Livestock keeping kwa wingi ni mikoa ya kaskazini, kanda ya ziwa pia
 
Hodi humu wadau.
Nataka kuingia kwenye ufugaji wa samaki aina ya sato.
Eneo ninalo la kutosha, ni uwezo wangu tu wa kutengeneza mabwawa.
Maji ninayo, nimechimba kisima kwa kutoboa kwa mtambo (drill).

Naomba ushauri kwa kuanzia nikitaka kuchimba mabwawa mawili, kila moja litakuwa na ukubwa wa 250m[SUP]2 [/SUP](urefu mita 10 na upana mita 25). Jumla mabwawa mawii yatakuwa na ukubwa wa mita za mraba 500. nitahitaji mtaji wa shs ngapi kwa ajili ya kuchimba hayo mabwawa mawili, kujengea, kuweka fence kuzuia nyoka, ndege, vyura, kenge na wadudu wengine waharibifu. Ningependa kupata picha kamili at least hatua ya mabwawa hayo kukamilika ujenzi ninahitaji mtaji wa sh ngapi kwa makadirio.

Nikikamilisha nitaenda awamu ya pili kutafuta bajet ya vifaranga na chakula, hainiumizi akili hiyo.
 
Weka estimate bwashee
Mkuu ukiulizwa uko mkoa gani sio vibaya, ujue kwenye kumpigia mahesabu ya uchimbaji wa mabwawa mtu sisi kama wataalam wa samaki kuna vitu huwa tunaangalia.

mfano kama ni udongo unaohifadhi maji [ mfinyanzi ] kuna hesabu zake na pia tunaangalia upatikanaji wa vibarua eneo husika ambapo mradi unafanyika.

Kujua mkoa aliopo mdau unarahisisha pia kama mnaweza kuonana ili umshauri macho kwa macho, kuliko haya mambo ya kuandikiwa maelezo.
 
Habarini ndugu zangu Kama heading inavyosomeka hapo juu

Mimi ni kijana wa kiume nimeamua kujitolea kwa yeyote anaetaka kufuga samaki iwe ni kibiashara au kwaajili ya matumizi ya nyumbani anicheki nitamsaidia bure kumshauri au hata kufika eneo analotaka kufugia kwa gharama zake

Nitamsaidia na kumshauri mambo yote yanayohusika na ufugaji kuanzia mwanzo mpaka mwisho .

Lengo-
Ujuzi huu Mimi niliupata mbeya tena bure kwa ufadhili wa serikali yetu ili kuinua uchumi wa wanainchi kupitia ufugaji samaki

Baada ya mafunzo hayo pia nilifanya kazi hio kwa miaka 4 nikapata uzoefu wa kutosha
Baada ya kuondoka mbeya tukapewa darasa la uzalendo na kuinuana

Muda wote sikuwahi kulipa chochote kila kitu nilipata bure

Kwahio Kama unataka au unatamani kufuga samaki na huna uelewa juu ya biashara hio nichek
Nimepewa bure na mimi natoa sadaka kwa wahitaji ili niwe huru kwenye nafsi yangu

0714839251
Karibuni
 
Back
Top Bottom